Mfahamu muigizaji Katrina Kaif

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
17,463
21,188
1702067809275.jpg
Katrina Kaif ni mwigizaji na mwanamitindo wa Uingereza na India. Alizaliwa mnamo 16 Julai 1983 (Ana miaka 40 sasa) huko Hong Kong na kukulia Uingereza. Wazazi wake ni mfanyabiashara wa Uingereza mwenye asili ya India, Mohammed Kaif na Suzanne Turquote, muingereza msomi na mwanasheria.

Katrina na ndugu zake wengine 7 wamelelewa na mama yao pekee(Single mother). katika watoto hao 8, Katrina ndiyo mwenye asili ya India na Uingereza lakini wengine wana asili ya Uingereza pekee. Baba yake na mama yake walitengana akiwa mdogo sana, na baba yake hajawahi kuwasiliana naye hadi sasa.

Kabla ya kuwa mwigizaji, Katrina Kaif alikuwa mwanamitindo. Aliacha chuo huko London ili apambanie ndoto yake ya umahiri katika uigizaji huko India(Bollywood).

Mwaka 2003 alifika India kwaajili ya usahili wa filamu yake ya kwanza iliyoitwa Boom.

Filamu yake ya kwanza ilitakiwa iwe ni Saaya, ambayo angecheza na John Abraham Lakini alitolewa kwa kuwa alikuwa hawezi kuongea kihindi vizuri. Baada ya kupambana sana hatimaye alishiriki filamu iliyomtoa akiwa na Akshay Kumar iliyoitwa Namastey London.

Katrina Kaif amekuwa maarufu hadi kufuatiliwa maisha yake binafsi, ikiwa ni pamoja na mahusiano yake na waigizaji wenzake. Waigizaji hao ni pamoja na Salman Khan na Ranbir Kapoor.

Disemba 2021 alifunga ndoa na Vicky Kaushal.

Katrina Kaif ni mmoja wa waigizaji wanaofutiliwa sana na wapenzi wa filamu. Alikuwa ndiye mtu maarufu mhindi aliyetafutwa sana kuliko wote kwa mwaka 2008, 2009 na 2010.

Bado anahesabika kama ni raia wa Uingereza anayeishi India kea Visa ya ajira.

Katrina ameshiriki katika filamu nyingi maarufu za Bollywood. Baadhi ya filamu zake ni pamoja na Ajab Prem Ki Ghazab Kahani (2009), Mere Brother Ki Dulhan (2011), Maine Pyaar Kyun Kiya (2005), Singh is Kinng (2008), Jab Tak Hai Jaan (2012), Tiger Zinda Hai (2017), Dhoom 3 (2013), Tees Maar Khan (2010), Sui Dhaaga (2018), New York (2009), Bharat (2019), Bang Bang (2014) na Tiger 3 (2023).
 
Lizuri sanaa sizipendi picha za kihindi ila nikijua yupo naangalia tuu
Bila shaka filamu za kihindi ulizokuwa unazitazama ni za wale wahindi wa kusini.

Angalia wahindi wa Bollywood utazipenda mwenyewe filamu za kihindi.
 
Kuna movie amecheza na akhshay kumar na Anil kapoor inaitwa "HAMKO DEWANA KOLGAY" bonge moja ya lobe story ,Yupo na Bipasha Basu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom