Mfahamu dereva aliyetumia saa 12 Dar - Songea miaka 90

Hakuna kitu cha namna hiyo usidanganywe! Labda kama alikuwa anaendesha helkopta! Basi likiondoka Dar saa 12 asubuhi linaingia Njombe saa 12 jioni, na toka Njombe hadi Songea ni masaa matatu na nusu hadi manne. Unamdanganya nani wewe!
Mkuu Maulaga59, huyu Dereva alikuwa ni Kiboko. Ameendesha pia KISWELE na RUVUMA LINE. Pale Stand alikuwa anachelewa kuondoka, badala ya Saa 12:00 yeye anaondoka Kuanzia Saa 12:20 - 12:30 Asubuhi. Wafanyabiashara wengi walikuwa wanapenda Kupanda gari alilokuwa anaendesha ili kuwahi.

Kuna siku tumetoka Songea Saa 12:20 Asubuhi na tukafika Dar Saa 11Jioni.

Niliapa sitapanda basi ambalo yeye ni Dereva na Sijawahi Kupanda tena mpaka nimehama Songea Miaka ya 2000's. Japo nilisikia alifariki (R.I.P)
 
Usikariri

Lupelo yenyewe na Widambe zilikuwa zinaingia Njombe saa 9 ndio viwe Vyuma vya Songea!!

Okalla, Rwambo na Yoge walikuwa wanapita Njombe saa.7 na zile.Kiswele
Welldone mkuu umemjibu vema, tatizo lake anasoma uzi huu na anavutiwa nao ila hawezi kuchangia maada kila kitu kwake ni kigeni, hajui Lupelo, Safina,matema, rombo investment etc etc ni kijana wa dot.com, nimemshauri aendekwenye mada zingine hii ni JF ina mada nyingi tu
 
Mkuu Maulaga59, huyu Dereva alikuwa ni Kiboko. Ameendesha pia KISWELE na RUVUMA LINE. Pale Stand alikuwa anachelewa kuondoka, badala ya Saa 12:00 yeye anaondoka Kuanzia Saa 12:20 - 12:30 Asubuhi. Wafanyabiashara wengi walikuwa wanapenda Kupanda gari alilokuwa anaendesha ili kuwahi.

Kuna siku tumetoka Songea Saa 12:20 Asubuhi na tukafika Dar Saa 11Jioni.

Niliapa sitapanda basi ambalo yeye ni Dereva na Sijawahi Kupanda tena mpaka nimehama Songea Miaka ya 2000's. Japo nilisikia alifariki (R.I.P)
Tatizo hapo mkuu umemjibu vema ila hajui kabisa hapo umeongelea nini,hiyo Kiswele, ruvuma line hajui ni kitu gani kabisa, ukiongezea Ile ya Bin kleb CD Leyland bus ndio utamchanganya kabisa, hii bus inashusha ule mlima wa kutokea Bombambili Kuja kwenye mlima wa kupandia ili ukate kona kuingia songea (ccm makao ya mkoa),huku stendi watu wamesimama na wanaisukilizia CD ile, yaaa songea nhe ,good life kipindi hicho
 
Mwaka 1994 nilipanda Mwanahapa Video Coach ya Mbeya Arush pale Mikumi nikielekea Korogwe! Aisee ilikuwa inatembea mpaka basi.

Halafu ndani tukawa tunaburudishwa na video ya Soukouss Stars ya akina Yondo Sister, Balou Canter, Shimita, Lucien Bokilo, nk Kiukweli niliinjoi sana ile safari.
 
Ni miaka ile ya 90. Ni Likungu Trans, ISUZU MV 118, TZK6150, Dar Njombe Songea. Dereva Selepion huyo wa Katikati na aliyeshika kiuno ni Juma Ndang'o.

Alisumbua sana njia ya Songea - Dar. Alishawahi kuingia Songea saa 12 kasoro jioni akitokea Dar, dereva, alikuwa ni Selepion.

Ilikuwa ni vigumu sana kuamini kama ISUZU inaweza kukimbia hivyo. Lakini Likungu ndiyo ilikuwa hivyo. Hatari sana, watu wa Songea hawawezi sahau hii gari.

View attachment 2327670
Hivi ile barabara inayoteleza sehemu ya Njombe-Songea huwaga wanapitaje wakiwa mwendokasi? Nasikia ukicheza tu unapindua gari kwenye hicho kipande kinachoteleza
 
Ni Isuzu Mv series, 110, 118, na 120 alikuwa nazo sadiq line dar moro
Ftr ilikuwa ni version kwa ajili ya mizigo haikuwahi kuja kama basi
Kuna moja bus za tanganyika bus zilipiga Mwanza Bukoba MWANZA tarime zilikuwa moto balaa
 
Hakuna kitu cha namna hiyo usidanganywe! Labda kama alikuwa anaendesha helkopta! Basi likiondoka Dar saa 12 asubuhi linaingia Njombe saa 12 jioni, na toka Njombe hadi Songea ni masaa matatu na nusu hadi manne. Unamdanganya nani wewe!
Acha ubishi mkuu mimi nilipanda shabiby kutoka songea kuja dar na tuliingia saa 12 kamili dar, sasa enzi hizo barabara nyeupe hakuna magari mengi wangeshindwa vipi?
 
Ukweli ni siku hizi mabasi yanadhibitiwa sana.... mwanzoni mwa miaka ya 2000 kabla ya ratiba na tochi, tulikuwa tunatoka Mby saa 12; saa 4 asubuhi tuko Bismillah Ilula tunapata msosi, Saa 8 kamili tuko Moro, saa 10 tuko Dar.
 
Tatizo hapo mkuu umemjibu vema ila hajui kabisa hapo umeongelea nini,hiyo Kiswele, ruvuma line hajui ni kitu gani kabisa, ukiongezea Ile ya Bin kleb CD Leyland bus ndio utamchanganya kabisa, hii bus inashusha ule mlima wa kutokea Bombambili Kuja kwenye mlima wa kupandia ili ukate kona kuingia songea (ccm makao ya mkoa),huku stendi watu wamesimama na wanaisukilizia CD ile, yaaa songea nhe ,good life kipindi hicho
Bila kuisahau special coach
 
Ukweli ni siku hizi mabasi yanadhibitiwa sana.... mwanzoni mwa miaka ya 2000 kabla ya ratiba na tochi, tulikuwa tunatoka Mby saa 12; saa 4 asubuhi tuko Bismillah Ilula tunapata msosi, Saa 8 kamili tuko Moro, saa 10 tuko Dar.
Nimewahi kupanda basi linaitwa Lucky Star, tulifika Ubungo saa 8 mchana likitokea Mby....
 
Nimewahi kupanda basi linaitwa Lucky Star, tulifika Ubungo saa 8 mchana likitokea Mby....
Watoto wa siku hizi wanaweza kudhani ni hadithi.... lakini ilikuwa kawaida sana kufika mapema Dar, enzi za Safina etc
 
Mbona huyo cha mtoto, kulikuwa na ligi ya masia express Tzj 3360 matema beach Tzj 7104 , Tawaqal Tzk110 etc , hizi zilikuwa zikikutana dae mnaingia saa nane mchana ,yani kipindi cha dj show ya radio one ya kina mike mhagama ndo kinaanza
Hood ye alikuwa ana game lake la kuingia saa kumi Tunduma ,
Mkwema bus Msm 34 , nayo ilikuwa inaingia Tunduma saa kumi jioni , ikitokea Dar.
Matema beach Kyela ilikuwa inaingia saa 9 alasiri
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom