R.B
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 6,296
- 2,573
Wakili wa mlalamikiwa mbunge wa Iringa , Tundu Lisu ameshindwa kuhudhuria mahakamani hivyo , ameomba shauri hilo lisikilizwe kwa njia ya maandishi uamuzi uliokubaliwa. maandishi,Lisu awasilishe ushahidi wake Machi 26,mwaka huu,upande wa mlalamikiwa ujibu Aprili 9,maelezo ya awamu ya pili Aprili 16 na Aprili 30 uamuzi." Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
Iringa. Meya wa Manispaa ya Iringa,Aman Mwamwindi amemfungulia kesi ya madai Mbunge wa Jimbo la Iringa, Mchungaji Peter Msigwa akidai fidia ya Sh100 milioni na kuombwa radhi kwa njia ya maandishi .
Kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mwandimizi Mfawidhi wa Mahakama Mkoa wa Iringa, Juma Hassan imefunguliwa mahakamani hapo Desemba 20,mwaka jana katika Mahakama ya Wilaya ya Iringa.
Ilidaiwa mahakamani hapo jana kuwa, mlalamikiwa akiwa na nia mbaya dhidi ya mlalamikaji alitamka maneno ya kashfa mbele ya umati wa watu huku akijua kuwa maneno yote ni ya uongo na yamelenga kumharibia sifa.
Pia mahakama hiyo jana ilikubali ombi la upande wa mlalamikiwa la kutaka pingamizi la kesi hiyo ya madai inayomkabili mbunge wa jimbo hilo kusilikizwa kwa njia ya maandishi ambapo ilipangwa Aprili 30,mwaka huu kuwa siku ya kutoa uamuzi wa pingamizi hilo.
Machi 26,mwaka huu upande wa mlalamikiwa unatakiwa ujibu na Aprili 9, maelezo ya awamu ya pili yanatakiwa kuwasilishwa .