Mgomo wa madaktari unachochewa na chama Pinzani-Gazeti RAIA MWEMA

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Katika hali ya kushangaza gazeti la Raia Mwema toleo la leo limeripoti kuwa mgomo wa madaktari nchini unachochewa na chama kimoja cha upinzani kikishirikiana na kundi moja ndani ya CCM linalotaka kudhoofisha serikali na kuijengea chuki kwa wananchi.Gazeti hilo limeendelea kuripoti kuwa baada ya njama hiyo kugundulika ndiyo maana wale madaktari wote wenye nia njema wamerejea kazini.
Pia gazeti hilo limesema limepata uthibitisho kwamba kamanda Ahmed Msangi hakuhusika katika tukio la utekaji na mateso kwa Dr Ulimboka Stephen.
Pia katika gazeti hilo kumetolewa Tangazo maalum la serikali la kurasa 2 lenye hotuba yote ya Rais aliyoitoa mwisho wa mwezi kuhusu onyo lake kwa madaktari

Source:Raia Mwema uk 3
------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Soma habari yenyewe hapa chini:
TAKRIBAN wiki moja baada ya kutekwa, kuteswa na kuumizwa vibaya kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka, mmoja wa marafiki zake, Dk. Deogratius Michael (36), aliyeshuhudia tukio la kutekwa amezungumza na Raia Mwema akisema taarifa za baadhi ya vyombo vya habari kwamba ametoweka si za kweli.
"Nasikia kuna redio moja wamesema kwamba mimi sionekani na kwamba nimetoweka. Ukweli ni kwamba nipo. Napatikana na nimekuwa nikiwasiliana na watu mbalimbali. Ushahidi wa hilo ni kama hivi sasa ninavyozungumza nanyi," alisema Dk. Deo jana Jumatano katika mazungumzo na Raia Mwema.
Lakini wakati hayo yakiendelea, taarifa ambazo gazeti hili limezipata zinaeleza kuwa mgomo wa madaktari nchini pamoja na tukio hilo la Dk. Steven Ulimboka, sasa umeingia katika sura mpya baada ya kikundi cha mtandao unaodaiwa kufanikisha ‘kumuingiza' Rais Jakaya Kikwete madarakani kwa mara ya kwanza mwaka 2005, kudaiwa kuhusika kufadhili baadhi ya madaktari kuchochea mgomo huo.
Pamoja na baadhi ya wanasiasa ndani ya CCM kuhusishwa, lakini pia wamo wanasiasa kutoka chama kimoja cha upinzani kinachotajwa kuwa nyuma ya shinikizo la kuendeleza mgomo huo wa madaktari.
Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari, lengo la ufadhili huo, ni kile kinachodaiwa kuwa ni hatua ya kulipa kisasi kwa kuzingatia mwenendo wa siasa ndani ya CCM na ‘panga-pangua' ya viongozi serikalini, pamoja na mikakati ya vyama pinzani kujenga chuki kwa wananchi dhidi ya Serikali.
Taarifa hizo zilizopatikana zinabainisha kuwa pamoja na madaktari kushinikiza uboreshaji wa maslahi yao, sambamba na utoaji wa huduma bora za afya, siasa za visasi ndani na nje ya CCM, zimeendelea kudandia mgomo huo na kuanza kuwafanya baadhi ya madaktari kufikiri upya ushiriki wao katika mgomo huku kukianza kujitokeza wito wa kutaka kurejea katika meza ya majadiliano.
Kujitenga kwa baadhi ya madaktari dhidi ya mgomo huo wa sasa kunathibitishwa na taarifa rasmi iliyotolewa na Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Aligaesha.
 
Kwani hauna ukweli ndani yake mpaka uwe uchochezi?
 
kwa hiyo kila mgomo hapa tz sasa hivi inachochewa na upinzani, kwani upinzani ndio wanawalipa mishahara wafanyakazi wa umma? kuongeza posho za wabunge wanaona sawa, kuongeza entertainment bill ili wageni wawe wananunuliwa vinywaji kutoka million 5 mpaka million 50 wanaona sawa..kuwaongezea mishahara madaktari..inakua issue
 
