Meno ya mtoto

bombu

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,127
542

Nina mtoto mdogo ambaye ndio ameanza kuota meno, lakini kilichonishangaza badala ya kuota meno mawili ya chini, limeota jino moja ambalo limegawanyika kwa juu (ni kama meno mawili yenye mzizi mmoja). Kuna watu wameniambia kuwa liking'oka hilo jino hakutaota jino jingine katika eneo hilo. Naomba wataalam mnisaidie kunijuza juu ya hili na kipi nifanye?
 
Usitishe na maneno ya watu madamu ni toto yataota utu ondosha wasiwasi. Au muone Daktari wa meno atakupa maelekezo zaidi lakini nionavyo mimi yakitoka hayo yatakuja mengine ondosha wasiwasi.
 
Ni kweli kama alivyosema mzizi, baada ya milk teeth kutoka! Permanent teeth zitaota kwa kufata utaratibu wa kawaida! Lakini ni vema ukaenda kwa wataalamu wa tiba za kinywa na meno utajiridhisha zaidi.
 
Asanteni wakuu kwa kuntia moyo, ntajitahidi nimwone daktari wa meno kwa uhakika zaidi
 
Sioni tatizo kwasababu hayo ni meno ya utoto tu. . . angekua ameshang'oa ndo kungekua na tatizo.
 
Sioni tatizo kwasababu hayo ni meno ya utoto tu. . . angekua ameshang'oa ndo kungekua na tatizo.

asante Lizzy, ila kuna mtu alinambia kuwa hakuna dental formula ya meno mawili kwa mzizi mmoja. yaani limeota jino moja then likagawanyika kwa juu as if ni mawili, so alidai kuwa yatakapong'oka kuna uwezekano wa kutokuota na pakabaki wazi
 
Back
Top Bottom