Mgomo mkubwa wanukia Ijumaa

Natumaini watakumbuka kuongelea kwanini wanaendesha vibaya na kukimbiza, kuovateki ovyo bila kujali usalama wa abiria bali kuua tu.

Tena waanze kushtakiwa na kufungwa.
 
ijumaa siyo mgomo ni mkutano wa madereva wote na viongozi wa juu na idara zao za serikali. ila wasipofika hao tunaowahitaji kujibu hoja zetu na kuafikiana basi hapo ndo mgomo utakapoanzia

Sasa kama ni mkutano wa madereva wote huoni tayari ni mgomo? Ni chombo gani cha usafiri kitakua barabarani?
 
Fast jet inahusika hapa kwa safari ya dar mwanza au mbeya kama gari itatembea speed 80 kwa saa, kwa kilomita zaid ya elfu moja huyo dereva baada ya miez michache mgongo utakuwa ushajaa maji na itakuwa unaichosha gari haraka hasa upande wa machine maana bus yenye speed zaid ya mia ishirini kuanza kuitembeza umbali mrefu hivyo na speed ndogo ni kuuwa mashine kiujumla na ata ulaji wa mafuta unakuwa mkubwa
 
Nilimsikia Mwenyekiti wa Madereva alilalamika sana kuhusu ajali ya MAFINGA akidai ajali ilisababishwa na shimo lililopo barabarani lakini hadi sasa aliyekamatwa ni dereva tu ambaye ni muhanga wa udhaifu wa Mwandisi wa eneo hilo na watu wengine wahusika na usalama wa barabara.

Pili, sheria zetu za nchi zinaruhusu magari yasiyozidi speed 80 lakini serikali ya CCM wenyewe wamenunua magari speed hadi 200 na wameacha wananchi wanunue magari speed 120, 180.

Hili suala la ajali linahitaji mjadala mpana kama ilivyo ugaidi

Mkuu kama chanzo cha ajali ni hilo shimo hapo barabarani basi magari yote yanayopita hapo yangepata ajali. Huyo kiongozi aache kutetea uzembe Hawa madereva huwa wanafanya mambo ya hatari mno wakati mwingine
 
Mkuu kama chanzo cha ajali ni hilo shimo hapo barabarani basi magari yote yanayopita hapo yangepata ajali. Huyo kiongozi aache kutetea uzembe Hawa madereva huwa wanafanya mambo ya hatari mno wakati mwingine

Mkuu sio swala la kubishania kuhusu ile ajali ya bus la majinjah wangeanza na mkandarasi anaesimamia kile kipande cha bara bara manake shimo ni kubwa na lipo kwenye mteremko ulionyooka! Dereva akijikosea aakaweka mkasi kati akikuta shimo anakata hoze pale.

Ndio kilichotokea pale na mara baada ya ajali tu ndio lile shimo lilizibwa nadhani na wanajeshi walioko kwenye kambi maeneo yale.

Sent from JamiiForums
 
Utakuwa hauli pweza sasaaa

Mchina hao Pweza, Ngizi, Chaza na takataka nyingine zote za bahari anaweza kuwa anaziimoprt tu it's a matter of time tu. As long CCM ikiendelea kuwa madarakani products za wavuvi wetu zitaendelea kuwa optional tu.
 
Mchina hao Pweza, Ngizi, Chaza na takataka nyingine zote za bahari anaweza kuwa anaziimoprt tu it's a matter of time tu. As long CCM ikiendelea kuwa madarakani products za wavuvi wetu zitaendelea kuwa optional tu.

Haahaaaaa…… what can we do about CCM??
 
ijumaa siyo mgomo ni mkutano wa madereva wote na viongozi wa juu na idara zao za serikali. ila wasipofika hao tunaowahitaji kujibu hoja zetu na kuafikiana basi hapo ndo mgomo utakapoanzia

mkutano ulikua tar 5 labda kama kuna mwingine.
 
taarifa za kiintelijensia nilizonazo ni kwamba madereva wa mabasi na malori wanatazamiwa kugoma nchi nzima kuanzia ijumaa. Madereva hao wana malalamiko lukuki yakiwemo mikataba ya ajira,ubovu wa miundombinu,sheria kali za barabarani na nyinginezo.

