Arusha: Mgomo wa madereva Coaster kesho Desemba 7, Mkuu wa Wilaya atajwa

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Kikundi cha Madereva wa Coaster zaidi ya 80 wanaofanya usafiri katika Mikoa ya Arusha-Kilimanjro kesho wanatarajia kugoma kusafirisha abiria kwa madai kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Felician Mtehengerwa analazimisha kufanyika uchaguzi wa Kikundi hicho bila kufuata katiba yao.

Viongozi wa Kikundi hicho leo wamekutana na baadhi ya waandishi wa habari na kusema kuwa Mkuu wa wilaya amekuwa akiwalazimisha kufanyika kwa uchaguzi bila kufuata katiba na kulazimisha vijana wake kufanya kazi stand Kuu kwa maslahi yake.

Viongozi hao walisema kuwa wameshapeleka malalamiko yao zaidi ya wiki mbili kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha,John Mongella kueleza hilo lakini hadi sasa hakuna kinachoendelea na kufikia hatua viongozi wa kikundi hicho kukamatwa na kuwekwa ndani katika kituo cha polisi Arusha ili aweze kutimiz amalengo yake.

Kutoakana na hali hiyo viongozi hao wameitisha mgomo kesho na kutoa sababu nne za kusema kuwa uchaguzi huo wa Mkuu wa Wilaya ya Arusha ni batili ikiwa ni pamoja na uchaguzi unapaswa kutangazwa siku 30 lakini uchaguzi wa Dc umetangazwa siku 4,uchaguzi wsa DC una wanachama feki kwani sio wanachama wa kikundi hicho.

Viongozi hao walitaja sababu nyingine ni pamoja na viongozi waliopo madarakani kutoshirikishwa kwani ndio wenye leja ya wanachama hai lakini hilo halitaki ili atomize malengo yake.hivyo chaguzi huo wa dc ni batili na ndio maana madereva wanajianda kugoma kesho na kumtaka Mkuu wa Mkoa kuingilia kati kwani wananyanyaswa wakati wako katika nchi huru yenye amani tele.

Tunaomba viongozi wa serikali wa ngazi ya Mkoa kuliangalia hilo kwa jicho la tatu kwani Mkuu wa Wilaya anataka kunyanyasa watu kwa maslahi yake wakati viongozi na wanachama wake hawana shida ila anasukumwa na mtu mmoaja anayeitwa Abdi Marijani maarufu kwa jina la Mutu.




20231206_172646.jpg
Untitled-7-1024x512%20(1).jpg
 
Dah! Mkuu wa wilaya anahusika vipi na watu wa magari kama hakuna tishio lolote la kiusalama? Ninaungana na hao madereva kupinga huo ujinga.
 
Back
Top Bottom