Elections 2010 Mdahalo wa wagombea urais 2010

Status
Not open for further replies.
It is a very good idea.lakini je do we think kwamba watanzania wanachagua mtu anayejua kujieleza au wana vigezo vyao vingine?Kwa sasa Tz hatujafikia hali ya kufanya midhahalo kwa wagombea wetu kwani mpaka sasa ninavyoandika tayari watu wanajua watamchagua nani bila kujali anajua kujieleza ama la.Hayo ya midahalo labda kwenye siku za usoni lakini sio sasa ni kupoteza muda tu.

- Mkuu GS, ninakubaliana na wewe kwa 100%!

Respect.

FMEs!
 
Walahi nitatoka mafichoni na kutumia jina la kweli wakikubali na nikapewa nafasi ya kuwa muuliza maswali!
 
GS,

Hata kama watu washaamua wanamchagua Mwanasesere, kuna ulazima wa kuwaweka watu kiti moto bila kujali matokeo. Hatiwezi kusema kisa Mwanasesere inajulikana atashinda basi tusijaribu kuleta utamaduni mpya, kufanya hivyo itakuwa ni woga na kujinyima haki.

Mimi ningesema tuongeze wigo, twende hata kwa Wabunge na kwenye wilaya na tugonge watu maswali magumu wakijinyea Wananchi waambiwe ukweli wa mambo!
 
a. Kikwete hawezi na hatokuwa tayari kushiriki mdahalo wowote.

b. JF ikiandaa nani atagharimia?

Mwanakijiji

Mdahalo wa namna hii utavutia watu wengi sana kwa hiyo itavutia sana wadhamini.

Kivutio kingine ni kwamba JF haifungamani na upande wowote kwa hiyo watazamaji watategemea objectivity.

Ninaamini if you come up with a budget ya kuendesha mdahalo na kutangaza nafasi za udhamini watajitokeza tu na ninaamini kuna uwezekano wa kupata watazamani wataoweza kujunja rekodi.

Give it a shot.
 
It is a very good idea.lakini je do we think kwamba watanzania wanachagua mtu anayejua kujieleza au wana vigezo vyao vingine?Kwa sasa Tz hatujafikia hali ya kufanya midhahalo kwa wagombea wetu kwani mpaka sasa ninavyoandika tayari watu wanajua watamchagua nani bila kujali anajua kujieleza ama la.Hayo ya midahalo labda kwenye siku za usoni lakini sio sasa ni kupoteza muda tu.

Waache watanzania wachague mtu wanayemtaka hata kama wanataka kuchagua mtu kwa kuwa tu ana meno mazuri na meupe.

Mdahalo utawawezesha wale wanaivutiwa na nguvu za hoja kujionea wenyewe nani kapita kutokana na kichwa chake na nani kapita kwa kuwa ana good smile.
 
Na kama inawezekana uwebroadcasted online ili na tulio mbali tushiri kwa simu pamoja na video calls-

just an observation:target:
 
Maneno mengi ya nini, mtu anamtetea JK kwa maneno meeeengi. Weka Mdahalo JK, Slaa and others ... uone moto utakavyowaka....

Ama kweli tenda wema uendezako, mtu anasema labda Dr. Slaa asimame yeye kama yeye.. eti chama chake hakina uwezo...., wakati juhudi zote alizofanya Dr. Slaa zimefanyika akiwa na support ya Chama chake.... what a joke!!
 
It is a very good idea.lakini je do we think kwamba watanzania wanachagua mtu anayejua kujieleza au wana vigezo vyao vingine?Kwa sasa Tz hatujafikia hali ya kufanya midhahalo kwa wagombea wetu kwani mpaka sasa ninavyoandika tayari watu wanajua watamchagua nani bila kujali anajua kujieleza ama la.Hayo ya midahalo labda kwenye siku za usoni lakini sio sasa ni kupoteza muda tu.

Mkuu acha woga....! kwenye nyekundu si kweli!

when you count you start with 0, then 1, 2 ......, siku za usoni unazosema ni zipi?, inatakiwa tuweke 'presha' kubwa mwaka huu kwa kuwa tayari mabadiliko makubwa ya kisiasa yanaonekana mwaka huu kuliko miaka mingine yoyote iliyopita, cha muhimu ni kutambua kuwa juhudi zinahitajika na watawala wetu hawapendi kitu hicho kwa hiyo ni kuwalazimisha wakubali na wakikataa tunajua wameogopa nini.... kukataa kwao ni ajenda nzuri sana kisiasa ya kuwakataa viongozi wabovu.....

