Mgomo wa kutoa unyumba mpaka barabara ijengwe

Kimbweka

JF-Expert Member
Jul 16, 2009
8,597
1,683
Zaidi ya wanawake 250 wa mji mmoja nchini Kolombia wameanza mgomo wa kuwapa unyumba waume zao ili kuishinikiza serikali iifanyie marekebisho barabara inayoingia mjini humo.
Wanawake katika mji wa Barbacoas wanaamini kwamba iwapo wataanza mgomo wa "kuibana miguu yao" kwa kuwanyima unyumba waume zao, basi waume zao watalazimika kufanya jitihada za kuishinikiza serikali yao kuijenga barabara inayoingia mjini humo ambayo iko kwenye hali mbaya sana kiasi cha kuhatarisha maisha yao.

Kwa miaka 20, serikali iliahidi kuifanyia marekebisho ya barabara hiyo inaoingia kwenye mji wa Barbacoas ambao una jumla ya wakazi 40,000 lakini haijawahi kutimiza ahadi yake, limeripoti jarida la Wall Street Journal.

Hivi sasa inawachukua watu masaa 10 kuweza kusafiri umbali wa kilomita 56.

"Wanawake hawa na watu wote katika mji huu, tumechoshwa na ahadi hewa za serikali", alisema Lucelly Del Carmen Viveros, mtetezi wa haki za binadamu kwenye mji wa Barbacoas.

"Hii ndio barabara pekee inayouunganisha mji wa Barbacoas na miji ya karibu nchini lakini ipo katika hali mbaya sana", aliongeza Viveros.


HII IMEKAAJE WAKUU HASA KWA HALI YA KISIASA TULIYONAYO HAPA KWETU???????????
 
huu uongo mtupu,barabarani tunaongea maneno mia ngoja tufike chumbani ukishikwa mkono tu husemi hata neno moja halafu kesho unatoka unadanganya wenzako .
 
huu uongo mtupu,barabarani tunaongea maneno mia ngoja tufike chumbani ukishikwa mkono tu husemi hata neno moja halafu kesho unatoka unadanganya wenzako .

teh teh teh nimeipenda hiyo duh haya mmmmhh
 
nani ata-audit kuwa mgomo unasimamiwa na wanachama wote? mgomo unahusisha pia nyumba ndogo na zile za biashara?
 
On the contrary wangewapa unyumba mpaka wajisahau kwenda kazini..ama hata wakienda, wanaenda wamechokaa na wanasinzia tu ofisini to the extent uzalishaji unakuwa mdogo...ndipo serikali ingechukua hatua za haraka zaidi!
 
huu uongo mtupu,barabarani tunaongea maneno mia ngoja tufike chumbani ukishikwa mkono tu husemi hata neno moja halafu kesho unatoka unadanganya wenzako .
najitolea kuwakagua kila monii.....nitajua nikikuta kumeloana najua kobosto iliingia
 
Back
Top Bottom