Membe katika tamasha la Pasaka uwanja wa taifa

Nipo uwanjani na mhe Membe ndio anaondoka hapaSi kweli Mhe Membe amezomewa ila watu wameshangilia sana pale alipogusa issues za ufisadi na ugumu wa maisha.Wananchi walifurahi zaidi pale alipotangaza kutoa millioni kumi,Pinda million 5 na Mhe rais millioni 10 kwa ajili ya kuchangia mfuko wa msama promotions kusaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu.OTIS
Kama hujazomea basi na wewe ni Msukule
 
Lema hajatua huko mmeshaanza mambo. Je akitua huko si itakuwa balaa jama!
 
Kumbe wewe unaamini idadi ya post na si ukweli? Wingi kwako ni ukweli? Wewe sio wa kujadili nae.
ukweli huletwa baada ya kukusanya evidence kadhaa kutoka kwa vyanzo tofauti.hii ndio imani yangu.
 
Lakini kumzomea Membe ni kama kumuonea bure mzee wa watu, kwa Nape hata sishangai maana alivyokuja na mbwembwe za kujivua gamba nikajua anayaweza kweli maana alivyokuwa anaongea kwa madaha huku makamera yamemzunguka nikajua basi kazi imekwisha watanzania watapunguza hasira kumbe ilikuwa geresha tu bora hata ngonjera za mzee makamba enzi zile tulikuwa tumezoea, unacheka tu kisha unapotezea!
 
Kukuta kwenye blogs sio kigezo mkuu.
Kuna watu kama nyie mlio busy kueneza uongo kwenye mitandao
OTIS
kigezo ni post ya OTIS?
Kwa nini tusieneze membe apigwa mawe taifa?au membe atukana taifa?
 
Ndugu uko nje ya uwanja au ndani? Maana sisi tulioko ndani ya uwanja huu wa taifa tunaona watu wanavyoshangilia kwa nguvu zote haswa alipokemea ufisadi, kuzungumzia changamoto za mfumuko wa bei na kuzungumzia haja ya kutumia mchakato wa katiba kuipata tanzania tunayoitaka yenye neema tele, yenye haki sawa, ambayo wananchi watafurahia na kunufaika na rasilimali zao nk.
Mimi nilikuwa ndani tena karibu na Meza Kuu. Membe alizoemewa na watu wengine walianza kutoka muda huo hasa alipoanza nimeongea na Askofu Malasusa, na Askofu sijui nani? Na Waziri Mkuu na kuwataka vijana sijui wadumishe amani n.k ALIZOMEWA hakuna kupindisha maneno hapa. Watu tunaenda kupata burudani yeye anaongozana na kundi lake la mwaka 2015 kutaka Urais hapa. Angalia orodha, Membe, Nape Nnauye, Richard Kasesela, Mary Mwanjelwa....
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Lakini kumzomea Membe ni kama kumuonea bure mzee wa watu, kwa Nape hata sishangai maana alivyokuja na mbwembwe za kujivua gamba nikajua anayaweza kweli maana alivyokuwa anaongea kwa madaha huku makamera yamemzunguka nikajua basi kazi imekwisha watanzania watapunguza hasira kumbe ilikuwa geresha tu bora hata ngonjera za mzee makamba enzi zile tulikuwa tumezoea, unacheka tu kisha unapotezea!

Hivi wewe kwa akili yako unafikili NAPE anaweza kumvua gamba LOWASA?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom