Mfahamu Omar Bongo, Rais aliyetawala muda mrefu kuliko wote Afrika

Amani Dimile

JF-Expert Member
Jul 27, 2022
243
395
Leo katika pita pita zangu za kusoma vitabu, nakutana na historia iliyojaa maajabu, vichekesho, hatamu na mafunzo. Historia ambayo iligusa moyo wangu na kuamua kuiandika angalau wengi wao waifahamu na kuisikia.

Mimi na wewe, tunarudi miaka 88 kutoka hii leo, tunaenda kupata stori katika mkoa wa Beteke kwenye mji wa Lewai ambapo baadae palibadilishwa jina na kuitwa Bongoville Nchini Gabon (kwenye Kanda za Central African Countries)

Jumatatu moja tulivu sana ya tarehe 30 Mwezi Disemba mwaka 1935, anazaliwa mtoto wa kiume ambae alipewa jina la Albert Benard Bongo. Kijana huyu Albert Bongo alikuwa ni Mtoto wa mwisho katika familia ya watoto 12.

Tangu alipokuwa mdogo aliwashangaza watu wengi kwa uwezo wake shupavu wa kudadisi mambo na kutabiliwa makubwa kwenye maisha yake.

Akiwa na umri wa miaka 28, Bongo alipata bahati ya kuchaguliwa kwenye Baraza la mawaziri la raisi wa kwanza wa nchi hiyo alieitwa Leon M'ba. Nafasi hiyo ya kipekee ndio ilifungua safari mpya ya uongozi kwa Bongo lakini pia naweza sema ilifungua safari ya majonzi, mateso na umaskini kwa wananchi wa Taifa la Gabon.

Mnamo mwaka 1967 mwezi March Bongo akabahatika kupata nafasi ya kuwa Makamu wa Raisi wa nchi hiyo kabla ya miezi 8 mbele yaani November mwaka huo huo kutokea kifo cha raisi aliyekuwa madarakani Leon M'ba (ambae ndie aliempa madaraka Bongo ya kuwa Makamu wa Raisi) na hatimae Albert Bongo akachukua nafasi ya kuwa Raisi wa pili wa nchi hiyo tangu kupata uhuru.

Hapa ndipo utamu ulipo, fahamu kwanza Albert Bongo alikuja kuhsilimu na kuwa Muislamu mwaka 1973 na kujipa jina la El Hajj Omar Bongo Ondimba. Basi ustadhi huyo Omar Bongo alipoanza tu kukikalia kiti cha uraisi wa nchi hiyo akaanza kuiongoza nchi atakavyo yeye na wala si wananchi watakavyo na wapendavyo wao.

Hata mimi kwa akili ndogo nilizonazo nathibisha kuwa Bongo hakuwa kiongozi sahihi wa nchi hiyo maana aliinyonya nchi mpaka nchi ikanyonyeka na kumumunyika ikayeyuka mariasili zikapukutika.

Kwanza kabisa Rais Omar Bongo anasomwa kwenye vitabu mbali mbali kama kiongozi mashuhuri mla rushwa na fisadi wa kutupwa. Alikula Mali za taifa la Gabon pamoja na wazungu, akaifanya nchi ya Gabon kama shamba la Wazungu maana walichota maliasili watakavyo wao na kula nae duniani kote hasa nchini Ufaransa.

Inakadiliwa Albert Bongo alikuwa na takribani akaunti za benki tofauti tofauti 70, akaunti ambazo zilishiba fedha.

Alikuwa na majumba ya kifahari 39, Ferrari 2 gari 6 aina ya Mercedes Benz, Gari 3 aina ya Porsches na Bugatti Moja vyote alivimiliki nchini Ufaransa. Aina zote hizo si magari ya bei rahisi hata kidogo tena ukizingatia nyakati za miaka hiyo ya nyuma acha kabisa.

