Mfahamu Yassine Chueko, Mlinzi binafsi wa Messi

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
1,590
2,088
Unapofanya kazi ya kuwa mlinzi wa mmoja wa wanasoka mashuhuri duniani, basi tambua ni kazi ngumu sana, tena yenye kuhitaji umakini mkubwa. Hii inakwenda mbali mpaka kusema kwamba lazima uwe na mafunzo ya juu, motisha ya kutosha, katika hali bora ya kimwili na macho daima na wakati mwingine wanajeshi au watu wenye taaluma ya usalama ndio hupata kazi za namna hii.
1704437529676.png


Wanamichezo wengi duniani wamepata kuajiri watu kwa ajili ya usalama wao na mali zao, sio kwamba wanajilinda dhidi ya mashabiki ila wanaelewa kuwa umaarufu pia unavutia matukio ya kihalifu kama vile Jordan Henderson, Raheem Sterling pamoja na Matteo Guendouzi. Mwanadada kutoka Jamhuri ya Czech Petra Kvitova alivamiwa na kibaka na kupata majereha katika mkono wake. Mwaka 2007 Anna Chakvetadze kutoka Urusi alivamiwa na kuibia vitu vyake na watu sita huko Moscow.

1704437620355.png

Derrick Williams mchezaji wa Mpira wa Kikapu alipigwa tukio na wanawake wawili na kuibiwa dola $700,000za kimarekani hii ni baada ya mwamba kuwachukua Malaya wawili na kwenda nao kwake, mwanalifind mwanakuliget. Draymond Green, na Vince Carter Robb pamoja na wengine wamekutana na matukio ya wizi ambapo wamepoteza vitu vyao vya thamani sana.
1704437668124.png

Ila majuzi kumeibuka video ikimuonesha Mlinzi wa Mchezaji nguli wa dunia, Bwana Mkubwa Lionel Messi akimzuia shabiki ambaye alitaka kwenda kumkumbatia Messi. Mwamba amepanda kweli na anaonekana anafanya kazi yake vyema sana toka Messi ametua katika klabu ya Inter Miami.
1704437713731.png

Huyu Mwamba anaitwa Yassine Chueko, Mwanajeshi mstaatu ambaye kwa sasa ndo mlinzi binafsi wa Messi. Inafurahisha sana kuona watu wakibeza msemo wa “Salimia watu, Connection zipo kitaa” , pendekezo la ajira ya Chueko ilikuwa ni pendekezo kutoka nahodha wa zamani wa England na mmiliki mwenza wa Inter Miami, David Beckham. Walakini, Chueko haifanyi kazi peke yake, nyuma yake kuna walinzi wengi ambao hutazama usalama wa Bwana Mkubwa Messi.

1704437775069.png

Ripoti zinaonyesha kuwa Chueko anaongoza timu ya wanausalama zaidi ya 50 ambao wanafanya kazi bila kuchoka kuhakikisha usalama wa mshindi huyo mara saba wa tuzo ya Ballon d’Or wakati alipokuwa Miami, wengine huwa majukwaani na wengine huwa karibu na uwanja, wapo baadhi hukaa nje kutazama hali ya usalama ila mara nyingi Chueko ndo anashughulikia usalama karibu na Messi. Hata akienda kushangilia basi Chueko anasogea karibu ili tu kuhakikisha kwamba Boss haguswi na watu wasiohusika.

1704438237979.png

Katika zama hizi ambazo usalama wa wanamichezo nyota ni jambo la muhimu sana, ustadi wa kipekee wa Yassine Chueko katika kufanya kazi yaeke unafanya usalama uwe ni wa uhakika kwa Messi kama vile alivyo Nordine Taleb ambaye ndo mlinzi wa Bwana mdogo Neymar. Ronaldo yeye amewapatia ajira mapacha wawili Sergio pamoja na Jorge Ramalheiro ambao waliwahi kufanya kazi kama Wanajeshi katika Jeshi la Ureno. Ila kwa muonekano wa huyu Chueko aisee! Mwamba anaipenda kazi yake! Hataki kuukosa ugali wake!

1704439007576.png

Chueko amepata kwenda Iraq pamoja na Afghanistan kama Mwanajeshi wa Marekani (Navy Seal) na uwezo pamoja na utaalamu wake katika usalama unazidi kumuongezea umaarufu mkubwa kwani kazi zake anafanya kwa weredi mkubwa sana. Chueko huwa busy sana kumlinda messi kuliko hata rafiki zake wakina Jordi Alba na Sergio Busquets.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom