Mengi kusomewa albadiri Dar es Salaam

Visomo vipo lakini sio kila kisomo kinachoweza kurudisha majibu kwa haraka basi ndio itafsirike ni Albadri.
Wengi waliouvaa mkenge wa albadri ni wale wanaolazimisha waonekane kwa watu kwamba wao ni 'makburiin"(wenyekukubaliwa na allah).
Lakini visomo vipo na nafikiri shekh wangu atakuwa anamaana ya "DUA YA ALIEDHULUMIWA" kwa sababu muislam hutakiwi kudhulumu wala kudhulumiwa.
Na unatakiwa kulipa haki ya watu kwa njia yoyote ile au kudai haki yako kwa njia yoyote ile yenye tija.na ukishindwa kupa hakiyako basi SHITAKI KWA ALLAH.
 
Kwani mapadri wanavaa nini au shimizi?

Nyie mnaotetea vyama vyenu vya siasa muwe mnajitenga na kukashifu dini za wengine maana itaonekana ndio msimamo wa chama chako.Hili nalo ni miongoni mwa sababu za kuanguka vibaya kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
 
Hapan ahlul badr ipo huwa wanafanya wasila wanawataja waliopigana vita vya badr na huwa ina dhuru sana me nlishawah kuona mtu akisomewa akafa
 
Kuna wakati huwa unatoa point bila kujali wala kuangalia kushoto au kulia.
Chanzo cha habari yako ni kipi??

Hata hivyo kwenye uislam HAKUNA KITU KINACHOITWA ALBADILI AU DUA YA ALBADILI

ETI UMSOMEEE MTU AGEUKE CHIZI AU AFE,,HUO NI UHUNI NA USHIRIKINA KAMA ULIVYO USHIRIKINA MWINGINE TUH

UISLAM NI DINI SAFI ISIYOAMIN NGUVU YA UCHAWI WALA MASHETANI
 
SHEIKH Maarufu jijini Dar es Salaam na nchini, Ali Bassaleh ametishia kusoma kisomo (albadiri) dhidi ya mfanyibiashara maarufu nchini Reginald Mengi iwapo hatalipwa fidia anayodai.

Sheikh Bassaleh amemfahamisha Mwandishi wiki hii kwamba, amefanya subira ya muda mrefu hivyo ameona wakati umefika kwa yeye kumlilia Mwenyezi Mungu (SW) dhidi ya dhuluma aliyodai kuwa imefanywa na mfanyabishara huyo.


Amesema anakusudia kusoma kisomo hicho muda wowote na atatangaza siku maalum kwa waumini wa dini ya kiislamu na watanzania kwa ujumla.


Amesema, madai ya fedha dhidi ya Reginald Mengi yanafuatia kumalizika kwa kesi ya kashfa dhidi ya chombo cha habari kinachomilikiwa na moja ya makampuni ambayo Mengi ana hisa.

Amesema, kufuatia kukashifiwa na chombo hicho cha habari, aliwasilisha malalamiko yake Baraza la habari ambako alishinda na kupewa ruhusa ya kwenda mahakamani.

"Nilimtumia Wakili Profesa Saffari, nikafungua madai, tukashinda kesi, chombo hicho na mmiliki wake wametakiwa kunilipa fidia ya shilingi Milioni 49", ameeleza Sheikh

Amesema, tangu wakati huo amekuwa akisumbuliwa, hali inayoashiria mwenye fedha ndiye mwenye haki ambaye hata vyombo vya sheria vinaashiria kutokuwa tayari kukunjua makucha dhidi yake.

Akizungumzia kisomo cha Albadiri Sheikh Bassaleh amesema, ni dua maalum, yenye utekelezaji maalum wa maombi ya mdhulumiwa ambayo huelekezwa kwa Muumba wa Mbingu na Ardhi, Mmiliki wa vyote, ambaye ndiye Mmiliki wa uhai wa Mwanadaamu, huweza kuuchukua wakati wowote atakapo.

Amesema katika mafunzo ya dini ya kiislamu, Dua ya mdhulumiwa inapoombwa kinyenyekevu haina pazia, hupokelewa moja kwa moja na kwa haraka na Mwenyezi Mungu dhidi ya aliyedhulumu na kwamba zipo aina tofauti za kujibiwa.


Miongoni mwa majibu ya Mwenyezi Mungu kwa dua hiyo ni pamoja na kuondosha uhai wa aliyedhulumu ili asiendelee kukera waja wema wanyonge au kumpa maradhi yasiyotibika kwa dawa za Hospitali wala mitishamba ili iwe ujumbe wa wazi kwa wengine.

Majibu mengine ni pamoja na kumpa aliyedhulumiwa nafasi ya juu ili kumfedhehesha aliyedhulumu au mbadala mwingine ulio bora zaidi kuchukua nafasi ya alichodhulumiwa kama mali, wasifu au heshima katika jamii.

Katika madai yake dhidi ya taarifa iliyochapishwa na chombo kinachosemekana kumilikiwa na Mengi ni kwamba, ilichapishwa taarifa yenye kumkashifu na kumshushia hadhi na heshima yake kama kiongozi wa Dini na jamii kwa ujumla.

Hata hivyo, baadhi ya watu wameendelea kumsihi Sheikh Bassaleh asichukue hatua hiyo kwa haraka kutokana na madhara yake kuto komea kwa mtu mmoja bali huusisha mlolongo wa watu wote wanaohusika kwa namna moja au nyingine.
View attachment 214123View attachment 214124
 
Albadiri ni faraja kwa wajinga tu.

Labda mseme mtamlipua kwa suicide bomber.

Kama albadiri inafanya kazi wanisomee mimi niliyesema mungu hayupo.

Frankly speaking when it comes to the issue of God Kiranga you make me sick!
Ulijiumba mwenyewe?
 
Frankly speaking when it comes to the issue of God Kiranga you make me sick!
Ulijiumba mwenyewe?

Sijaongelea mungu, nimeongelea albadiri.

Albadiri ni mungu?

Kutojiumba mwenyewe si ithibitisho kwamba mungu yupo.

Kama unakubali mungu yupo thibitisha.
 
mil 49! si mchezo kama ni kweli hiyo pesa ni halali kumdai basi dua itajibu lakini kama kuna mazingira ya dhuluma, uongo na chembechembe za kujinufaisha. potezea shekhe!
 
Back
Top Bottom