Mgombea CCM azimia akihesabu kura!

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Imeandikwa na Kennedy Kisula, Liwale | Habari Leo | 04 Oktoba 2012

KATIBU wa CCM wa Uchumi aliyemaliza muda wake wilayani hapa, Said Lihomba alipoteza fahamu, wakati akihesabu kura zake juzi katika uchaguzi wa ndani wa CCM.

Lihomba alikumbwa na kadhia hiyo ndani ya chumba cha kuhesabia kura, baada ya kukataa kuchagua mwakilishi wa kumh esabia kura na kuamua kwenda mwenyewe.

Kabla ya kutokewa na hali hiyo, Msimamizi wa Uchaguzi huo, Farida Kikoleka aliwataka wagombea baada ya kupigwa kura, wateue wawakilishi au waende wao wenyewe kuhakikisha kura zao katika chumba cha kuhesabia.

Kauli hiyo ya Farida, ilisababisha wagombea wote, akiwamo Lihomba kwenda kuhakikisha kura zao zikihesabiwa. Wagombea wengine ni Mdai Mahela na Amidu Likwawatu.

Hata hivyo, wakati wakihakiki kura zao, Lihomba aliyekuwa akipata kura chache huku Likwawatu akiongoza kwa kura nyingi, alianguka ghafla.

Kutokana na hali hiyo, wasimamizi wa uchaguzi huo, Farida na Mathew Makwinywa waliamuru Lihomba atolewe katika chumba hicho na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu.

Baada ya kumaliza kuhesabu, Farida alimtangaza Likwawatu kuwa mshindi wa nafasi hiyo baada ya kupata kura 58 na kufuatiwa na Mahela aliyepata kura 43 huku Lihomba aliyekuwa hospitalini akiambulia kura 10.

Wagombea wengine Katika nafasi ya Mwenyekiti wa Wilaya, Mohamed Ngomambo alishinda kwa kura 510 na kufuatiwa na Nasoro Kimbendela (130) na Halima Huki (19).

Mohamed Ndemane alichaguliwa ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kwa kura 420 na kuwashinda Jafari Musa aliyepata kura 218 na Abdalah Kitura aliyeambulia kura 49.

Uchaguzi Meatu Naye Kareny Masasy anaripoti kutoka Meatu, Simiyu kwamba Juma Mwibuli amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Wilaya kwa kuwashinda wenzake watatu waliokuwa wakiwania nafasi hiyo.

Msimamizi wa uchaguzi huo Jumanne Kisote ambaye ni Katibu wa CCM wa Wilaya ya Bariadi alisema kuwa wajumbe waliopiga kura walikuwa 1,174.

Alisema Mwibuli alipata kura 693 na kufuatiwa na Juma Kisija (379) na Emmanuel Masunga (92) huku 10 zikiharibika. Kwa ujumbe wa NEC aliyeibuka na ushindi ni Salum Khamis (997) akifuatiwa na Paul Guyashi (145), Kulwa Komanya (30) huku mbili zikiharibika.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa ni Zuhura Chiluba (766), Elius Shukia (640), Anjela Milembe (450), Christina Jisena (434) na Tito Masele (428).
 
Kule CCM kuwapitisha wale magwiji wa UFISADI nchini kwa maana ya MAPACHA WATATU kuwa ni sehemu na vinara wa uongozi wao tukielekea 2015 si tu kwamba itakua imedhihirishia Umma wa Tanzania ya kwamba GAMBA KWAO NI MWIKO KULIVUA 'HATA IWEJE', hapana;

isipokua, kubwa zaidi hapa ni kwamba sasa Wana-CCM kwa ujumla wao wamelitangazia taifa kuwa UFISADI ni sera rasmi ya chama chao na kwamba hata kutokee vugu vugu la mageuzi la kiwango gani nchini wao ni mbele kwa mbele kwa sana.

Kiama cha CCM ni kule kukumbatia kwa sana hii sera ya ajabu na kero kubwa kwa taifa letu. Kwa kifupi, CCM kaburi lake ni UFISADI uliotukuka na kutamalaki kila idara ya chama hicho na serikali yake na sasa kuzaa mbegu chipukizi kwenye NEC-CCM hii mpya.
 
Haaaahaaaahaaaa...iiiiiiiii....haaaaahaaaaahaaaa!
Kazimia kwa kukosa kauongozi ka wilaya ka Magamba; ingekuwa ubunge/urais angekufa kabisa!
Magamba wana vituko mwanzo mwisho!
 
Tehe tehe tehe tehe,wakuu madaraka matamu acheni mchezo kabisa.
 
ccm watazimia sana na msubiri wasira siku akishindwa nahisi itakuwa ndio siku ya kifo chake
 
Duh, hii imenikumbusha 2010, mama Monica Mbega kilichomkuta Iringa baada ya kubwagwa kisawa sawa. Nasikia alilazwa pale hospitali ya Mkoa baadaye akakimbizwa kwa ndege Dar.

Dereva kanyaga twende
 
Nilisikia hii habari kwenye redio wakati wakisoma vichwa vya magazeti ya Leo kuwa "mgombea azimia akihesabu kura" hawakutaja chama lakini nikajua ni wa CCM tu!
 
Haaaahaaaahaaaa...iiiiiiiii....haaaaahaaaaahaaaa!
Kazimia kwa kukosa kauongozi ka wilaya ka Magamba; ingekuwa ubunge/urais angekufa kabisa!
Magamba wana vituko mwanzo mwisho!


mkuu pamoja na kukosahako kacheo ishu kubwa nikupoteza pesa alizo honga nyingine kapata kwanjia ya mukopo
 
Hahah ahahaaaaaaaa! Hii ndo hali itakawakumba wagombea wa CCM 2015 watakuwa wanaanguka na kuzimia tu! Akiamka anakutana na nyimbo za peoples power!
 
Back
Top Bottom