Ninaunga mkono mdahalo uandaliwe
 
a. Kikwete hawezi na hatokuwa tayari kushiriki mdahalo wowote.

b. JF ikiandaa nani atagharimia?

Kuonesha kuwa na yeye msomi ndio maana anakwenda kusoma speech kwenye vyuo vikuu huko marekani lakini hapa nyumbani hahudhulii hata makongamano mazito yanayoaandaliwa!! Mdahalo ndio kabisa lazima atakacha kwani yeye na wapambe wake wanaogopa kuumbuka!! Hata kama akialikwa akakacha na wengine wakashiriki, hii itaonesha weakness kwa upande wake na wananchi watakuwa wamefahamu first hand kuwa jamaa ni mwanaserere!!
 
We unatafuta balaa, JK atakimbia hawezi kutunisha kifua na akina Lipumba plus Mbowe...hana mtiririko wa kuongea thus CCM hawatakubali.

Angekuwa Mkapa ninge guarantee
 
Maneno mengi ya nini, mtu anamtetea JK kwa maneno meeeengi. Weka Mdahalo JK, Slaa and others ... uone moto utakavyowaka....

Ama kweli tenda wema uendezako, mtu anasema labda Dr. Slaa asimame yeye kama yeye.. eti chama chake hakina uwezo...., wakati juhudi zote alizofanya Dr. Slaa zimefanyika akiwa na support ya Chama chake.... what a joke!!

- It is a big joke kudai kwamba chama kilichotaka kumvua Spika uongozi kwa sababu ya mafisadi, kikidahalo na chama kilichomvua Zitto fomu ya kugombea uenyekiti wa Chadema kulinda status quo, vinaweza ku-debate na kutusaidia taifa,

- it takes just one second to think critically, kwamba you cannot be wrong and get it right in the end, huwezi kupanda mahindi ukavuna mihogo!

Respect.

FMEs!
 
Nimesoma michango yoote ya waandikaji kwenye hii mada na kufikia conclusion ya kuona kuwa ni wakati sasa wa viongozi wetu kutueleza ni nini wanategemea kufanya pindi tukiwachagua. Naomba zile zama za kugawa doti za kanga, kilo mbili mbili za sukari na shilingi elfu tano elfu tano zifikie tamati.
Ishu ya mdahalo ni muhimu, itangazwe kwenye vyombo vyote habari, luningani na redioni. Hii itawafanya washiriki (candidates) kuwa makini na nini wanachoongea ili next time, tuweze kuwahold accountable.
 
- Ndugu yangu sana Mwanzange, kwema huko uliko maana ni longtime ingawa nilipata ujumbe kule FB, unafikiri hawa viongozi watatuambia nini hasa kipya ambacho hatukjiui tayari kwamba hawana uwezo wa kutuongoza katika maendeleo, off course watasema anything kwa sababu wanajua hakuna wa kufuatilia kauli zao when it matters,

- Nani atawa-hold accountable wakati taifa zima tumesambaratika kila mmoja na lwake, unajua it is so frustrating kwamba kusingekuwa hata na sababu ya uchaguzi, wangewaapisha tu waendelee bila kupoteza hela za taifa bure, inachosha sana!

Respect.

FMEs!
 
Yeah ni long time...lakini I know ni maisha tu ndio yanatupeleka mbio.....ntakutafuta baadae...
Tukirudi kwenye mada hii, lakini honi ya kuwa at least tuanze mahali?...Maana inachosha, inaudhi, inahuzunisha na inasikitisha kuona jinsi nchi inakopelekwa.....
 
FMES,

Mbona una give up kirahisi namna hii mkuu? Ndio tunajua hatuna watu mahiri katika uongozi, mdahalo utawasaidia Watanzania wengi kuelewa udhaifu huu na hata watafakari kama kuna haja ya kuendelea na mazoea.

Just think pale Mttikila akianza kumbana Kikwete na maswali magumu na kuonyesha wazi ni jinsi gani CCM ilivyo mbofumbofu.

