Membe kaa kimya our goverment lacks credibility since Nyerere's era

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
Wakuu nawasilisha.....

Nimeshangazwa na hatua ya Benard membe pale bungeni kutumia nguvu nyingi ili kutuaminisha kuwa serikali/taasis ya uingereza inadhalilisha taifa letu.ukweli ni kuwa sisi wenyewe ndio wa kwanza kujidhalilisha kama ilivyo desturi yetu.wote tunalifahamu sakata la rada ambalo serikali yetu iliziba masikio na mdomo mpaka juzi waziri wa mambo ya nje alivyokuja na jazba zake pale bungeni.sitaki kujikita sana kwenye suala hili la rada kwa kuwa limeshajadiliwa sana hapa jamvini,lakini napenda kumuambia mh. Membe aache kulalama na kupoteza muda wa kutafuta maendeleo.SERIKALI YETU IMEKOSA UAMINIFU!
Kama kuna mwenye kumbukumbu atakubaliana na mimi kuwa mara baada ya iliyokuwa jumuiya ya africa mashariki(defunct East Africa community) kuvunjika kuna makubaliano yalifikiwa kati ya nchi wanachama na mdhamini wa jumuia hiyo,ukiacha kugawana mali kulikuwepo na suala la mafao ya wafanyakazi wa jumuiya hii.inasemekana fedha zilitolewa kwa serikali zote tatu yaani kenya,uganda na Tanzania.
Serikali ya kenya na uganda ndio walikuwa wa kwanza kuwalipa wazee hawa,jiulize wazee wetu hapa Tanzania(WAZEE WA EAC) wamelipwa LINI au NINI?

Fedha tulipewa! na fedha hizi hazikuwa za serikali bali mafao halali ya wafanyakazi sasa nini kilitokea wasilipwe au wapunjwe?

Dhambi hii ya kutokuwalipa wazee wetu ndio inayofanya serikali yetu isiaminike!

Naomba hizo hela za BAEs zitumike kujenga mahospitali,shule na madaraja chini ya usimamizi wa NGO za kizungu halafu vikikamilika membe apewe HESHIMA ya kwenda kukata utepe!
 
BAE wakae nazo tuu izo ela mpaka Tz watakapowakamata watuhumiwa ambao wanapeta tuu mitaani
 
BAE wakae nazo tuu izo ela mpaka Tz watakapowakamata watuhumiwa ambao wanapeta tuu mitaani
tuwaulize fedha za wazee wa EAC walizifanyia nini na kuwaacha wazee wetu wakitaabika na jua kufuatilia malipo yaliyochakachuliwa.Hii ni dhambi mbaya ambayo imetendwa na serikali katika awamu zake zote.
 
Back
Top Bottom