PakiJinja
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 7,683
- 15,858
Kwa kiwango na mfumo wanaoenda nao Yanga tangu mechi za Majaribio msimu huu, hadi mechi za ushindani, ni ukweli ulio dhahiri kwamba Yanga ipo kwenye form nzuri sana.
Hali ikiendelea hivi kwa mechi tatu zijazo, basi walio chini itabidi wakaze buti tu na wamfuate hukohuko juu, kumsubiri chini itakua ni dua la kuku.
Pamoja na hayo, hali hii imeibua hamasa na furaha kwa mashabiki wa timu ya Yanga, kiasi cha wengi kujisahau na kudhani zimebaki mechi mbili ligi kuisha wakati ndiyo kwanza ni mechi ya pili.
Ni vyema sana kufurahia, ila ni vyema zaidi kuwa na akiba ya furaha na maneno, maana huu ni mchezo, wakati mwingine ushindi katika mchezo huu hautokani na ubora wa timu, bali makosa ya binaadam wote wanaohusika na mchezo, kuanzia wachezaji, waamuzi, viongozi wa timu, viongozi wa Chama Cha Mpira, viongozi wa kisiasa, afya, mashabiki n.k.
Alamsiki