Elections 2010 Mgombea Ubunge wa Chadema avamiwa, mmoja auawa, wana CCM washikiliwa

LUSAJO L.M.

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
270
126
Nimepata taarifa kwamba msafara wa Mgombea wa Ubunge kupitia CHADEMA jimbo la Kibakwe wilayani Mpwapwa Kamanda Benson Kijaila Singo umevamiwa na Green Guards wakiongozwa na Kaka wa Mbunge aliyemaliza muda wake na kuua Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Lucas Kiwanga na kujeruhi wanachama wengine wa CHADEMA. Hili limetokea leo mida ya saa moja usiku.

Tutajulishana zaidi taarifa zaidi zikitufikia.
 
Hivi tuna kwenda wapi kama Taifa? Je haya si ndiyo mambo Dr. Slaa anayepiga vita? Je Kikwete na Mwema wamechukua hatua gani kuvunjilia mbali vikundi vya kigaidi vya kijani? Ninalaani kwa nguvu zangu zote. Ninamuomba Mungu ailaze peponi roho ya yule aliyetutangulia. Amina
 
RIP the deceased, sasa tunahitaji tumuone Manumba akielekea huko mara moja na mgombea wa CCM kuwekwa ndani!
 
Nimepata taarifa kwamba msafara wa Mgombea wa Ubunge kupitia CHADEMA jimbo la Kibakwe wilayani Mpwapwa Kamanda Benson Kijaila Singo umevamiwa na Green Guards wakiongozwa na Kaka wa Mbunge aliyemaliza muda wake na kuua Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Lucas Kiwanga na kujeruhi wanachama wengine wa CHADEMA. Hili limetokea leo mida ya saa moja usiku.

Tutajulishana zaidi taarifa zaidi zikitufikia.

Tupe chanzo cha taarifa kinaweza kutusaidia kuchangia post yako. Hivi sasa tuna siku moja mkononi kuelekea siku ya uchaguzi propaganda zitaongezeka maradufu.
 
Ni masikitiko makubwa. Chama kinachojiita cha amani kinafanya mambo haya. Ingekuwa wengine tayari wangeshaswekwa ndabi.
 
Wafuasi watano wa Chama Cha Mapinduzi akiwemo mdogo wa mbunge wa jimbo la Kibakwe wilayani Mpwapwa wametiwa mbaroni na polisi kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mfuasi mmoja wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) yaliyotokea katika kijiji cha Pwaga wilayani humo.
tukio hilo lilitokea siku ya alhamisi tarehe 28/10/2010, inadaiwa katika tukio hilo wafuasi wa chadema walikuwa wakitoka kwenye mkutano wao na wakapita karibu na eneo ambalo CCM pia walikuwa wakifanya mkutano, kisha CCM kuona wafuasi wa chadema wanashangilia wakaanza kuwashambulia na katika tukio hilo mtu mmoja aliyekuwa amepanda powertiller alivutwa na kuanguka kisha akaanza kushambuliwa na wafuasi wa CCM mpaka mauti yalipomkuta

watuhumiwa wametiwa mbaroni na upelelezi kamili juu ya tukio hilo unaendelea

ikumbukwe jimbo la kibakwe upinzani kati ya CCM na Chadema ni mkali mno.
 
Kama kweli sheria ni msumeno; basi mbona mgombea wa ccm akuswekwa ndani na kuzuiwa kupiga kampeni siku mbili kama ilivyofanywa kwa Shibuda-CHADEMA?
 
Namuomba jamani Katibu Mkuu wa CCM Mzee Makamba aende na huko akasaidie kuweka mambo sawa, maana ni mtaalamu wa kugundua ushahidi wa kimazingira unaomhusisha mgombea mmojawapo na kifo hicho. Tunakumbuka alipoenda Maswa aligundua ushahidi wa kimazingira unaomhusisha mgombea mmojawapo.
 
Hakika mwaka huu ni kiama kwa ccm , hawakutarajia upinzani mkali kiasi hicho hivyo wanafanya kila mbinu kuhakikisha wanashinda, lakini cha kushangaza wao ndio wanawaambia wenzao wanamwaga damu ilhali wao ccm ndio wanafanya vurugu
 
Ilishasemwa mapema kuwa MMWAGAJI DAMU MKUU NI CCM.
Au wame-copy kwa CHADEMA hata kumwaga Damu, maana wanapaste kila kitu sasa hivi....fyuuuuuu...aibu sana kwa lichama la majitu yenye vitambi kama nyumba!
 
Nashangaa HABARI LEO hawajaandika CCM waua???
Nyie waandishi wa Habari leo mtaganga njaa mpaka lini???
yani CCM hii kampuni ya CCM ni wavunja haki na wavunja sheria sijui wanafikiri Tanzania ni CCM??
ukitaka kujua ujinga wao angalia mtu yeyete anayejua anavunja sheria anaweka Bendera yao juu, Mmachinga amesimama eneo ambalo haliruhusiwi anahalalisha kwa kuweka Bendera ya CCM, Milori mibovu, migari mibovo, sehemu Taxi zinapopaki na wakakataliwa utaona wanaanzisha Tawi la CCM, hivi hamuwezi kutumia akili na kujua serikali bila sheria sio serikali... yani huku vijijini wanapouza Pombe za gongo ili wasikamatwe wanaweka bendera ya CCM....
mpaka watoto wadogo mtoto akimpiga mwenzake anamwambia unajifanya wewe ni mtoto wa kigogo wa CCM??
CCM INATUPELEKA WAPI JAMANI....
EHEE MUNGU TUHURUMIE!!! WANACHIMBA DHAHABU MVUMI WAMEFUNIKA KWA KIWANDA CHA WINE , WANADANGANYA WANANUNUA ZABIBU ZA WATANZANIA KUMBE WANATOKA NA MATERIAL YAO ITALI....
VIONGOZI WAKIWATEMBELEA WANAINGIZWA CHUMBA CHA NDANI WANAPEWE WINE WANARUDI WAKICHEKA......
KAMA MNADHANI MIMI NI MUONGO MUULIZENI MRAMBA NANI ALIYEMSAIDIA ASHINDE 2005

TUTAKUTANA MBINGUNI HATA TONE LA MAJI SITAWADONDOSHEA.....
 
Sasa hapa ndo utaona midomo itakavyokaa kimya. hata wafanyeje, sisi tunamjua rais wa wanyonge. Hatudanganyiki
 
Ni AIBU kubwa kwa CCM, Habari Leo, Mtanzania, Makamba na wengineo wenye mawazo hasi. Poleni wafiwa wote. CCM kwa kutumia Green Guard imefanya unyama ambao imekuwa ikisema haihusiki na ghasia! tumsubiri DCI, Tuone kama Simbachawene atatiwa nguvuni japo kwa uchunguzi tu ingawa alikuwepo kwenye tukio
 
Back
Top Bottom