Mgao wa mali za Jide, Gadner 'UTATA'

warumi

R I P
May 6, 2013
16,273
18,389
HALI tete ! Bado vuguvugu la madai ya kuvunjika kwa ndoa ya mtangazaji mahiri Bongo, Gardner Gabriel Fikirini Habash ‘ Kapteni’ na Mbongo Fleva , Judith Daines
Wambura Mbibo ‘ Lady Jaydee au Jide ’ , sasa lingine limeibuka ambapo mali za wawili hao zinatajwa kuzua utata , Risasi Jumamosi linachambua .

Kwa mujibu wa chanzo cha ndani , Gardner ameshapeleka hati ya kesi kwa mwanasheria wake kwa kusudio la kumpandisha kizimbani
mtalaka wake huyo ili mgawo wa mali ujulikane na kila mmoja apate haki yake .

KILICHOZINGATIWA

Kilichozingatiwa katika mgawo huo ni uhalali wa ndoa yao iliyofungwa Mei 14, 2005 ambapo mali zote zilizopatikana ndani ya ndoa ni za wote kwa mujibu wa sheria ya Ndoa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .

Nyumba anayomiliki Judith Daines Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee na aliyekuwa mumewe Gardner Gabriel Fikirini Habash ‘ Kapteni.

“Gardner anataka mgawo wake, lakini sasa utata ulioibuka ni kwamba, inaonekana kama
mali zote ni za Jide kwa vile zimeandikwa majina yake hivyo jamaa ana wasiwasi kwamba Jide anaweza kusema mahakamani
kuwa alizichuma mali hizo kabla ya ndoa , ” kilisema chanzo hicho kilicho jirani na familia hiyo .

Chanzo hicho kiliendelea kudai kwamba, utata huo umemfanya Gardner kuwa bize ili kuhakikisha anaumaliza hususan kwenye
nyumba yao iliyopo Mbezi ambapo wengi wanaamini ilijengwa kwa kutumia fedha ya Jide kabla hawajafunga ndoa .

MALI ZINAZOTAJWA

Mali zinazotajwa kuibua utata ni Mgahawa wa Nyumbani Lounge uliopo Kinondoni, Dar ambao hivi karibuni Jide aliubadili jina na
kuuita M .O . G Restaurant . Mgahawa huo walipangishwa na mtu.Gari aina ya Range Rover Evoque linalomilikiwa na Judith Wambura ‘Lady Jaydee .

Kuna madai kwamba, Jide na Gardner kabla ya ndoa yao kuparaganyika walikwenda kwa
mmiliki huyo na kusema wameamua kuuacha baada ya mkataba wao kumalizika . Lakini kilichoonekana baadaye, Jide alirudi kwa njia
ya uani na kuanzisha mkataba mpya bila Gardner na kuuita M. O .G .

Mali nyingine mbali na nyumba na mgahawa ni mabasi madogo mawili aina ya Toyota Hiace , moja la Machozi Band na la M .O .G Restaurant . Mabasi hayo yameandikwa Lady Jaydee & Machozi Band .

Hata hivyo , yapo madai kwamba Machozi Band nayo imebadilishwa jina, sasa inaitwa Lady Jaydee
& The Band .

Mali nyingine ni Albamu zote za Jide alizotoa tangu mwaka 2005 wakiwa tayari kwenye ndoa ambapo kwa kawaida mauzo yake ni
endelevu na gari la kutembelea aina ya Range Rover Vogue .

Albamu hizo ni Moto ( 2005) , Shukrani, The Best of Lady Jaydee ( 2006 ) na Nothing But the Truth ( 2014 ) .
 
Attachments

  • 1416093592199.jpg
    1416093592199.jpg
    37.2 KB · Views: 3,147
Gadner naye aache uchizi mimi pia naamini mali ni za Jide , hakuna mwanaume ambaye atanunua magari,kiwanja na ajenge nyumba halafu vyote aandike jina la mke wake, wanaume ni wabnafsi sana.Jide kwahapo namsifu alikuwa mjanja sana.
Gadner atafute hela akaanze maisha aache kulilia mali za mwanamke, yani mali za Jide zigawanywe halafu Gadner akatanue na mwanamke mwingine aha hapana sikubali. Hapa Jide akaze buti hasikubali
 
Gadner atafute hela akaanze maisha aache kulilia mali za mwanamke, yani mali za Jide zigawanywe halafu Gadner akatanue na mwanamke mwingine aha hapana sikubali. Hapa Jide akaze buth hasikubali

Gadner hana chake, anatapa tapa, alikuwa ni kati ya marioo waliobahatika kupendwa na mwanamke mwenye pesa zake na maisha mazuri, kila kitu alipewa ila akaona bado akataka hata visivyotakika, mwache ahangaike na maisha, hana jipya
 
Hapo ndo nashindwa muelewa GADNER.
 
Ilikuaje aruhusu Mali zote ziandikwe jina la mke wakati wamechuma pamoja.

Inawezekana jamaa alikua analipwa kama mfanyakazi tu, Na mapato na matumizi alikua hajui na kiasi kilichopo bank alikua hajui pia.

Kuna mawili inawezekana Gadner alijisahau pesa yake akaishia kutanua au ana mali zake(nyumba) ya siri ambayo Jide hajui. Imeandikwa''enyi waume ishini na wake zenu kwa akili'' yeye hakuishi kwa akili mpk mwanamke akamzidi akili .
 
Gadner hana chake, anatapa tapa, alikuwa ni kati ya marioo waliobahatika kupendwa na mwanamke mwenye pesa zake na maisha mazuri, kila kitu alipewa ila akaona bado akataka hata visivyotakika, mwache ahangaike na maisha, hana jipya
Sasa itakula kwake, ukiwa jeuri kwenye mahusiano inapaswa uwe umejiandaa na matokeo, sasa yeye anahangaika na michepuko halafu hana hata pa kulala.
 
Gadner naye aache uchizi mimi pia naamini mali ni za Jide , hakuna mwanaume ambaye atanunua magari,kiwanja na ajenge nyumba halafu vyote aandike jina la mke wake, wanaume ni wabnafsi sana.Jide kwahapo namsifu alikuwa mjanja sana.
Gadner atafute hela akaanze maisha aache kulilia mali za mwanamke, yani mali za Jide zigawanywe halafu Gadner akatanue na mwanamke mwingine aha hapana sikubali. Hapa Jide akaze buti hasikubali

Hapo mwanamke ndo angefanyiwa hivi kama anavyofanyiwa gardner humu pasingekalika
 
jidejide wewe ni sururu! sasa habashi akale alipokuwa anapeleka mboga looo. na atashangaa ile michepuko ilokuwa inamchuna sahivi akienda hana kumi watamkimbiza.
Ila tuacheni unafiki mwanamke akiachwa mambo ya nyumba gari atazugwa oooo mara za watoto oo alinikuta navyo mwishowe utakuta mnagawana hotpot' thermos n.k. duu
 
Gadner hana chake, anatapa tapa, alikuwa ni kati ya marioo waliobahatika kupendwa na mwanamke mwenye pesa zake na maisha mazuri, kila kitu alipewa ila akaona bado akataka hata visivyotakika, mwache ahangaike na maisha, hana jipya

Mkataa pema pabaya panamwita.........................
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom