Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,564
- 7,973
Wadau,
Kama mnavyofahamu kuna baadhi ya watumishi wa serikali walioamua kutumia haki yao ya kidemokrasia kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika nchi yetu kwenye uchaguzi mkuu wa 2010.Wapo waliogombea kupitia ccm na wengine vyama vya upinzani.
Miongoni mwa wengi waliogombea kupitia vyama vya upinzani ni mwalimu Marwa Ryoba(Mwalimu wa shule ya sekondari Tarime) anayefundisha masomo ya sayansi (fizikia na kemia). Huyu bwana 'inasemekana" amefukuzwa kazi mara tu baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 kwakuwa aligombea kupitia chama cha upinzani.
Binafsi nimeongea naye, ameniambia serikali imesitisha mshahara wake tangu mwezi novemba mwaka jana, pamoja na kwamba alirejea kazini kwake mara tu baada ya uchaguzi.Pamoja na juhudi alizofanya kutaka kujua sababu ya kusitishwa mshahara wake, hajapewa majibu ya kueleweka na wala hajapewa barua rasmi kumjulisha kama amefukuzwa kazi, ama kasimamishwa kazi ama kuna tatizo gani lililosababisha kufikiwa kwa uamuzi huo.
Kwakuwa hili jambo linaweza kuwa limewatokea watumishi wa umma wengi, kama ilivyomtokea Pro.Baregu mwaka juzi, nadhani kuna sababu za msingi hili jambo likawekwa wazi, kama ni muongozo wa utumishi wa umma uwekwe wazi ili kila mtu ajue.Ni jambo la ajabu kwamba mtumishi wa umma akiwania nafasi ya kisiasa kupitia ccm inakuwa halali lakini akifanya hivyo kupitia vyama vya upinzani inakuwa haramu.
Hii tabia ya serikali kuleta ubaguzi miongoni mwa watanzania inabidi tuipinge kwa nguvu zote. Ili kila mwananchi awe na uhuru wa kweli wa kushiriki zoezi la demokrasia pasipo na kificho wala wasiwasi.
Nawasilisha.