Mpenzi msomaji kwanza kabisa tambua huyu Omar Bongo ndie raisi aliyetawala muda mrefu kuliko wote Africa. Alikalia kiti hiko cha utawala kwa muda wa miaka 42. Alikuwa na watoto zaidi ya thelathini na moja kwa wake tofauti tofauti akiwemo Ali Bongo ambae hivi sasa ni raisi wa Gabon.

Omar Bongo aliitawala nchi kwa ubabe sana na kufanya kila alilotaka yeye. Ilifikia hatua mpaka wananchi wakamtishia maisha yeye pamoja na wanachama wake wa chama chake cha kisiasa alichokiunda yeye mwenyewe kilichoitwa Parti Democratique Gabonais (PDG)

Omar Bongo alioa wanawake wengi sana wajulikanao na wasiojulikana. Miongoni mwa wanawake aliowaoa ni Marie Josephine Kama ambae alipata watoto wawili tu kutoka kwake na akaja kumuacha mwaka 1986. Mnamo mwaka 1990 Omar Bongo akavuka mipaka ya nchi yake mwenyewe na kwenda kumuoa Mtoto wa rais Deniss Sassou Nguesso ambae alikuwa ni raisi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Binti huyo aliitwa Edith Lucie Sassou Nguesso.

Hakika wahenga hawakukosea kusema "Baniani mbaya kiatu chake dawa". Huwezi amini ingawa alifanya hayo yote ya kuila nchi ya Gabon atakavyo yeye lakini ajabu ni kwamba alitoa misaada kwa watu mbali mbali wenye shida ndani na nje ya nchi. Alizisaidia nchi kama Chad, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Angola na Burundi juu ya vita ambavyo vilikuwa vikiendelea nchini mwao. Lakin pia katika mwaka 2000 Omar Bongo alinunua kompyuta (tanakilishi) na madaftari vyote hivyo vikiwa na thamani zaidi ya maelfu ya Dola na kwenda kuwakabidhi wanafunzi wa chuo pekee cha nchi ya Gabon ambacho kinaitwa Omar Bongo University (hapo awali kiliitwa University of Gabon)

Tarehe 9 Mwezi wa 6 mwaka 2009 Malaika mtoa roho alimfikia Omar Bongo ambae alikuwa nchini Hispain katika jiji la Barcelona na kuchukua roho yake. Omar Bongo alisumbuliwa na ugonjwa wa Saratani ambao ulimmaliza taratibu mpaka kifo chake. Mazishi yake yalihudhuriwa na viongozi wa mataifa mbali mbali mashuhuri.

Baada ya kifo cha Baba mtu Omar Bongo Ondimba basi kijana mtanarifu Mtoto wa kiume wa Bongo aliyeitwa Ali Bongo ndie alievaa viatu vya uraisi wa baba ake na kuanza kuiongoza nchi hiyo hadi hii leo. Yaaani tangu kupata uhuru wa Gabon mwaka 1960 basi nchi hiyo imetawaliwa na maraisi watatu tu, huku baba na mwana wakikalia kiti hiko cha urahisi kwa takribani miaka 56 hadi hivi sasa (1967 - 2023).

Katika kitabu cha Global African History kinaelezea kwamba kuna siri kubwa nyuma ya utawala wa Omar Bongo. Taasisi mbali za kidini, freemason na baadhi ya jumuiya za kisiri za kitamaduni ndio zilimfanya Bongo akae madarakani Kwa muda mrefu. Katika hili sitaki kugusia sana maana nitaibua dhana nyingine.

. Sina mengi sana ya kusema hii ni stori fupi kati ya stori ndefu za nchi ya Gabon lakini pia za bara la Afrika.
Ahsante kwa kunisikiliza, ulikuwa nami AMANI DIMILE

Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app
 
Mtoa mada

Braza Ally Bongo nae kapinduliwa na nafas yake imechukuliwa na Braza Ngueso
 
Back
Top Bottom