Katika hali ya kushangaza gazeti la Raia Mwema toleo la leo limeripoti kuwa mgomo wa madaktari nchini unachochewa na chama kimoja cha upinzani kikishirikiana na kundi moja ndani ya CCM linalotaka kudhoofisha serikali na kuijengea chuki kwa wananchi.Gazeti hilo limeendelea kuripoti kuwa baada ya njama hiyo kugundulika ndiyo maana wale madaktari wote wenye nia njema wamerejea kazini.
Pia gazeti hilo limesema limepata uthibitisho kwamba kamanda Ahmed Msangi hakuhusika katika tukio la utekaji na mateso kwa Dr Ulimboka Stephen.
Pia katika gazeti hilo kumetolewa Tangazo maalum la serikali la kurasa 2 lenye hotuba yote ya Rais aliyoitoa mwisho wa mwezi kuhusu onyo lake kwa madaktari

Source:Raia Mwema uk 2

Acha UONGO wewe, uzushi haukusaidii hapa jukwaani,

Elewe kuwa mtu yeyote kuwepo jf amepitia mengi, haina tofauti na kumuona nyani mjini ujue kuwa kakwepa mishale mingi!

Gazeti hilo mimi ninalo hapa tangu saa kumi na mbili asubuhi na nimesoma mpaka matangazo yoooooote hakuna habari hiyo!

Danganya wajinga wenzio wa ccm sio wanajf waliofuzu manuvazi yote!

Mods Ondoeni hii habari ni yakizushi tu!
 
Mbona tuhuma hizo zimetolewa na gazeti la chama tawala vile vile ,UHURU la tarehe 4 Juni , 2012.
Tukienda na facts ukweli utajilikana tu.
Leo asubuhi nilitoa quote hii, ikahamishwa chap chap.

Mgomo wa Madaktari: CHADEMA yahusika

Na Mwandishi wetu.
Hatimaye imebainika rasmi kwa viongozi wa CHADEMA wapo nyuma ya mgomo wa Madaktari uliosababisha baadhi ya wnanchi kupoteza maisha na wengine kuendelea kutaabika.
Kuhusika kwa CHADEMAkatika mgomo huo kunathibitishwa na jinsi wanavyoendesha mikutano ya siri na baadhi ya vinara wa mgomo na mipango mingine kufichuliwa na baadhi ya wabunge.

UHURU imebaini kuwa juzi , madaktari watatu wa jukwaa la madaktari waliwasili mjini Dodoma kwa ndege ya kukodi na kukutana na baadhi ya vigogo wa CHADEMA.
Hiyo ilikuwa ni siku moja baada ya Rais Jakaya Kikwete mkutano(msimamo) wa serikali kuwa haiwezi kuwalipa mshahara wa shillingi milioni tatu kama wanavyotaka na kuwa, anayetaka fedha hizo ajiondoe na kutafuta kazi sehemu anayoweza kulipwa.

Habari za uhakika zinasema madaktari hao walikwenda Dodoma na kukutana na baadhi ya wabunge wa CHADEMA katika hteli ya Desert Palm, saa tatu na nusu hadi saa saba usiku.
Kutokana na kulifanya jambo hilo la faragha, viongozi wamadaktari ambao mmoja ni mtaalamu wa magonjwa ya wanawake na mwingine wa upasuaji(majina tunayahifadhi) walifanya mkutano huo kwenye moja ya chumba cha kulala hotelini hapo.
Baada ya mkutano huo , madaktari hao walisafirishwa kwa siri wakitumia gari aina ya Nissan hadi hoteli ya Dear Mama.

My take:
Wengine tulidhani ni propaganda za Chama Tawala, lakini kutokana na facts zilizotolewa hapa tunaomba CDM wakanushe kama hawahusiki na upotevu wa maisha kwa waTanzania.
Je ni mpango wa CDM kuingia Ikulu by whatever means possible?
Au kufanya nchi isitawalike?
Yote yamekwisha tamkwa hadharani before na ushahidi upo-wananoumia ni wananchi.
(Pls wale maningwa wa matusi humu JF wasubiri tu)
Nwasilisha.
 
Mmekuja na chorus nyingine!
Bado ya walimu mtasema tuuuuuuu!
 
Acha UONGO wewe, uzushi haukusaidii hapa jukwaani,

Elewe kuwa mtu yeyote kuwepo jf amepitia mengi, haina tofauti na kumuona nyani mjini ujue kuwa kakwepa mishale mingi!

Gazeti hilo mimi ninalo hapa tangu saa kumi na mbili asubuhi na nimesoma mpaka matangazo yoooooote hakuna habari hiyo!

Danganya wajinga wenzio wa ccm sio wanajf waliofuzu manuvazi yote!

Mods Ondoeni hii habari ni yakizushi tu!

Hujui unachokisema Gamba la kobe wewe
 
Afadhari umemwambia ukweli, hilo gazeti ninalo hapa wala hakuna hiyo habari!

