Mr Alpha
Senior Member
- Jul 31, 2018
- 195
- 522
Jana nimelala usiku nikaskia makelele mtaani nikajua kuna binti anaolewa kuja kukumbuka badae kumbe Yanga ilikua inacheza. Azam wana masifa sana kumkanda bwana harusi mtarajiwa wa robo fainali klabu bingwa Afrika ni kumdhalilisha.
Unapoelekea kukutana na timu kubwa kama mamelodi sundowns alafu unafungwa mechi ndogo za ligi ni dalili mbaya sana tuambiane ukweli tu ndugu zangu katika imani.
Azam ni timu ya maonesho siku zote haina soka la ushindani ndio maana hata kwenye mechi za kimataifa ilitafunwa mapema tu haina uzoefu wowote sasa Yanga jana pamoja na kuchezesha mastaa wote mpaka Pacome kuumia wamepasuka inashangaza sana, sijui kocha alikua anajaribu kibuyu kipya au?
Kupoteza mchezo dhidi ya Azam ni aibu, kimkakati Mamelodi sundowns wamepata maeneo ya kuwashika na kuwafanya mpoteane kwa sasa kirahisi tu wanaangalia ubora wa Azam ulikua wapi na wachezaji mlochezesha ni wapi kisha wanaboresha na kuwaekea mijitu yao ya mtumba
Yanga na simba bado zina ushindi wa papatu papatu pangu pakavu pwagu na pwaguzi soka la janja janja nyingi halitatufikisha mbali inabidi kucheza kitimu kimkakati hatua ya robo fainali sio lele mama hata kidogo.