Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini?

Nawasalimu kwa jina la jamuhuri ya Muungano.

Kama kichwa kinavyosema. Naomba kuelimishwa kuhusu faida ya mgombea binafsi, hasara zake na status ya jambo hilo hapa Tanzania.

Mchungaji Mtikila alilipigania sana hili suala, napenda kujua vita yake iliishia wapi hadi mauti yanamkuta.
Pia napenda kujua athari za jambo hilo kwa vyama vya siasa.

Cc MALCOM LUMUMBA
 
View attachment 1370580

Mahakama yasisitiza wagombea binafsi

na Happiness Katabazi | Tanzania Daima

Mahakama ya Rufaa Tanzania, imetupilia mbali rufaa iliyofunguliwa na serikali, ya kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuruhusu kuwepo kwa mgombea binafsi katika chaguzi za Tanzania.

Uamuzi huo ulisomwa jana na Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama ya Rufaa, Ferdinand Wambali, kwa niaba ya jopo la majaji watatu, ambao ni John Mroso, Edward Rutakangwa na Engela Kileo.

Akisoa uamuzi huo, Wambali alisema jopo hilo limekubali pingamizi la upande wa mawakili wa mdaiwa, Richard Rweyongeza na Mpare Mpoki, ambao waliiomba mahakama kutupilia mbali rufaa hiyo.

Katika pingamizi hilo, Rweyongeza aliieleza mahakama ombi la rufaa la serikali limejaa dosari za kisheria, likiwemo kosa la kuandika tarehe tofauti ya tarehe ya hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu.

Wambali alisema wamefuta kesi hiyo iliyofunguliwa mwaka jana baada ya kubaini mawakili wa serikali, Mwaimu na Ndunguru waliwasilisha hoja dhaifu, ambazo zimeshindwa kulishawishi jopo hilo kutengua uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Kwa sababu hiyo, jopo hili linakubaliana na pingamizi la upande wa mdaiwa, na linatupilia mbali ombi la mrufani, na linaamuru upande wa mrufani kumlipa mdaiwa gharama za uendeshaji wa kesi, alisema naibu msajili huyo.

Hata hivyo, alisema serikali inaweza kuwasilisha tena rufaa yake mahakamani kwa kufuata sheria kama itaona kuna haja ya kufanya hivyo.

Machi mwaka jana, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, aliwasilisha rufaa iliyopewa namba 20/2007 akiomba Mahakama ya Rufaa itupilie mbali uamuzi wa Mahakama Kuu wa kuruhusu mgombea binafsi, kwa kuwa umeonekana kuwa na dosari za kisheria.

Mei 5 mwaka 2006, Mahakama Kuu chini ya jopo la majaji watatu walioongozwa na Jaji Kiongozi mstaafu, Amir Manento, waliruhusu kuwepo kwa mgombea binafsi katika chaguzi kwa sababu katiba ya nchi inatoa haki hiyo. Majaji wengine walioshiriki kutoa uamuzi huo ni Jaji Kiongozi wa sasa, Salum Massati na Thomas Mihayo.

Jopo hilo lilibainisha kuwa, katiba inatamka wazi kuwa kila mwananchi anayo haki ya kuchagua au kuchaguliwa kuwa kiongozi na haiweki masharti kuwa hilo lifanyike kwa mwananchi kujiunga na chama fulani cha siasa.

Katika hati ya rufaa ya serikali, Mwanasheria Mkuu wa serikali anadai Mahakama Kuu ilikosea kisheria katika kutafsri Ibara ya 21 (1) (c), 39 (1) (c) (b) na 69 (1) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mwaka 1993, mbele ya Jaji Khawa Lugakingira (sasa marehemu), Christopher Mtikilia alishinda kesi kama hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma. Hata hivyo, Bunge lilishindwa kutunga sheria ya kuruhusu mgombea binafsi katika chaguzi zilizofuata, na ndipo Mtikila alipoamua kufungua tena kesi hiyo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na kushinda.

Mtikila alifungua kesi hizo akiomba mahakama itamke kwamba mabadiliko ya ibara ya 39 na 67 chini ya marekebisho ya 11 ya katiba ya nchi kuwa ni batili na kwamba itamke kuwa ibara ya 21(1) inampa haki ya kikatiba ya kuwa mgombea binafsi katika nafasi ya urais na ubunge.


Katika madai yake, Mtikila alieleza mabadiliko hayo ya katiba yanavunja haki za binadamu ambazo zimeainishwa wazi kwenye ibara 9(a) na (f), 13(2), 20(4) na 23(1) ndani ya katiba kama ilivyoainishwa kwenye tamko la haki za binadamu ambayo Tanzania imeridhia.
---

MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU KUHUSU MGOMBEA BINAFSI TANZANIA

===

---

MICHANGO ILIYOTOLEWA NA WADAU

===

===

===


===

===

===

===

===



Pia Soma:

1) Serikali yaamriwa kuanzisha mchakato wa mgombea binafsi, ni baada ya Mtikila kushida kesi

2) Rev. Mtikila ashida kesi ya kuruhusu mgombea binafsi mahakama ya Africa
Mkuu ZZK, Zitto , pokea baadhi ya nondo, zipime, mkiona zina sifa, zijumuishe katika maazimio ya kikao chenu cha TCD, leo yanayokabidhiwa Kwa kile kikosi kazi, yatue mezani Kwa Mama, ili sheria zifanyiwe mabadiliko kabla ya uchaguzi wa 2025.

