Mfanyabiashara anayeuza vifaa vya magari vya wizi Ilala akamatwa, Polisi wasema msako unaendelea

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,827
12,009
Jeshi la Polisi limemkamata Gamariel Swai (43) mfanyabiashara na mkazi wa Mbezi kwa tuhuma za kuuza spea za magari zilizoibwa kwenye magari ya watu mbalimbali. Duka lake lipo Mtaa wa Songea, Ilala.

Awali, Jeshi la Polisi tarehe 23 Julai 2022 lilipokea taarifa ya wizi wa vifaa vya gari huko maeneo ya Kivule bombambili Ukonga ambapo Sifael Msemwa (38) mkazi wa Bombambili aliibiwa vifaa vya gari yake aliyokuwa ameiegesha nyumbani kwake aina ya Toyota Prado yenye usajili namba. T. 429 BKK ambavyo ni side mirror 03, power window 04, control box na betri la gari.

Tarehe 15 Agosti 2022 baada ya upelelezi alikamatwa mtuhumiwa Gama Swai na katika upekuzi katika duka lake Namba 21 lililopo mtaa wa Songea, Ilala alikutwa na side mirror 02 na power window 04 zilizoibwa toka katika gari hilo Toyota Prado.

Aidha vilikamatwa vifaa vingine mbalimbali vya magari dukani hapo vinavyodhaniwa kuwa ni vya wizi kutokana na kutokuwepo na maelezo ya kutosha kuhusiana na vifaa hivyo. Vitu vilivyokamatwa ni .

Taa za mbele 93 za magari ya aina mbalimbali, taa za nyuma 130 za magari ya aina mbalimbali, power window 189 za magari ya aina mbalimbali, side mirror 62 za magari ya aina mbalimbali, show za mbele za magari 07 mbalimbali, show za ndani za magari 35 za aina mbalimbali, mikono ya milango (vitasa) 26 za magari, rejeta 01 na betri moja.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linaendelea na oparasheni kali dhidi watu wanajihusisha na matukio ya kihalifu ikiwa ni pamoja wizi wa magari na uuzaji wa vifaa vya magari vitokanavyo na magari ya wizi.
 
Polisi minya huyo Swai mpaka ataje mtandao wote.
Jeshi la Polisi limemkamata Gamariel Swai (43) mfanyabiashara na mkazi wa Mbezi kwa tuhuma za kuuza spea za magari zilizoibwa kwenye magari ya watu mbalimbali. Duka lake lipo Mtaa wa Songea, Ilala...
 
he hao wako miaka na miaka hapo siku moja tu anatoka labda mshataki awe ni mtu mzito
Na Mapolisi wamekuwa wakila nao. Huwa wanawapiga ambush akiibiwa mkubwa. Huyo waliyemtaja ni kweli aliibiwa ila hiyo operation hadi wanakamata hivyo vitu, ilifanywa kwa sababu ya mkubwa fulani, then wakafumania na vya wengine. Ili kutuziba macho wamemtaja mlalamikaji wa kawaida.
 
Ndio maana tunaomba Police traffic wapunguzwe na waongezwe polisi WA uchunguzi wapunguze huu uhalifu, ambao network Yao ni rahisi kufahamika
 
Gari zinaibiwa zinakatwa Kama spea Kisha wanaletewa hao wauza spea.

Huyo lazima anaujua mtandao mzima
IGP Wambura atupunguzie hii adha Kwani kama hakuna mnunuzi WA jumla mbona Hawa vibaka akina Swai wataacha!! Ila pia chunguzeni kama huyu ndio Swai anayekaa Kwa Mrema Bonyokwa huyu ni mzoefu WA siku mingi sana
 
Ndio maana tunaomba Police traffic wapunguzwe na waongezwe polisi WA uchunguzi wapunguze huu uhalifu, ambao network Yao ni rahisi kufahamika
Unadhani tatizo ni upungufu wa polisi wa upelelezi? Maweee! Tatizo ni polisi wenyewe. Tena ukiwaongeza utakuwa unazidi kuongeza matatizo.
 
Polisi ndio tatizo,polisi wa nchi hii wengi wanashiriki uhalifu,polisi wanawajua vibaka,wezi,majambazi,ukiona umeibiwa na umeripoti polisi hujampata mwizi wako ujue ujatoa dau la maana.
 
Kama wao ndo wanashirikiana na wezi, sijui kuna nini tena hapo......nchi zetu hizi ni kama zina laana.
 
Na Mapolisi wamekuwa wakila nao. Huwa wanawapiga ambush akiibiwa mkubwa. Huyo waliyemtaja ni kweli aliibiwa ila hiyo operation hadi wanakamata hivyo vitu, ilifanywa kwa sababu ya mkubwa fulani, then wakafumania na vya wengine. Ili kutuziba macho wamemtaja mlalamikaji wa kawaida.
Huu ndio uhalisia itakuwa
 
Eeh na mara nyingi wenye namba B au C ndio gari za maafande. Itakuwa vijana wa bw. Swai walidandia mtumbwi wa vibwengo 😂😂😂
 
Polisi ndio tatizo,polisi wa nchi hii wengi wanashiriki uhalifu,polisi wanawajua vibaka,wezi,majambazi,ukiona umeibiwa na umeripoti polisi hujampata mwizi wako ujue ujatoa dau la maana.
Polisi wa kibongo ni Legal Gangstas 😂😂😂
 
Jeshi la Polisi limemkamata Gamariel Swai (43) mfanyabiashara na mkazi wa Mbezi kwa tuhuma za kuuza spea za magari zilizoibwa kwenye magari ya watu mbalimbali. Duka lake lipo Mtaa wa Songea, Ilala.

Awali, Jeshi la Polisi tarehe 23 Julai 2022 lilipokea taarifa ya wizi wa vifaa vya gari huko maeneo ya Kivule bombambili Ukonga ambapo Sifael Msemwa (38) mkazi wa Bombambili aliibiwa vifaa vya gari yake aliyokuwa ameiegesha nyumbani kwake aina ya Toyota Prado yenye usajili namba. T. 429 BKK ambavyo ni side mirror 03, power window 04, control box na betri la gari.

Tarehe 15 Agosti 2022 baada ya upelelezi alikamatwa mtuhumiwa Gama Swai na katika upekuzi katika duka lake Namba 21 lililopo mtaa wa Songea, Ilala alikutwa na side mirror 02 na power window 04 zilizoibwa toka katika gari hilo Toyota Prado.

Aidha vilikamatwa vifaa vingine mbalimbali vya magari dukani hapo vinavyodhaniwa kuwa ni vya wizi kutokana na kutokuwepo na maelezo ya kutosha kuhusiana na vifaa hivyo. Vitu vilivyokamatwa ni .

Taa za mbele 93 za magari ya aina mbalimbali, taa za nyuma 130 za magari ya aina mbalimbali, power window 189 za magari ya aina mbalimbali, side mirror 62 za magari ya aina mbalimbali, show za mbele za magari 07 mbalimbali, show za ndani za magari 35 za aina mbalimbali, mikono ya milango (vitasa) 26 za magari, rejeta 01 na betri moja.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linaendelea na oparasheni kali dhidi watu wanajihusisha na matukio ya kihalifu ikiwa ni pamoja wizi wa magari na uuzaji wa vifaa vya magari vitokanavyo na magari ya wizi.

Tunaona watu wamekaa bar wanakula bia wana mausafiri ya maana kila siku wanabadikisha magari kumbe wanaishu ndefu ilala
 
Back
Top Bottom