Mengi Vs Masha tuhuma, vitisho na matokeo!

Status
Not open for further replies.
Ajiuzulu kwa nini? Kwa habari za heresay? Puuulleeeaaassse!!! Maybe Mengi aache tabia yake iliyopitwa na wakati wa kuaniki bifu zake na wananchi wengine hadharani! Amekuwa na tabia mbovu sana huyu Mengi wa ku-seek public sympathy for his behalf.

Kuhusu mauaji ya maAlbino, Masha has said it is a national problem and the serikali is trying to fix it. With all due respect to Albinos, since when have they, or any other group of people in Tanzania, had a mandate to demand a minister to resign simply because he supposedly slipped up in an interview? Come on now, killing of Albinos is a major issue that the government is looking into. Now, even the public is getting into the mix and trying to protect them also.

My 2 cents.......
 
..jamani labda nina matatizo ya kuelewa lakini statement ya Mzee Mengi hapa chini inamuondoa Laurian Masha ktk tuhuma za kupanga/kupendekeza hujuma dhidi ya Mzee Mengi.


Reginald Mengi:

“Sipendi tena kuongelea masuala haya, pia kutoka rohoni mwangu natamka kuwa nimemsamehe waziri kijana aliyekuwa anapanga njama za kunifilisi, lakini pia kumsamehe Waziri Masha kwa kuwa wote hawajui walitendalo,” alisema Mengi
..bonyeza hapa kusoma makala ya gazeti la Mwananchi

..inaelekea Mengi amesamehe Mawaziri wawili. Waziri wa kijana aliyepanga kumhujumu, na Waziri Laurian Masha.

..naona wananchi tulitumia karibu wiki nzima na kujaza kurasa zaidi ya 100 kumjadili Waziri Masha. pia tuliingiza mpaka majina[Lilian..] ya wananchi wengine wasiohusika ktk kutetea hoja zetu.

..kwa kifupi tuko palepale tulipoanzia: WAZIRI KIJANA ALIYEPANGA KUMFILISI MZEE MENGI NI NANI??
 
Last edited:
MASHA AMPA MENGI SIKU SABA
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, amempa siku saba Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, kuthibitisha madai ya kutishiwa kuuawa na suala kwamba kuna waziri anayepanga kumfilisi.
Pia amesema kuwa madai hayo ya Mengi ni mazito na umefika wakati ayathibitishe tuhuma hizo, kwani hakumtaja waziri yeyote wakati anazungumza na waandishi wa habari.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi Dar es Salaam, Masha alisema atamwandikia rasmi barua Mengi ya kutaka kuthibitisha madai hayo.
“Leo hii nitamwandikia ingawa mpaka sasa sijamwandikia barua, ili ndani ya siku saba kuanzia leo (juzi) awe amethibitisha,” alisema Masha.
Masha pia alizungumzia suala hilo juzi asubuhi wakati akizungumza kwenye kipindi cha Jambo Tanzania cha Televisheni ya TBC1.
Alisema Mengi licha ya kuwa na uhuru wa kutoa maoni yake, lakini tayari amejenga hisia kwenye akili za wananchi kuwa kuna jambo la namna hiyo, hivyo anapaswa kulithibitisha.
Masha alisema iwapo Mengi hatathibitisha madai hayo atachukuliwa hatua za kisheria ingawa hakufafanua hatua hizo.
Hata hivyo alisema madai ya Mengi kutishiwa kwa kutumiwa ujumbe mfupi wa simu, vyombo vya dola vitayachunguza na wale watakaobainika kufanya hivyo lazima nao wachukuliwe hatua.
Alisema pamoja na hayo suala la yeye kutaka abambikiwe kesi, halihitaji uchunguzi na ndio maana serikali inampa siku saba awe ametoa ushahidi wake.
Alisisitiza kuwa iwapo Mfanyabiashara huyo hatapeleka uthibitisho wowote, na kwa kuwa nchi inaongozwa kwa utawala wa sheria, mamlaka zitaangalia taratibu zipi zitumike ili mambo ya namna hiyo yasiendelezwe.
Juzi, gazeti la Uhuru lilimkariri Kaimu Kamishna wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Evarist Mangala akisema Jeshi la Polisi halina taarifa yoyote kuhusu madai hayo ya Mengi kutishiwa kuuawa.
Jumatano wiki hii, Mengi aliitisha mkutano na wanahabari na kudai kuna waziri mmoja kijana ambaye anaongoza wizara nyeti, amependekeza hivi karibuni katika moja ya vikao ili Mengi abambikiziwe kodi bandia ya kiasi kikubwa atakachoshindwa kulipa na hatimaye afilisiwe.
Aidha katika mkutano huo alisema amekuwa akipokea vitisho vya kuuawa kutoka kwa watu wasiojulikana kupitia ujumbe mfupi wa simu yake ambao wanadai amezidi kushabikia kwa kupiga vita ufisadi.
 
Mkuu una siku nne tu za kujirekebisha na kuacha kupost ujinga kama huu otherwise ccm law will haunt u.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom