EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,483
- 15,308
Serikali imesema haijapata taarifa za Waziri wa Ulinzi wa Israeli, Ehud Barak, kutoa matamshi kwamba Tanzania sio nchi muhimu kwake. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu kauli hiyo jana kwa njia ya simu, alisema kwamba hajapata taarifa kamili kuhusu suala hilo.
Hata hivyo, alitaka apigiwe simu jana mchana, lakini alipopigiwa simu yake ya mkononi ili kueleza msimamo wa serikali, simu yake iliita bila kupokelewa. Kauli hiyo kwamba Tanzania si muhimu kwa Israeli ilitolewa na Waziri Barak alipofanya mahojiano na Radio Israel na kunukuliwa na vyombo vingine vya habari vya nchi hiyo wiki iliyopita. Waziri Barak alitaja nchi muhimu na zenye maslahi kwa Israel kuwa ni Ujerumani, Uingereza na Ufaransa na siyo baadhi ya nchi maskini, ikiwamo Tanzania.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa wa Chadema, John Mnyika, alisema kupitia kauli ya kiongozi huyo wa serikali ya Israel, inaiona Tanzania sio nchi muhimu. "Tunamtaka Waziri wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa, Bernard Membe kuitaka serikali ya Israel kuomba radhi kufuatia kauli hiyo au kueleza wazi iwapo mazungumzo hayo ya Waziri Barak ni msimamo wa nchi hiyo kuhusu uhusiano wa kidiplomasia wa mataifa yetu," alisema Mnyika.
Chanzo: Nipashe
UPDATE
And the deputy minister for Foreign Affairs and International Cooperation, Mr Mahadhi Juma Maalim, told The Citizen Tuesday that the government has taken the issue seriously and is holding consultations over recent derogatory remarks.
"We are holding meetings to see how we can respond to Mr Barak's comments. We will let you know when we are ready," he said during a telephone interview. Mr Barak has refused to apologise to Tanzania after branding the country as irrelevant as far as Israel's relations with other nations are concerned.
Source: http://thecitizen.co.tz/news/4-national-news/18379-israels-remarks-raise-concerns.html