Taarifa nilizonazo ni kuwa madereva wa mabasi na malori nchi nzima watamaliza kufanya kazi zao alhamisi. Watasubiri ijumaa kujua hatma ya malalamiko yao. Ijumaa,madereva wote wa mikoa ya dar na pwani watakutana na ujumbe wa serikali na wengineo ubungo

madereva wamewataka mawaziri wanne:sitta-uchukuzi,magufuli-ujenzi na kabaka-ajira na chikawe-mambo ya ndani wafike ubungo saa moja asubuhi,siku ya ijumaa tar 10 mwezi wa 4 kutoa majibu ya malalamiko ya madereva hao. Pamoja nao,wanatakiwa viongozi wa polisi,taboa,takuboa na tbs.

Majibu yao yatazuia au kuchochea mgomo wa madereva wa mabasi na malori nchi nzima.

Mimi tu,kuwaletea habari!

Mzee tupatupa wa lumumba,dar es salaam

madai yao yana umuhimu
 
Naamini siku WAALIMU wakigoma nchi nzima mwezi mmoja basi shule zetu za kata zitaboreshwa sanjari na maslahi ya walimu,mgomo ni haki na haki haitolewi bure kwenye kisahani,ukipewa bure basi unahongwa kama sio kutongozwa ili utumike,kwa nchi zetu zenye watawala wapuuzi!!!!

Mkuu huna taarifa kwani?!mbona tuko kwenye mgomo siku nyingi tu....
 
Huu mgomo umeshaanza muda mrefu wala si suala la tetesi. Hiyo Ijumaa ni kutekeleza hatua ya pili endapo serikali haitasikiliza madai yao. Hatua ya kwanza wameanza kwa kuendesha mabasi kulingana na alama za barabarani. Kwamba kama ni spidi 50 basi ni 50, kama ni spidi 30 basi ni 30. Na kwa upande fulani imeleta effect kubwa kwa wasafiri, mfano Dar - Iringa ilikuwa basi likitoka saa 12 asubuhi Ubungo linafika Iringa saa 7 mchana, ila kwa huu mgomo wao wanafika saa 11 jioni.

Maboso, niliondoka Dar j5 last week kuelekea BKB, Ubungo tuliondoka saa 12asubuhi. Ilibidi tulale Igunga kwani tulifika hapo saa tano usiku. Saa 12 asubuhi the next day tukaendelea na safari na kufika BKB saa 10unusu jioni! On my way back nikapitia MZA ambapo safari tumeianza saa 12asubuhi, na hivi sasa saa nane ndo tunaingia SNGD, inachosha sana.
 
Wakigoma nayo njaa haitagoma,wacha wagome tuone kama njaa haitawarudisha tena njiani.Watakuwa wanajigomea wao wenyewe na familia zao,njaa lazima itawarudisha tena barabarani,na ikizingatiwa hawa madereva wana michepuko kila mahali.
 
Walimu wa nchi hii wanashindwa na madereva na makondakta ambao kila siku tunawabeza ni wanywa viroba huku Walimu wakilipa kisasi kwa wanafunzi kuwafundisha hovyo na kuwafelisha baadala ya kuikaba serikali elimu iwe bora na mishahara yao"!

Mathalani,kwa nini nyumba za NHC katikati ya miji wasipewe watumishi wa umma ie WAALIMU na MADAKTARI ili wawe karibu na vituo kazi na kuwapa nafuu ya maisha baadala ya wahindi ambao wanapack magari ya 100 million nje wakati wanaishi nyumba ya umma na wanaweza kujenga huku waalimu wakiadhrika??!!! Kwa nini walimu hawagomi??!! Ama ndio kuwa kada ya ualimu na upolisi zinaongoza kuwa na watu vihio ambao hawawazi nje ya box zaidi ya rushwa na kumkomoa mwananchi??!!

Naamini siku WAALIMU wakigoma nchi nzima mwezi mmoja basi shule zetu za kata zitaboreshwa sanjari na maslahi ya walimu,mgomo ni haki na haki haitolewi bure kwenye kisahani,ukipewa bure basi unahongwa kama sio kutongozwa ili utumike,kwa nchi zetu zenye watawala wapuuzi!!!!

hapo ndipo panaponiuma,,,,walimu wamekuwa hawana msimamo kana kwamba elimu aliyonayo haimsaidii,,,wewe unalipwa 630000/= kabla ya makato wakati kuna watu wanakula mamilion ya shilingi kila siku,,,,,hakuna malalamiko ya walimu yanayofanyiwa kazi,,,,,na ni walimu hawa hawa na vikofia vyao vya CCM kuongoza kuwapigia debe sisiem,,,,,,,,Aaaaaaaggggghhhh,,,,ngoja nikanywe viroba vyangu mie
 
Back
Top Bottom