Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 950
- 2,866
Mwaka Mpya wa China umewakutanisha Wachina na kufanya tathmini juu ya mfumuko wa bei Tanzania.
Wachina wauza mashuka, mataulo, mapazia, chupa za maji, vyombo vya Udongo, maua, chupi, chupa za chai na vyandarua wamesema bei wanazouza sasa zinawapa hasara kubwa sababu dola imepanda thamani maradufu dhidi ya shilingi ya Tanzania.
Dola Leo pale Kariakoo ni 2850 miaka nyuma wakati wa Magufuli, wao walinunua Dola 1 sawa na shilingi 2,180 hadi 2,200 mfumuko huo wa bei unawalazimisha wao kupandisha bei za bidhaa zao na kufanya soko kuwa gumu kwa kukosa wateja.
Kuna bidhaa kama chandarua wanayouza sh 6,000 kwa bei ya jumla kupandisha hadi sh 10,000 kwa bei ya jumla, hii inawawia vigumu wafanyabiashara wa rejareja waliozoea kununua kwa 6,000 na kuuza kwa 10,000 kama watanunua 10,000 kwa jumla itabidi wauze 14,000 kwa rejareja.
Wafanyabiashara wa chupa za maji wanazouza chupa moja kwa sh 6,000 kwa bei ya jumla itawabidi wapandishe hadi sh 10,000 kwa bei ya jumla, hii inakuwa ngumu kwa mfanyabiashara wa rejareja ataenunua chupa moja ya maji kwa sh 10,000 itamlazimu kuuza sh 14,000 kwa bei ya rejareja.
Biashara inakuwa ngumu kwa wauzaji wa jumla na rejareja sababu ya Dola kupanda bei, ukihitaji Dola laki Moja kuagiza mzigo,itabidi 100,000×2850=285,000,000 itakulazimu uwe na Milioni mia mbili themanini na tano wakati miaka mitano nyuma ilikuwa 100,000×2180=218,000,000 sasa kuna hasara ya 285,000,000-218,000,000=67,000,000 mfanyabiashara anapata hasara ya sh milioni 67,000,000 akipata hasara kwa miaka mitano itamlazimu kurudi kwao China.