Meya wa Bukoba atembeza kichapo kwa mwandishi

KAUDO

Senior Member
Aug 10, 2011
138
67
Meya wa Manispaa ya Bukoba Dkt Anatory Amani ametembeza kichapo kwa mwandishi wa Gazeti la Mtanzania Audax Mutiganzi akimtuhumu kuandika habari za upotoshaji kuhusu miradi inayotekelezwa katika manispaa hasa ujenzi wa soko jipya.

Mtuhumiwa amefunguliwa kesi ya shambulio la kawaida kituo cha polisi Bukoba namba BU/RB/3161/2012.Tukio limetokea ofisi ya Meya. amani dr.jpg
 
Hebu fuatilia hiliswala utupe undani wake kwa sababu tunajua swala la soko kuu lina utata mkubwa sana na ndio maana meya anampiga mwandishi ili ukweli usifahamike; hebu makamanda livalieni njuga hili mpaka kieleweke, kuna fununu fedha nyingi zimefisadiwa kwa kutumia kampuni hewa!!!!!!!!!
Meya wa Manispaa ya Bukoba Dkt Anatory Amani ametembeza kichapo kwa mwandishi wa Gazeti la Mtanzania Audax Mutiganzi akimtuhumu kuandika habari za upotoshaji kuhusu miradi inayotekelezwa katika manispaa hasa ujenzi wa soko jipya.

Mtuhumiwa amefunguliwa kesi ya shambulio la kawaida kituo cha polisi Bukoba namba BU/RB/3161/2012.Tukio limetokea ofisi ya Meya.View attachment 54870
 
Na JK ataanza kutembeza mkong'oto kwa wale wote wanaodai ameshindwa kutekeleza ahadi zake za 2010. Bahati nzuri mimi simo!
 
Safi sana Meya wa Bukoba hawa waandishi makanyanya dawa yao ni kichapo ningefurahi sana kichapo hicho angekipata muandishi wa Tanzania Daima.
 
Mtingazi alikuwa na bia ngapi kichwani????? Tehe tehe tehe...kama namwona vile na kigugumizi chake!!!
 
MCT walivalie njuga hili,walevi wa madaraka hawa watawauweni,komaini hadi aondoke hafai kuongoza watu kama habari zilipotoshwa kwa nini asikanushe kwa ushahidi,hovyo kabisa ni sawa na timu kufungwa halafu unabamiza TV kwa hasira,what a mayor!
 
Hao watakuwa na bifu zao binafsi maana Meya si peke yake mwenye soko kiasi kwamba imuume mpaka apigane.
 
Hayo ndio matatizo ya vyeo vya kupewa.Na ninyi waandishi wa habari hamna misimamo ktk kazi zenu.
 
Safi sana Meya wa Bukoba hawa waandishi makanyanya dawa yao ni kichapo ningefurahi sana kichapo hicho angekipata muandishi wa Tanzania Daima.

Wewe nani alikuroga?

Tiba
 
Pole sana Ndugu yetu. Mbali ya kuwa wako timu moja na Mkuu wa nchi, hajaitendea haki sera ya "uhuru wa vyombo vya habari"
 
Safi sana Meya wa Bukoba hawa waandishi makanyanya dawa yao ni kichapo ningefurahi sana kichapo hicho angekipata muandishi wa Tanzania Daima.

na meya amesema baada ya huyo wa mtanzania anafuatia wa uhuru na baadae mzalendo
 
Inasemekana huyu meya ana jazba na ni mtu anayependa sifa na ana uchu wa madaraka kweli. nilimsikia redioni nilipokuwa huko mwezi wa nne akiwaambia watu kuwa atavunja soko kuu la Bukoba na kulijega upya; sasa watu wakawa wanalalamika sana.Pale SENATE (KIJIWE KIMOJA CHA KAHAWA PALE SOKONI) kukawa na baadhi ya hoja zifuatazo;
1.Kwa nini hatukushirikishwa kama wadau kuanzia mwanzoni mwa mpango mzima mpaka inasubiriwa dakika ya mwisho ambapo tumekopeshwa na mabenki, tumelipa kodi tra tayari
2.Meya aliwaambia wananchi kwamba soko litajengwa la kisasa na kwamba litawekewa mnara,ili kuwavutia watalii, na kwamba hiyo ramani kaitoa nchi moja ya ulaya sasa swali je ni mzungu ataacha mnara kwao aje kuushangaa Bukoba?
3.Ilisemekana kwamba soko lina wafanyabiashara zaidi ya 1200 ambapo kila mmoja anategemewa na watu wasiopungua 4, sasa ukilibomoa maisha ya watu karibu elfu tano yatakuwa rehani.
4.Wanaunga mkono mipango ya maendeleo na soko lijengwe, lakini itafutwe sehemu nyingine mbadala kama stendi ilivyoamishiwa Kyakailabwa likajengwe soko hilo, isaidie kupanua mji na kuongeza ajira lakini ili libakie kuwahudumia watu wachini, kwani hata soko la kisasa likikamilika bado watu hawatamudu gharama mpya za pango i.e watakuwa wamekufa kabisa kibiashara na kimaisha
5. Kwa sasa Halmasauri inauza viwanja 5000 kwa wananchi, je imeshindwa kutenga eneo la kujenga soko la kisasa?
6.Uendelezaji wa mji wa kisasa si lazima kuharibu kilichopo kwa hoja kwamba
a.ofisi ya mkuu wa mkoa ya kisasa inajengwa nje ya mji kule kahororo na ile ya regional block imeachwa
b.nssf wameacha jengo lao la old airport road na kujenga jengo jipya la kisasa pale jirani na polisi
c. hata soko kuu la Mwanza halikuvunjwa badala yake limetafutwa eneo jingine kubwa maeneo ya Ghana
d. hata uwanja wa taifa haukuvunjwa badala yake ulijengwa mwingine pembeni
7. hoja yao kuu ni kwamba soko lifanyiwe ukarabati mkubwa ikibidi hata kwa awamu lakini isiathiri hali ya maisha ya wananchi ambazo tayari ni duni,
hayo niliyaacha mwezi wa nne sielewi hadi leo imefika wapi lakini inawezekana haya mambo pamoja na mambo mengine ya kisiasa maana kuna uhasama kati ya meya wa sasa na aliyekuwepo kabla kila mtu akitaka ashinde kwa upande wake ndani na nje ya vikao
8. vile vile meya anatuhumiwa binafsi kwamba alifanya utapeli wanafunzi wa form 4 mwaka jana waliokuwa kwenye sule yake ya sekondari ya peace aliwapeleka kwao karagwe wakafanye mtihani ili shule yake isionekane haikufaulisha vizuri, kwa bahati mbaya necta ikastukia deal na kuwafutia matokeo zaidi ya wanafunzi 80 (sina hakika nayo sana lakini nayo pia nliisikia) wazazi wanaangaika sasa.
KWA KWELI KUNA MALALAMIKO MENGI SANA.

NILIACHA WANAPANGA KWENDA MAHAKAMANI SIELEWI ILIPOFIKIA.
HIYO NDIYO BUKOBA NA UKIWEPO UNAWEZA KUSHANGAA,NI MENGI, NI ZAIDI YA UIJUAVYO.
 
Back
Top Bottom