Huu ni uzushi tu!
 
Mbona tuhuma hizo zimetolewa na gazeti la chama tawala vile vile ,UHURU la tarehe 4 Juni , 2012.
Tukienda na facts ukweli utajilikana tu.
Leo asubuhi nilitoa quote hii, ikahamishwa chap chap.

Gazeti la Uhuru hata kama wanapata support ya CCM wanatakiwa wawe makini sana na wanachoandika. Wanaweza kutumika kueneza propaganda sana lakini hawana uwezo wa kuzima madhara yatokanayo na propaganda hizo.

Kama wana ubavu wataje majina ya hao madaktari wanaosema walienda Dodoma juzi na waseme walionana na nani? Lakini kinachonisikitisha ni tabia ya serikali ya CCM kuamua kufanya siasa na huu mgomo wa madaktari badala ya kutafuta suluhu.
 
Toka mgomo huu ulipoanza, nimekua nikijiuliza maswali mengi kadiri siku ziendavyo. Lazima nikiri kwamba na mimi nilitumbukia katika mtego wa kulaumu upande mmoja wapo kabla ya kujiuliza vizuri... Ama baada ya kutafakari kwa kina, nikagundua kwamba kwa vyovyote vila itakavokua, tunaoathirika ni sisi wananchi, bila kujali tunaunga mkono madaktari au serikali.

Nilianza kujiuliza hivi: Hawa wanasiasa wanaotupiana mpira, mara CHADEMA, mara CCM, bila kujali vyama vyao, wanatibiwa wapi kwa kawaida? Hawa kwani hawana madaktari maalum ambao wanawalipa binafsi? Hivyo basi, huyu kiongozi anayesema fukuza, hakutani na daktari wake binafsi ambaye huenda anatugomea sisi wananchi? Mimi mwananchi wa kawaida ambaye sijuani na daktari na wala sina pesa, nani atanitibia?

Je, nikisema serikali ifukuze madaktari wote, nani atanitibia? Nikisema pia wagome, kwani nikienda hospitali wataniuliza kama nawaunga mkono ili wanitibie? Au ndio yale ya "naunga mkono mgomo", lakini kwa sababu mimi sina jamaa daktari, au sio daktari, basi sina wa kunitibia. Lakini wao wanasema wananisaidia, ilihali wananiacha nateseka na wao wakitibia ndugu na marafiki zao!

Baada ya kuangalia hali yangu na hao viongozi wa siasa, bila kujali vyama vyao, nikajiuliza maswali mengine: Je, miongoni mwa madaktari wanaogoma, hawana wateja wao binafsi ambao ndio hao hao mawaziri wanaowatuhumu kufisidi sekta ya afya? Je, mawaziri hawa wakienda katika clinics zao binafsi wanawagomea? Je, ni kweli kwamba madaktari wote wanaoshiriki mgomo, hakuna hata mmoja ambaye aliwahi kwa njia moja au nyingine kushiriki katika kufisidi sekta ya afya, iwe kwa kuiba panadol au vifaa vya malaki au hata mamilioni? Je, na wao wanahaki ya kusema kwamba wanagoma kwa sababu ya ukosefu wa vifaa?

Sikuishia hapo tu... nikajiuiza tena: vipi sisi wenyewe, ambao tunashangiia au kushabikia ama serikali kufukuza madaktari, au madaktari kugoma: Hakuna miongoni mwetu walioshiriki kuziibia hospitali zetu? Je, ni haki, kwa mwananchi mwenzetu, ambaye naye ameshiriki kufisidi hospitali, kunyoosha kidole, au kushabikia akisema serikali ifukuze, au madaktari wagome, wakati huyo naye ni sehemu ya tatizo?

Bado nikajiuliza maswali zaidi: Hivi tunaposikia serikali na madaktari wameshindwa kuafikiana, tunayachukua hivyo hivyo tu, au tunauliza kwa kina ni kwa nini wameshindwa? Tunaposikia serikali au madaktari wanasema wako tayari kwa majadiliano, tunawauliza ni hatua gani wanazichukua kwa ajili ya majadiliano, wakati upande mmoja unaendelea kufukuza na mwingine unaendelea kugoma? Tunapozikosoa taarifa zao, ni kwa sababu tumeamua kuchukua upande mmoja, au tunajua madhara ya mgomo huo kwetu sisi?

