Leo nimeoana taarifa mtandaoni, kwamba Mgombea udiwani Kata ya Kiboroloni-moshi kwa tiketi ya CHADEMA Bw. Frank Kagoma kuwa si raia wa Tz. Swali: ni mpaka mtu agombee udiwani au ubunge au uraisi ndo ionekane si raia wa Tz? Mbona hatukusikia tangu chaguzi zote za udiwani na ubunge kwamba wahamiaji wakisema Mgombea fulani wa ccm si raia wa Tz.
Implication ya hii kitu:
1 Watu watakichukia ccm hata kama Mgombea angekuwa anafaa.
2 Itampa "credit" yule mgombea anayetuhumiwa kwamba si raia wa Tz kama ilivotokea Kwa Ezekiel Wenje na Lawrence Masha huko Mwanza. Masha alitumia mamlaka yake ya Uwaziri wa Mambo ya Ndani ili kuonyesha Wenje si raia wa Tz ili yeye apite bila kupingwa hatimaye yakamtokea puani.
mbona kuna wengine ni wasomali lakini wamo kwenye uongozi wa nchi - kama tukianza kutafutana kila mmoja wetu alipotokea tutabakia wanane tu ndani ya nchi hii.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.