Think about kule kwenye majimbo atakapobanwa Sitta na kuulizwa miaka yote 40 kaleta nini cha maana Urambo na watu wakamkokotoa kwa kutumia yale maswali yangu 22 niliyowahoji Chadema kwa nini hawayatumii kwenye Operesheni Sangara.

Kampeni za Tanzania zinabidi kubadilika sura, ni ahadi zinahutubiwa zikiandamana na pilau, gagulo na hizi hongo sasa hivi mara sijui Ambulance au Msolla kuweka Umeme wa Upepo jimboni mwake ili watu wachaji simu zao bure.

75% ya Wabunge na Wawakilishi ni watu dhaifu. Hawafanyi kazi majimboni, hawatetei wananchi wao hata kuibana Serikali ila wao hukimbilia kwa Wafadhili na kukilinda Chama na serikali na kusahau kuwa wajibu wao mkuu ni kuibana Serikali kuu ili ilete maendeleo kwa Wananchi na si kutegemea misaada.

Tumechoka ahadi, tumechoka kungoja, tumechoka kuburuzwa, tumechoka kudanganywa, tumechoka kuambiwa subirini kesho tumechoka, tumechoka, tumechoka.

Tunataka mapinduzi mapya na sura mpya itakayotupa nuru mpya na pumzi mpya na hata kama mayai 20 katika trei ni mabovu, ni lazima tuwaambie wananchi ubovu wao na mdahalo ni njia moja wapo.

Ikiwa sisi hapa tunawachambua na kujua udhaifu wao, hamuoni kuwa tukianza mchakato wa kuwachambua Wabunge wote na Wawakilishi waliopo madarakani na kuwaambia wananchi wa majimbo kuwa huu ndio uchapakazi wa mbunge na mwakilisho wao na kuonyesha jinsi alivyoshindwa kuleta maendeleo au kuiaamsha serikali ilete maendeleo basi ule ugoigoi utaanza kufutika.

Tena kazi yetu ya kuchambua na kudahalo isiishie kwenye uchaguzi pekee, bali iwe ni kazi ya kudumu ya kila siku?
 
Nakuunga mkono mchungaji....siku zote common sense ni kitu cha bure kabisa kukitumia, kama kila siku tunatumia njia moja ambayo haileti manufaa, basi ni busara kubadili njia ili kupata matokeo tofauti....
I know establishment itapinga kwa misuli yote mfumo huu wa kuulizana maswali kinagaubaga....lakini itatubidi tu kuelekea huko ili kuinusuru nchi.
 
Mkuu Rev K,

Uko sahihi kabisa, hoja za mkuu FMEs zinaangalia weekness ya mtu/chama basi lakini hataki kabisa kukubali strength ya mtu/chama au weekness ina mipaka na si kwamba itazuia jambo jingine la maana lisifanyike, kwani CCM wao ni wasafi?... nijuavyo mimi 'institution au umoja wa aina yoyote lazima una maenaeo ya udhaifu na strength, sasa FMEs anasema CHADEMA hakina Demokrasia kwa hiyo pasiwe na Mdahalo!!, Ha!
 
Rostam ni meneja wa Muungwana halafu leo uwakutanishe na Mtikila anayedaiwa na Rostam, sasa eti kutakua na debate fruitable kwa taifa? CCM wanapindisha Demokrasia kila siku na Chadema nao wamejifunza hiyo tabia, sasa eti hawa mediocre wakilumbana taifa tutapata faida?

- Samahani sana wakuu na infact I am out of this debate, maana muda wa kupoteza siana tena!

Respect.

FMEs!
 
Wana JF, nakumbuka katika uchaguzi wa mwaka 2005, CCM walikataa mgombea wao kuwekwa pamoja na wagombea urais wenzake kwenye mdahalo. Sababu walizotoa tu ratiba ngumu na uchovu. Lakini alipokuwa Mwanza, alihojiwa LIVE na Star TV katika mahojiano ambayo mtangazaji wa siku hiyo alikuwa anamuuliza maswali ambayo yanamtaka Kikwete kuelezea sera zake kama vile yupo kwenye mkutano wa kampeni.

Sasa wana JF, tufanye nini ili kuhakikisha mdahalo unakuwepo katika uchaguzi wa 2010? Najua CCM hawataki Kikwete awekwe kwenye mdahalo kwani wanaujua udhaifu wake.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom