Mdhamini wa Yanga Kuinunua TMK United

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MFADHILI na mdhamini wa klabu ya soka ya Yanga Yusuph Manji yuko mbioni kuinunua timu ya TMK United endepo timu hiyo itafanikiwa kuwa miongoni mwa timu nne zitakazopanda na kucheza ligi kuu msimu ujao.
TMK ambayo kwa sasa inashiriki ligi daraja la kwanza hatua ya tisa bora ikiwa chini ya kocha John William Del Peel na ikisimamiwa na mwenyekiti wake Abbas Mtevu ambapo alimkabidhi mikoba kocha huyo ambaye ameahidi kuipandisha timu hiyo yenye uchu wa kucheza ligi kuu.

Habari kutoka kwa mtu wa ndani wa timu hiyo ya TMK ni kuwa Manji tayari ameshakutana na Mtemvu ambaye ni Mwenyekiti wa TMK na kumueleza nia yake ya kuhitaji timu hiyo ambayo kwa sasa iko katika maandalizi ya mwisho ya kujiandaa na tisa bora ya ligi daraja la kwanza inayotarajia kufanyika Tanga.

Chanzo hiko kilisema kuwa Manji anania ya kuinunua TMK muda mrefu hasa kipindi ambacho anaihitaji timu hiyo ikiwa imefanikisha kucheza ligi kuu ambapo ana imani inakuwa rahisi kwake hasa kwa kujitangaza.

"Manji amekuwa na nia ya kuinunua timu hiyo ya TMK ila kwa masharti ambayo hadi ipande Ligi kuu, kutokana na TMK ambayo inafanikiwa kucheza hadi hatua ya mwisho na kutolewa katikati ila kwa mwaka huu timu hiyo ina imani itacheza ligi kuu msimu ujao na kununuliwa na bosi huyo wa Yanga" kilisema chanzo chetu.

Hata hivyo chanzo hicho kilieleza kuwa haijajulikana endapo timu hiyo ikifanikiwa kucheza ligi msimu ujao na kununuliwa na Manji kama itaendelea kuwemo katika maskani yake ya Temeke na kama itaendelea kutumia jina hilo ama laa.

"Kusema kweli suala la timu hiyo itaendelea kubaki Temeke kama ninavyojua ila sidhani kama itabadilishwa jina ama itatumia jina lake hili la TMK ambalo linatumiwa kwa sasa" kilisema chanzo chetu hicho.

Alisema kuwa suala la kupanda daraja na kucheza ligi kuu msimu huu hawana shaka wana imani kubwa na kocha wao Del Peel ambaye wamemkabidhi mikoba, pia hasa kwa kufanya usajili mzuri wa wachezaji ambao wako nao kwa sasa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom