St. Paka Mweusi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2010
- 7,639
- 4,526
Natanguliza salamu,
Jumuiya ya Afrika ya Mashariki iliundwa mwaka 1967 na kuvunjika mwaka 1977. Baada ya kuvunjika Jumuiya hii, Serikali ya Uingereza ilitoa fedha kwa ajili ya kuwalipa pensheni zao wafanyakazi wa iliyokuwa Jumuiya hiyo. Wafanyakazi wa Kenya na Uganda walilipwa pesa zao.
Hapa kwetu Tanzania ambapo Ujamaa ulikuwa umeshika hatamu ilionekana kuwa kuwalipa wafanyakazi hao fedha hizo zitakuwa ni nyingi sana, hivyo Serikali chini ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ikaamua kuzipangia pesa hizo matumizi mengine. Ikawa imeisha.
Kufikia mwishoni mwa miaka ya 90 yakaanza majadiliano ya kuunda upya Jumuiya hiyo, changamoto ikawa Tanzania na wafanyakazi wake ambao hawakulipwa stahiki zao. Makubaliano yakawa wafanyakazi hao walipwe kwanza ndiyo Jumuiya mpya ianzishwe. Kweli mchakato ulifanyika wakalipwa stahiki zao.
Cha kusikitisha ni kuwa wafanyakazi hawa walilipwa malipo waliyostahili kulipwa mwaka 1977. Serikali yetu haikujali mfumuko wa bei wala kushuka kwa thamani ya Pesa.
Unakuta mtu alilipwa 400,000/= mwaka 1999, lakini kiuhalisia thamani ya pesa hiyo haipo sawa na 400,000/= ya 1977. Laki nne ya 1977 mtu angeweza kununua nyumba nne Ilala, lakini laki nne ya 1999 mtu huyo angeweza kujenga nyumba Tegeta?
Haki iliyocheleweshwa ni haki iliyodhulumiwa, wazee hawa walidhulumiwa stahiki zao. Sasa basi tunaiomba Serikali yetu inayojali watu wake iwatazame wazee wetu hawa na kuwalipa stahiki zao kwa kuzingatia mfumuko wa bei na kushuka kwa thamani ya pesa.
Wote wenye vyeti feki na wastaafu wa EAC walikuwa watumishi, japo hawa wenye vyeti feki walighushi vyeti ili kupata ajira isivyo halali. Kwa mtazamo wangu wanaostahili malipo stahiki kati ya makundi haya mawili ni wastaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Tushirikiane kupaza sauti ili wazee wetu hawa wapate stahiki zao.
Laana zingine hawa tunajitafutia wenyewe kwa dhulma zetu.
Naomba kutoa hoja.