Mgombea wa CCM awapiga mkwara wapiga kura warudishe mali zake kabla kifo hakijafika

Tukundane

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
11,455
8,249
Mgombea Ubunge aliyeshindwa katika kura za maoni kupitia chama cha mapinduzi ambaye jina lake halijatajwa katika jimbo mojawapo la wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.

Akiwa amepandwa na hasira kutokana na kushindwa kwenye kura za maoni amewapiga mkwara wapiga kura wa jimbo hilo kwa kuwataka wamrudishie fedha na mali mbalimbali ambazo alikuwa amewahonga ili wamchague kuwa mgombea kupitia chama hicho na kama watashindwa kurudisha mali zake basi wajiandae kufa kwa uchawi.

Baada ya muda mfupi baadhi ya wananchi walionekana wakiwa wamebeba mabati wakiwa wanayapeleka nyumbani kwa mgombea huyo,mabati ambayo yalitajwa na wahusika kuwa walikuwa wamenunuliwa na mgombea huyo kwa makubaliano ya kumpigia kura.

Chanzo: Bomba FM.
 
ningekua mm nisingerudisha aisee, nakumbuka hum jf ulitolewa ushauri mmoja kuntu kwamba wagombea wa ccm wasiwekeze pesa zao za kinua mgongo watakula hasara! sasa si umeona ishaanza kula kwao
 
Mgombea Ubunge aliyeshindwa katika kura za maoni kupitia chama cha mapinduzi ambaye jina lake halijatajwa katika jimbo mojawapo la wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.

Akiwa amepandwa na hasira kutokana na kushindwa kwenye kura za maoni amewapiga mkwara wapiga kura wa jimbo hilo kwa kuwataka wamrudishie fedha na mali mbalimbali ambazo alikuwa amewahonga ili wamchague kuwa mgombea kupitia chama hicho na kama watashindwa kurudisha mali zake basi wajiandae kufa kwa uchawi.

Baada ya muda mfupi baadhi ya wananchi walionekana wakiwa wamebeba mabati wakiwa wanayapeleka nyumbani kwa mgombea huyo,mabati ambayo yalitajwa na wahusika kuwa walikuwa wamenunuliwa na mgombea huyo kwa makubaliano ya kumpigia kura.

Chanzo: Bomba FM.

Maweeeee na wale wa kwa Mwigulu na Nape wao hawajadaiwa au kwa vile wao wamepewa ushindi?
 
Tena huyo mpole sana kuwaomba warudishe kuna mmoja sehemu fulani yeye alipokatwa kesho yake akaenda mlango kwa mlango kuchukua mali yake
 
Huu mwaka tutashuhudia mengi sana ya kustaajabisha.
Kama ana uchawi kwanini hakuutumia kujiongezea kura ashinde?
 
Back
Top Bottom