Mgao wa Umeme wawa kero Dar

Dr. Chapa Kiuno

JF-Expert Member
Sep 11, 2009
443
18
</SPAN>





MGAO wa umeme wa zaidi ya saa 14 kwa siku katika kila kona ya jiji ya Dar es Salaam, ulioanza wiki iliyopita nchi nzima, umekuwa ni kero na kuwasababishia watu kuingia hasara katika shughuli zao za kila siku.


Kufuatia mgao huo wakazi wa jiji hilo wamekuwa na hali ya kuingia na hali ya mashaka kuhusu mgao huo unaokuwa kero katika jiji hilo.

Hali hiyo imedaiwa kuwa ni mchongo uliochongwa na wenye nyadhifa ili kuifanya Serikali, Bunge na Watanzania wote walazimike kukubaliana na uamuzi wa kununuliwa kwa mitambo ya kuzalisha umeme ya Kampuni ya Dowans, ambayo ni mbadala wa kampuni tata ya kuzalisha umeme ya Richmond.

Hayo yanahisiwa kwa kuwa hadi kufika sasa Serikali haijawa na mikakati madhubuti ya kuondoa tatizo hilo la umeme nchini ambalo linapunguza vipato vya baadhi ya watanzania kwa siku.

Baadhi kwa wakazi wa jiji hilo na wanasheria wanasema kuwa endapo serikali ingeamua kuvalia njuga suala hilo basi tatizo hilo lingemalizika mara moja kwa kuwa Serikali yetu ina pesa nyingi sana, na kudaiwa kuwa hivi sasa inakusanya zaidi ya shilingi bilioni 250 kwa mwezi kupitia kodi.

Na isingeshindwa kuwapatia Watanzania umeme wa uhakika kuliko hii hali iliyopo sasa wa kukaa bila umeme zaidi ya masaa 12 na kuendelea nchi nzima.

Hata hivyo uongozi wa juu wa shirika hilo walipohijiwa kuhusiana na tuhuma hizo walikana vikali na kudai kuwa mgao huu hauhusiani hata kidogo na mitambo ya Dowans.

Na kusema kuwa mgao huu unatokana na vyanzo vya umeme kuwa hafifu na kuzalisha umeme ambao hautoshelezi kwa kutumia nchi nzima na ndio chanzo cha mgao huo.

Kufuatia mgao huo wananchi wameulani vikali mgao huo mana unawarudisha nyuma kimaendeleo kwa kuwa bila umeme hawawezi kuongeza kipato cha siku kutokana na shughuli zao zinaenda na umeme.




</SPAN>
Source: NIFAHAMISHE
 
Back
Top Bottom