Waliosusa waacheni wasuse, maana kama awamu ya 5, la katiba lilikuwepo kwenye ilani ya CCM, na hatukumlazinisha JPM kubadili katiba, sasa la katiba halimo kwenye ilani ya Samia, hivyo kumshiza au kumlazimisha Samia kukamilisha mchakato wa katiba mpya ni kumuonea!. Tunaweza kubadili baadhi ya sheria kandamizi na kuvibadili baadhi ya vipengele kandamizi vya katiba iliyopo, kuwezesha uchaguzi wa 2025, kuwa ni uchaguzi huru na wa haki, halafu mchakato wa katiba mpya ukaendelea, Kwa nafasi baada ya 2025.

Paskali
 
Mkuu ZZK, Zitto , pokea baadhi ya nondo, zipime, mkiona zina sifa, zijumuishe katika maazimio ya kikao chenu cha TCD, leo yanayokabidhiwa Kwa kile kikosi kazi, yatue mezani Kwa Mama, ili sheria zifanyiwe mabadiliko kabla ya uchaguzi wa 2025.

Waliosusa waacheni wasuse, maana kama awamu ya 5, la katiba lilikuwepo kwenye ilani ya CCM, na hatukumlazinisha JPM kubadili katiba, sasa la katiba halimo kwenye ilani ya Samia, hivyo kumshiza au kumlazimisha Samia kukamilisha mchakato wa katiba mpya ni kumuonea!. Tunaweza kubadili baadhi ya sheria kandamizi na kuvibadili baadhi ya vipengele kandamizi vya katiba iliyopo, kuwezesha uchaguzi wa 2025, kuwa ni uchaguzi huru na wa haki, halafu mchakato wa katiba mpya ukaendelea, Kwa nafasi baada ya 2025.

Paskali
mkuu unaweza kunisaidi ilani ya mama samia tofauti na ilani ya magufuli, navyofahamu wote wanatumia ilani ya ccm na mama alipoingia ccm haikuleta ilani nyingine tofauti na ile waliyotumia 2020.
Mang'ula aliwahi kuwajibu wale waliotaka bandari ya bagamoyo kuwa ilani yao ilisema wajenge gati na sio bandari.
Kwa kifupi ilani inayotumika ni ya awamu ya tano.
 
Akili Kichwani,
Sasa unaanza kueleweka kuwa ni mabavu tu ya serikali yatatumika kuzuia hoja ya mgombea binafsi kwa hiyo kizingiti cha mahakama kitakuwa kimerukwa lakini kumbuka serikali hiyo hiyo ilikuwa inasema ni ndoto kuwa na serikali ya mpito kule zanzibar kwa vile katiba nasisitiza tena katiba hairuhusu wala si sheria

tofauti na hila la mgombea binafsi katiba inaruhusu kwa mtazamo wako lipi kati ya serikali ya mseto zanzibar na mgombea binafsi lilihofiwa zaidi na serikali kuu obvious ni serikali ya mseto ambayo rais na makamu wake wa zanzibar watakuwa na impact kubwa kwa serikali kuu zaidi ya huyu mgombea binafsi
Kwa wale msiojua, kile kilichonikuta kwenye lile jambo langu, kinatikana na ubatili huu niliuzungumza hapa!. Kuna uwezekana mtu una jambo lako unalitaka, unalipania sana la Mungu anakunyima, unalikosa, unakubali matokeo kwasababu waliochaguliwa wamekupita sifa, ila kuumia kulikosa jambo lako unakuwa umeumia!. Kumbe kuna uwezekano, majanga mengine sio majanga, ni mapito!. Unapitishwa kwenye mapito ya majanga huku unachapwa mijeledi, kumbe ni kwa kupigwa kwako, unapigwa ili wengine waponywe, hivyo majanga hayo yakawa ni a blessing in disguise!.

Mungu Nisaidie Niyaweze yote katika YEYE anitiaye nguvu!.
P.
 
"Hata marehemu baba wa taifa, mwalimu Nyerere kwa nguvu zote naye alisimamia hoja hiyo katika hotuba yake kwenye sherehe za sikuu ya wafanyakazi zilizofanyika mkoani Mbeya 1995 na mahakama za sheria mara kwa mara zimekuwa zikiamua kwa uwazi kuhusu hoja hiyo na zinasisitiza kwamba ni kinyume na katiba ya nchi kuizika hoja ya mgombea binafsi".
Katika kuadhimisha Nyerere Day, tumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kulitekeleza hili!.
Rais Samia akiamua, anapaswa kuwapuuza wahafidhina wa CCM, na kulitekeleza hili!.
Happy Nyerere Day!

P
 
Back
Top Bottom