Mfuko wa Bima ya afya uliingizwa kinyemela.Wala wafanyakazi hatukuhojiwa kama tunapenda au laa.Kwa hiyo mishahara yetu ilikatwa bila ridhaa yetu.Kitendo hiki kisheria si halali,na nadiriki kusema kwamba serikali ilikiuka haki za msingi za wafanyakazi wake.Kana kwamba hilo halitoshi,bado mfuko huo umeendelea kuwa kero kubwa kwa wafanyakazi.Mpaka leo wafanyakazi wengi hawana vitambulisho na vituo viko mbali mno na wafanyakazi,kiasi kwamba wengi hatupati huduma hiyo muhimu.Jambo la kushangaza ni kwamba uongozi wa mfuko huo hauonyeshi jitihada zozote za dhati za kupeleka huduma hiyo karibu na wanachama wake.Hata pale unapojikongoja na kufika kwenye kituo chote chote kinachotoa huduma hizo, huduma kwa ujumla ni mbovo sana.Hata zile huduma ambazo mfuko unasema unatoa kama vile miwani ya macho,matibabu ya Typhoid nk.vituo vingi hata kama vina uwezo wa kutoa huduma hiyo vinasema havitoi.Mimi binafsi nimeanza kukatwa huduma ya afya zaidi ya miaka mitano iliyopita,kwa kiwango cha Sh.20,000 kwa mwezi,lakini nimeshawahi kupata huduma hiyo mara tatu tu.Jamani kama sio uonevu huo na wizi wa hela zetu ni nini.Malengo ya huduma hiyo sio mabaya,lakini utekelezaji wake ni mbaya mno.Naomba serikali ichukue hatua za dhati za kusimamia uboreshwaji wa huduma zinazotolewa na mfuko huo.