Mgawo wa umeme wapungua • Lema ataka wananchi kuvuta subira

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,975
9,566

na Hellen Ngoromera na Grace Macha


amka2.gif
MGAWO wa umeme unaoendelea nchini hivi sasa umepungua hasa katika Jiji la Dar es Salaam, kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji katika mitambo ya kufua umeme ya kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL).
Kwa zaidi ya siku tatu hali ya mgawo katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam yameonyesha unafuu wa kupata umeme kwa siku nzima huku mengine yakipata mgawo kidogo.
Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Philip Saliboko, alisema uzalishaji wa mitambo hiyo umeongezeka tangu kati kati ya wiki iliyopita.
“Uzalishaji katika mitambo ya IPTL umeongezeka tangu siku tano zilizopita, kwa sasa tunazalisha megawati 100 na hali hiyo inatokana na serikali kununua mafuta mazito ya kuendeshea mitambo hii,” alisema mtendaji huyo wa Rita ambaye kampuni yake ni Mfilisi wa Kampuni ya IPTL.
Kabla ya uzalishaji wa IPTL kuongezeka, mitambo hiyo ilikuwa ikizalisha megawati 10 pekee za umeme.
Kwa mujibu wa Saliboko, kupungua kwa mgawo huo kunatokana na IPTL kuongeza uzalishaji na kwamba jinsi siku zitakavyokwenda ndivyo hali itakavyozidi kuwa nzuri kwa nchi nzima ikitegemeana pia na kunyesha kwa mvua.
Aliwataka wananchi kuendelea kuvuta subira na kuwa na imani na utendaji wao na serikali kwa ujumla.
Katika hatua nyingine, baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wamepongeza hatua ya mgawo kupungua hivyo kuitaka serikali kutimiza ahadi inazowaahidi ili kumaliza kabisa mgawo.
Salim Ahmed, mkazi wa mbagala alisema hakuamini baada ya kuona tangu juzi nyumbani kwake kukiwa na umeme kwa siku nzima na kwamba kama mgawo umemalizika ni furaha kwake.
Naye Flora Amon wa Buguruni, alisema pamoja na kupungua kwa mgawo serikali haina budi kutafuta mbinu mbadala za kutatua matatizo yanayosababisha mgawo.
Naye Khalfan Abdulah alisema serikali haina budi kuwa makini na mambo mbalimbali yahusuyo maendeleo ya nchi hasa tatizo la umeme.
Hatua ya IPTL kuongeza uzalishaji imetokana na serikali kupitia Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kuahidi kwa jamii kama njia ya kupunguza mgawo.
Kwa mujibu wa Ngeleja ambaye alitoa kauli hiyo mjini Dodoma hivi karibuni wakati akizungumza na waandishi wa habari, hatua hiyo itatokana na Hazina (Wizara ya Fedha) kutoa fedha za kununua mafuta mazito ya kuendesha mitambo hiyo.
Naye Tumaini Steven mkazi wa Mtoni Kijichi alisema tangu Jumamosi wakazi wa huko wamekuwa wakipata umeme kwa siku nzima na kwamba anapongeza juhudi zilizofanywa na serikali.
Naye Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA) amewataka wananchi kuwa wavumilivu wakisubiri serikali ipatie ufumbuzi suala la mgawo wa umeme unaondelea nchini ambao Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ameahidi utamalizika Agosti 30, mwaka huu.
Lema alisema endapo muda huo utaisha bila tatizo hilo kumalizika hatakuwa na pingamizi kwa wananchi hao kuingia barabarani kufanya maandamano kushinikiza kupatikana kwa nishati hiyo aliyodai kuwa kukosekana kwake mbali ya uchumi wa nchi kuyumba lakini linaongeza kasi ya vijana kuondolewa kwenye ajira.
Aliyasema hayo juzi alipokuwa akifafanua hatua yake ya kukwepa kupokelewa kwa maandamano yaliyoandaliwa na madereva wa daladala mwishoni mwa wiki katika eneo la Kisongo kwa lengo la kumpokea akitokea mjini Dodoma anakohudhuria vikao vya Bunge la bajeti ambayo yalikuwa yaishie kwenye viwanja vya NMC.
Lema alisema kuwa leo atakutana na madereva wa magari madogo ya abiria maarufu kama vifodi kusikiliza kero zao kama alivyowaahidi wiki iliyopita alipowasiliana nao akiwaomba kuacha mgomo wao uliodumu kwa siku tatu mfululizo ili wananchi wasiendelee kuteseka.
Alisema kwa kuwa serikali imeonyesha nia ya kusikiliza kero za madereva hao na wako tayari kuzipatia ufumbuzi aliona hakuna sababu ya kuandamana na yeye kama mwakilishi wa wananchi wa Arusha Mjini ataendelea kufanya mazungumzo na serikali mpaka madereva hao wapatiwe haki zao ikiwa ni pamoja na kuacha kuonewa.
“Nawaomba wananchi wasubiri mpaka Agosti 30 kama ahadi ya Pinda (Waziri Mkuu) haitatimia hapo tutaandamana mpaka kieleweke; hatuwezi kuadhimisha miaka 50 ya taifa huru tukiwa gizani huku serikali ikikosa sababu za msingi za kuwepo kwa tatizo hilo,” alisema Lema.


 
Ili jamaa Jembe!lina Roho ya ajabu..ujasiri ata Simba linaweza kumpga busu!LONG LIVE MunguBariki Lema
 
wanatuteka watanzania kwa siku hizi chache ili budget ipite, then tutarudi kwenye mgao wa giza.... Kama tupo makini mgomo na maandamano nchi nzima wakidhubutu kupitisha budget ya Ngeleja.
 
ndo maana hii geresha imeanza toka juzi mpakacleo umeme upo. mimi siamini wanachosema ni usanii tuu
 
Mtendaj wa Rita amekuwa msemaji wa masuala ya nishati. Hayo yanatokea Tz only.
 
Ili jamaa Jembe!lina Roho ya ajabu..ujasiri ata Simba linaweza kumpga busu!LONG LIVE MunguBariki Lema
Linaweza hata kumla denda Mamba kwa ujasiri huu. CDM ingekuwepo toka 1977 ikiikimbiza CCM kwa mwendo huu, ingekuwa vipi...
 
Tunachotaka siyo kupunguza kasi ila pasiwe na mgao kabisa. hata hayo makali yenyewe sioni kama yamepungua Dar ni mkoa mmoja kati ya ishirini na kitu iliyopo Tzz. sisi huku wa mbali mbali hata kabla ya mgao umeme kwetu ni tatizo huo mgao umetukutia tu. tusiwe kama wototo kunyamazishwa kwa kupewa pipi wakati tuna njaa kali. hali bado ni teteeeeeeeeeeeeeeeeee!!!
 
Back
Top Bottom