Mgomo mkubwa wa wasafirishaji abiria waingia siku ya tatu Bukoba Mjini

TONGINDI

Senior Member
Nov 23, 2011
174
32
Hali si shwari katika manispaa ya Bukoba baada ya mabasi yaendayo wilaya za mkoa wa Kagera kuendelea na mgomo.

juhudi za kujadili kero zao na mkurugenzi wa manispaa zimegonga mwamba baada ya mkurugenzi kutoa kisingizio cha kushughulikia sensa, utafikiri yeye ndo kamishna wa sensa kitaifa.

baadhi ya madai yao:

1. kulipishwa ushuru mkubwa kila uingiapo na kutoka stand ya bus mfano ukiwa na basi aina ya costa ni sh. elfu tano (5000) kwahiyo ukipakia abiria awamu tano kwa siku ni elfu ishirini tano.

2. ukarabati wa stand ambayo imechoka na haina hadhi ya manispaa, wasafirishaji wanashangaa mamilioni yanayokusanywa yanakwenda wapi? kama siyo ufisadi mtupu?

Msimamo wao;

Mgomo utaendelea mpaka tarehe 1/9/2012 siku ambayo mkurugenzi amewaahidi kukutana nao

Changamoto;

katika kutunishiana misuri kati ya mkurugenzi na wasafirishaji, wanaoumia ni wananchi wasiokuwa na hatia, leo nimepita stand, ni kweupe kabisa hamna magari, wananchi ndo wapo wanabung'aaa macho infact hawajui la kufanya.

hivi hawa viongozi wa manispaa mfano, meya, mkurugenzi, mkuu wa wilaya, sijui R.C, RAS, DAS .n.k

huuu utitiri wa viongozi unatusaidia nini? if they cannot solve even these minor challenges?

toa maoni yenu wana jamvi, uwanja ni wenu,
 
Sh. 5000 kwa kila trip ni nyingi: Mkurugenzi wa manispaa inabidi aueleze umma hususani wa kazi kagera hizo pesa zinaenda wapi: ni aibu Mji Bukoba kwa ujumla wake unatia aibu kwa uchakavu:

stand ni ya hovyo alafu vijinyumba vya mjini bukoba vyote ni vya mwaka 1957: hakika huyu Mkurungenzi anazo hoja za kujibu-yeye kama BOSS pesa za makusanyo ya ushuru wa stand anazipeleka wapi???
 
Aisee babaangu huku ndio kwakina mugambile stupid in front of my wife???
 
imefika wakati bukoba pawekwe stand binafsi za kisasaa ili kuweka ushindani na manispaa
 
Hali si shwari katika
manispaa ya Bukoba baada ya mabasi yaendayo wilaya za mkoa wa Kagera
kuendelea na mgomo.
juhudi za kujadili kero zao na mkurugenzi wa manispaa zimegonga mwamba
baada ya mkurugenzi kutoa kisingizio cha
kushughulikia sensa, utafikiri yeye ndo kamishna wa sensa kitaifa.

baadhi ya madai yao:

1. kulipishwa ushuru mkubwa kila uingiapo na kutoka stand ya bus
mfano ukiwa na basi aina ya costa ni sh. elfu tano (5000) kwahiyo
ukipakia abiria awamu tano kwa siku ni elfu ishirini tano.
2. ukarabati wa stand ambayo imechoka na haina hadhi ya manispaa,
wasafirishaji wanashangaa mamilioni yanayokusanywa yanakwenda wapi? kama
siyo ufisadi mtupu?

Msimamo wao;
Mgomo utaendelea mpaka tarehe 1/9/2012 siku ambayo mkurugenzi
amewaahidi kukutana nao

Changamoto;
katika kutunishiana misuri kati ya mkurugenzi na wasafirishaji,
wanaoumia ni wananchi wasiokuwa na hatia, leo nimepita stand, ni kweupe
kabisa hamna magari, wananchi ndo wapo wanabung'aaa macho infact hawajui
la kufanya.

hivi hawa viongozi wa manispaa mfano, meya, mkurugenzi, mkuu wa wilaya,
sijui R.C, RAS, DAS .n.k

huuu utitiri wa viongozi unatusaidia nini? if they cannot solve even
these minor challenges?
toa maoni yenu wana jamvi, uwanja ni wenu,

as far as hawatumii hug usafiri they just don care
 
Back
Top Bottom