Memorandum of understanding kwa viongozi wetu - CHADEMA, CCM na CUF

More Tiz

JF-Expert Member
Mar 28, 2013
2,232
426

VIONGOZ
I WETU AMANI ZILISHINDIKANA KUPATIKANA KWA NGUVU ZA DOLA BALI ZILIPATIKANA KWA KUKAA MEZANI.

Tangu mwaka huu uanze, wananchi wa Tanzania tumeshuhudia matukio kadhaa ambayo katika macho ya wengi na dhamira ya Taifa kama Tanzania ambalo kwa sasa lina nusu karne likisifika kwa Amani na utulivu ni ya kusikitisha.

Ni taaswira gani tunataka kuijenga katika macho ya raia waliotambua kuwa Tanzania ni kisiwa cha amani, na hata ukiachilia mbali macho ya watu. Je hali hii inayoendelea nchini inatusukuma kulipeleka taifa letu mbele kimaendeleo? (Swali hili najua kila mtu atatafsiri kulingana na theories mbalimbali) lakini tunapaswa kukaa meza moja, kutafakari na kuchukua hatua ambazo zitamaliza tatizo linaloendelea na sio kutumia nguvu kama inavyotaka kuonekana kwa muda huu.

Ni dhahiri kuwa ukiona moshi unafuka ujue kuna moto unawaka mahala na dawa ya kuzuia moshi sio kuufunika bali ni kuzima moto. Mfano huu ndio unatokea hapa kwetu, Ukiona wananchi wanaanza kujichukulia sheria mikononi ujue kuna kinachowasababisha kufanya hivyo na dawa yake sio kuwazuia kwa nguvu bali ni kuzuia kinachowasababisha wananchi kufanya hivyo.

Ukijaribu kuangalia katika nchi zingine duniani, moshi ulitokea sehemu kadhaa na watawala walijaribu kuufunika moshi bila kuzima moto matokeo yake mataifa hayo badala ya kuwa rahisi kuongoza ndio yalizidi kuwa magumu na hatimaye moshi ulizidi mpaka watawala wakashindwa kuufunika, wakashindwa kuona na hatimaye kukimbia nchi zao.

Nadhani ingekuwa ni Jambo la busara sana viongozi wetu wa siasa ambao ndio injini ya mabadiliko wajaribu kukaa pamoja na wakubaliane kuwa kwa sasa kumekucha na wananchi wameshaamka na kuendela kutumia nguvu haitosaidia kuepusha tatizo bali itazidi kuongeza tatizo na itafikia viongozi wetu watashindwa hata kukaa humu nchini na kukimbia huku wakituacha wananchi tukiteseka. "Rejea Misri, …………)

Hebu viongozi wetu kubalianeni kuwa hakuna Chama ambacho kinaweza kuongoza milele, na hii ni mungu mwenyewe hakujaalia vitu viishi milele. Hivyo hakuna kiongozi atakayeweza kuishi milele, kama sisi wanadamu tunavyopata watoto tunawalea lakini inafikia kipindi wazazi wanashindwa kuwaamrisha watoto wao na kuwaambia wamekuwa na waende wakatafute maisha.
Pamoja na kuwa wanaadamu ni wagumu kukubali kiustaarabu (Njia ya mezani) juu ya vile wanavyoona vinawapa manufaa na sasa vinaenda katika mikono ya wengine, tawala nyingi hulazimisha kubaki madarakani bila ridhaa ya waongozwaji na matokeo yake machafuko hutokea halafu mwisho wa machafuko ni kurudi tena mezani, hatua ambayo huenda ilikataliwa mwanzo.

Ni ushauri wangu, viongozi wetu (Wa vyama vyote) wakae meza moja na watoe tofauti zao na matakwa ya nafsi zao na wavae matakwa ya watanzania wote ambao wanalilia kuachana na umasikini na hali ngumu ya kimaisha inayowakabili kwa muda mrefu. Kwani kwa mwenendo unayoonekana sasa kama utaachwa na ukaendelea watawazidishia watanzania umasikini badala ya kuwapunguzia tabu ya maisha yanayowakabili kwa nusu karne sasa tangu walivyosema kuwa "Afadhali tumewafukuza wakoloni waliokuwa wanatunyonya na kutukandamiza na sasa tujitawale wenyewe "

Pia nimalizie kwa kutoa rai tena kwa viongozi wetu ambao naamini hakuna ambaye hakusoma enzi za Utumwa ambapo Mtumwa alilazimishwa kumbeba Mfalme begani kwake tena kwa umbali mrefu sana kwa miaka mingi sana, lakini ilifikia kipindi watumwa walierevuka na kujifahamu / Kujitambua kiakili juu ya haki zao wakahitaji kutawalwa kwa kutumia akili sio nguvu tena, Ndipo yalipoanza masekeseke ya kudai uhuru.

Karibuni wanajamvi tusaidiane kuishauri mihimili yetu inayotuongoza.

 
Back
Top Bottom