Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,409
- 31,394
Inawezekana ni upungufu wa kuelewa hiyo diplomacy. Nadhani balozi wa Rwanda anaelewa diplomacy vizuri sana labda kama tutachukulia Rwanda kwa 'context' ya Ehud.Mbona umeanza vizuri tu, asante sana jwa kunielewa vizuri, umemtamka Ahmedinajad, yeye ni Head of State sio sectoral minister, anazo full powers za kutamka msimamo wa nchi kimataifa. Kwa uelewa wako tu, wenye mamlaka ya kutoa misimamo ya nchi ni head of State or goverment( diplomat number 1), Foreign Minister (Diplomat number 2)na Balozi wa Nchi ambao kwa wadhifa wao ni extraordinary and plenipotential. Hiyo ndio tradition ya diplomasia. Wengine wote wataweza kutoa misimamo kwenye specific context tena wa vibali (credentials au Special Envoy).
Akitoka hapa PM Pinda akaenda kutoa kauli ambayo ikaudhi nchi ningine watakwenda foreign kutafuta ufafanuzi maan Waziri Mkuu wa tanzania hayumo kwenye order of precedence ya diplomacy. Ukishaelewa hili, wala sina haja ya kujibu hoja zako nyingine.
Barak anaweza kuongelea masuala yake ya sekta ya ulinzi lakini sio mahusiano kati ya nchi na nchi.
Balozi alisikia waziri Ngeleja(kama nipo sahihi) akisema '.......kama mauji ya Rwanda'. Waziri hakuwa katika order of precedence ya diplomacy lakini balozi kwa niaba ya nchi yake alipeleka malalamiko serikali ya Tanzania rasmi na kutaka nchi iombwe radhi.
Anyway, inawezekana Balozi wa Rwanda naye hajui diplomacy kama mimi ndio maana naweza kumnukuu na yeye anaweza kufanya kinyume cha diplomasia halisi.
Inawezekana balozi wa heshima bwana Kirikich naye pia hakuliangalia jambo hili kwa mtazamo wa diplomasia ndio maana akapeleka malalamiko kwa waziri wa mambo ya nje wa Israel na kisha sisi kupata taarifa.
Na ukweli unabaki kuwa mimi si mwana diplomasia, naliangalia jambo kwa upeo kidogo na uzooefu tu wa habari n.k.
Nakumbuka nilipohitimu kakozi kadogo nilijua najua kila kitu kwasababu nimesoma kwenye vitabu na kufaulu mtihani. Siku nilipoanza ajira niligundua kuwa kumbe yale ya kitabuni ni kunipanua uwezo wa kuelewa na kuunganisha mambo kadhaa ya kikazi, in real world kuna vitu vinakwenda tofauti na vile vya vitabuni na kuna wakati busara na uzooefu ilibidi vitumike.