Meli sita zazuiwa kubeba abiria Zanzibar

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=2]Sunday, January 27, 2013[/h][h=3]
[/h]



Kampuni ya Seagull Transporter Zanzibar imesema haikuwa muafaka kwa serikali kuzuia meli kubeba abiria na badala yake kuruhusiwa kuchukua mizigo kama njia ya kuondoa ajali za meli visiwani Zanzibar.

Hayo yameleezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Said Abdulrahman Juma, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar juzi.

Alisema kwamba dawa ya kuondoa ajali za meli ni serikali kuimarisha huduma za ukaguzi wa meli na sio kuzuia meli kubeba abiria wakati zimeundwa kufanyakazi ya kubeba abiria na mzigo.

Alisema tangu kuzama kwa meli ya MV Skagit mwaka jana, Serikali imezuia meli ya MV Karama licha ya meli hiyo kuwa na sifa na uwezo wa kufanya kazi hiyo.

Alisema meli hiyo imetegenezwa nchini Marekani mwaka 1989 ikiwa na uwezo wa kubeba abiria 300 na tani 200 za mzigo lakini serikali imezuia kutoa huduma Zanzibar.
Alisema mbali na meli hiyo pia MV WETE yenye uwezo wa kubeba abiria 250 na tani 400 za mzigo imezuiwa kuchukua abiria na kuruhusiwa kuchukua mzigo peke yake.

“Tunaomba serikali kuangalia upya uamuzi wake… jambo la msingi tunaomba kuimarishwa huduma za ukaguzi wa meli na uokozi badala kuzuia wakati zimeundwa na kupasishwa kuchukua abiria na mzigo,” alisema Said.

Alisema bahati mbaya serikali imefanya maamuzi hayo bila ya kuwashirikisha wataalamu wa meli na wamiliki wake visiwani humo.

Alisema iwapo serikali itaendelea na msimamo wake wanafikiria kuhamishia huduma ya usafiri wa meli hizo mikoa ya Kusini kabla ya kufikiria kufungua kesi kupinga uamuzi huo.

Alisema sekta ya usafirishaji baharini Zanzibar inahitaji kuchunguzwa kwa kina kwa sababu baadhi ya watendaji wamekuwa wakitekeleza majukumu yao kwa kuangalia maslahi binafsi badala ya kuzingatia maslahi ya taifa.

Alisema kuna baadhi ya boti zimekuwa zikizimika kila mara baharini na wakati mwingine kulazimika kusafiri kwa kutumia injini moja kati ya Zanzibar na Tanzania bara lakini wameendelea kutoa huduma.

Alisema kampuni hiyo inakabiliwa na hali mbaya baada ya kupata hasara ya Sh. bilioni mbili tangu kuzuiwa kutoa huduma ya kupakia abiria Julai mwaka jana.

Akizungumza na NIPASHE Mjini Zanzibar Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafirishaji Zanzibar, (ZMA), Abdu Omar Maalim, alisema serikali imezuia meli sita kutoa huduma ya kupakia abiria kutokana na sababu za kiusalama.

“Haya maamuzi ni ya Baraza la Mapinduzi sisi kazi yetu kubwa kutekeleza kama wanaona hawakutendewa haki wanahaki ya kuhamisha meli zao au kuzikata na kuuza vyuma chakavu Ulaya,” alisema Maalim.


CHANZO: NIPASHE


 
Back
Top Bottom