Mgombea nafasi ya Uwakilishi kwa tiketi ya Chadema katika jimbo la Uzini Zanzibar anatarajia kurudisha fomu yake ya kuomba kuteuliwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar ili awe Mgombea wa Chadema katika uchaguzi huo. Zoezi hilo litafanyika majira ya saa 4 asubuhi ambapo mgombea huyo atarudisha fomu hiyo kwa maandamano makubwa ya Wananchama wa Chadema walio Zanzibar wakiongozwa na Fuso la matangazo pamoja na msafara wa magari na pikipiki na baiskeli. Mpaka sasa Makamanda wa kikosi maalum wa Chadema wameshafungua matawi 20 katika jimbo hilo yenye jumla ya wanachama 1236. Mgombea huyo wa Chadema alishika nafasi ya pili katika uchaguzi wa 2010 akifuatiwa na mgombea wa CUF