Maswali haya mengi yamenileta katika swai moja muhimu... Sisi wananchi, tusio wanasiasa, wala tusio madaktari au walau na ujamaa na daktari - tumekua tunatoa maoni yenye kuleta suluhu, au yenye kuchochea mgogoro? (bila kujali uko upande gani)

Watanzania wenzangu, katika hili, tunahusika wote. Kwa wale wanaosema madaktari wasigome, wasiishie tu hapo, watafakari sababu za matatizo ya sekta ya afya. Na kwa wale wanaosema wagome, wajiulize swai moja tu: Je, sababu kwamba ukosefu wa huduma bora kwa miaka kadhaa umesha sababisha vifo fingi, ni kisingizio haswa cha mgomo ambao na wenyewe pia unasababisha vifo na mateso?

Mimi na wewe tunafanya nini ili kurudishiwa huduma ya afya? Tuendelee kupiga siasa? au tutoe maoni ya suluhu?
 
mlianza na wanachuo, sasa madr. na tunaelekea walimu, kazi mnayo. hata mimi mimi nikimgomea baba angu kuchunga ng'ombe mtasema tu ni chadema
 
Tanzania yetu hii hivi sasa inachekesha sana. Daktari si mbeba mizigo kwamba utamlazimisha kusomba; nawe utajiridhisha kuwa ametii pale utakapokuta mizigo imetoka point A kwenda B. Huyo anadeal na maisha ya watu; kutompa vifaa stahiki vya kufanyia kazi ni sawa na kumgomesha kutimiza wajibu wake wa kuokoa maisha ya wagonjwa.
Kuwepo kwenye majengo ya hospitali wanaweza kwenda madaktari wote, suala linabaki pale pale Je wanatimiza wajibu wao angalau kwa asilimia 50? Au ndo inabaki ile ya mgonjwa unaingia kwenye chumba cha Dkt kabla hujamaliza kujieleza; jamaa anaita mwingine aingiye na wewe kesha malizana naye kwa kukuandikia dozi ya panadol.
Tafakuri inahitajika kupata suluhi; hii nchi hivi sasa ni kama baberi hakuna anayehitaji kumuelewa mwingine hasa wenye madaraka hofu kwao ni tumbo lao na wenzi wao.
Tafakari
 
Acha UONGO wewe, uzushi haukusaidii hapa jukwaani,

Elewe kuwa mtu yeyote kuwepo jf amepitia mengi, haina tofauti na kumuona nyani mjini ujue kuwa kakwepa mishale mingi!

Gazeti hilo mimi ninalo hapa tangu saa kumi na mbili asubuhi na nimesoma mpaka matangazo yoooooote hakuna habari hiyo!

Danganya wajinga wenzio wa ccm sio wanajf waliofuzu manuvazi yote!

Mods Ondoeni hii habari ni yakizushi tu!
duh!kama ni kweli unalo hilo gazeti na umesoma yote yaloandikwa humo mpaka matangazo yote halafu hujaona hiyo habari basi utakuwa una tatizo kubwa sana...nikupe tu pole.
Labda uombe mtu akusaidie.. Habari yenyewe ina heading.."Aliyemshuhudia Ulimboka Alonga'' uk.1 na habari kamili uk.3.(au labda una raia mwema la kenya labda!!!!)
 
Mkuu nakushukuru sana sana.Kuna watu hapa wanadhani wao ndiyo wenye uwezo wa kuleta habari tu.Mtu mzima bila aibu anasema amesoma gazeti lote na hakuna hii habari.Shame on them!
 
Afadhari umemwambia ukweli, hilo gazeti ninalo hapa wala hakuna hiyo habari!

Huu ni uzushi tu!

Mkuu huwa nakuheshimu sana lakini kwa leo nimekudharau sana.Nikushauri tu acha kusoma vichwa vya habari na kukurupuka kukomenti.Ukitaka hii habari niliyoandika soma taarifa yote ya 'MWANDISHI WETU' Uk 3.Na kama ni uongo Mods wanipe BAN
 
Acha UONGO wewe, uzushi haukusaidii hapa jukwaani,

Elewe kuwa mtu yeyote kuwepo jf amepitia mengi, haina tofauti na kumuona nyani mjini ujue kuwa kakwepa mishale mingi!

Gazeti hilo mimi ninalo hapa tangu saa kumi na mbili asubuhi na nimesoma mpaka matangazo yoooooote hakuna habari hiyo!

Danganya wajinga wenzio wa ccm sio wanajf waliofuzu manuvazi yote!

Mods Ondoeni hii habari ni yakizushi tu!

huyu molemo siyo gamba mkuu!
 
Back
Top Bottom