Men's Only: Sala ya Mume Mwenye Wivu

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,810
Nimeiokota hii kitu sehemu, nami nikaona si vibaya ku-share nanyi...!

Ewe Muumba nakuomba muharibie maisha mwanamme yoyote anaefikiria kuniibia mke wangu... Na kila anapotaka kutongoza basi sauti yake iwe kama ya chura au kunguru...Tena umfanye apate matende sehemu zake za siri na uzirefushe ziwe ndefu hata akivaa suruwali zitokeze nje na kila mtu azione, pia umpe maradhi ya kutoa hewa chafu kila anaposimama na mke wa mtu kwa nia ya kutongoza, na kila anapochukuwa changudoa basi umjalie Kunguni kwenye kitanda chake, mtese kwenye shopping asipate nguo size yake, zote ziwe ndogo kwake! Nakuomba mjazie chawa kwenye nywele zake, na viroboto wenye ukubwa kama mende...!

Amin.
 
Kwani mwanaume anaetembea na mke wa mtu ana kosa gani?
Hao wake zenu wanalazimishwa?
Si wanataka wenyewe?
 
Poleni sana, yani ni aibu kubwa sana mwanume kuomba dua kama hilo, ni dalili wazi kabisa hajiamini kama yeye mwanaume :cool2:
 
Kwa kile akina baba wenye wake chungeni sana wake zenu.
Wanang'ang'ania wanamme, tena mama wa watoto kumi ana-act kama 14yrs old.
 
Mkuu kwa nini usiwe mkweli kwamba sala hii ni yako badala ya kusingizia kwamba umeiokota? Kuwa mkweli mkuu maana sabato karibu inaingia.
 
Kwa wenye wanawake wenye tabia za kutoka nje ya ndoa zao basi nawashauri wawe wanasali hii mara tatu kwa siku inaweza kusaidia kama anaamin kwani IMAN IKIWA THABITI YAWEZA KUHAMISHA MILIMA
 
Kwa wale ndoa zao nawatangazia kuwa nauza kufuli za maeneo ya kati na ni nzuri hazionekani wakati wa kutembea. Hii ndio itasaidia tu manake 80% wanandoa wanatoka nnje ya ndoa. Kama unahitaji ni pm
 
Nimeipenda sana , ngoja niwe nasali hivi kila siku . Maana kuna watu wanajidai mapedeshee kwa wake za watu.
 
Nimeiokota hii kitu sehemu, nami nikaona si vibaya ku-share nanyi...!

Ewe Muumba nakuomba muharibie maisha mwanamme yoyote anaefikiria kuniibia mke wangu... Na kila anapotaka kutongoza basi sauti yake iwe kama ya chura au kunguru...Tena umfanye apate matende sehemu zake za siri na uzirefushe ziwe ndefu hata akivaa suruwali zitokeze nje na kila mtu azione, pia umpe maradhi ya kutoa hewa chafu kila anaposimama na mke wa mtu kwa nia ya kutongoza, na kila anapochukuwa changudoa basi umjalie Kunguni kwenye kitanda chake, mtese kwenye shopping asipate nguo size yake, zote ziwe ndogo kwake! Nakuomba mjazie chawa kwenye nywele zake, na viroboto wenye ukubwa kama mende...!

Amin.
dua la kuku mzee halimpati mwewe,wa kuliwa ataliwa tu,usicheze na mapedeshee wa mjini.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom