Meli yazama ziwa Tanganyika na kuua wawili

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,945
156,107
Wawili wafariki kwa ajali ya Meli ndani ya ziwa Tanganyika.

Watu wawili akiwemo kapteni wa MV. Tanganyika wamefariki kwenye ajali ambayo imetokea usiku wa tarehe 16 juni 2023

Meli hiyo ambayo ilikua ikitokea Kigoma nchini Tanzania kuelekea Kalemi nchini RDC ikiwa na mzigo wa mafuta ya petroli imepata ajali baada ya tatizo ambalo limetokea kwenye mfumo wa mashine ya meli hiyo.

Kwenye ajali hiyo watu wa wili wamefariki akiwemo kapteni wa meli hiyo ambaye ametambulika kwa jina la Bw. Florent.

Kulikua na watu 17, watu 12 wameokolewa, wawili wamefariki na watatu hawajapatikana, lakini pia meli hiyo haiku weza kuokolewa, imezama yote ndani ya maji.
 
Ajali ziwa Tanganyika ni nyingi , uwa tunasikia chache tu.

R.I.P marehemu wote.
 
Siku mwanadamu atafanikiwa kufanya shuguli zake bila ya kutokea ajali ndio itakua furaha timilifu ya mwanadamu kwenye dunia hii.
 
Polen ndugu na familia , mliopata na huo mkasa. Mungu awape moyo wa tumaini
 
Ziwa tanganyika hakutaki kujengwa daraja kama la zanzibar au bajeti yake kubwa sana?.
 
Back
Top Bottom