Mdahalo wa urais wa marekani live!

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
5,139
1,139
tujifunze kuendesha mijadala ya kuwapata viongozi kwa wenzetu,sio mtu anazuka tu hata hatujui alikotokea na jinsi anavyopanga na kujenga hoja tunampa uongozi,no lazima wagombea wetu wawe testedGOP Debate
 
Tatizo wagombea wetu wengi ni vilaza,ndio maana wanakacha debate....mtu anagombea tu hajui hata akishapata hiyo nafasi vipaumbele vyake vitakua ni vipi,hili ni tatizo
 
mdahalo ni njia nzuri ya kumjua kiongozi kilaza ila karibu nchi zote za Kiafrika utamaduni huu haupo hiyo ni kwa sababu viongozi wanataka kupata madaraka ili kujinufaisha wao wenyewe halafu ni waoga sana kujibu hoja za wananchi
 
wana midahalo yao flani hivi ya "kichina"...wanaandaa maswali wenyewe na kuwachagua wahariri wa vyombo vya habari watiifu kwao kujifanya ndio wanawauliza live kwenye tv.....siipendi ile kitu!
 
wana midahalo yao flani hivi ya "kichina"...wanaadaa maswali wenyewe na kuwachagua wahariri wa vyombo vya habari watiifu kwao kujifanya ndio wanawauliza live kwenye tv.....siipendi ile kitu!

ha ha ha haa... Midahalo ya kichina?! Sikuwahi kulijua hilo,labda nakumbuka ile ya urais,2010. Rose anauliza maswali ya maana,audience inauliza maswali ambayo hata kwa macho unajua ni ya kupangwa! Tuboreshe jina...midahalo ya kichinese....
 
wote tu hakuna hata mmoja mwenye afadhali,labda lipumba na zitto kabwe ndio ma good debator niliowahi kuwashuhudia so far!

Usiwe mdhaifu kaka, kama una mapenzi na Kikwete na umejisikia vibaya alivyokimbia mjadala 2010 sio sababu ya kumuunganisha Dr.Slaa humo. Kusema kuwa wote tu hakuna hata mmoja mwenye afadhali labda Lipumba na Zitto ni ujuha na kujaribu kujidanganya mwenyewe. Siku Dr.Slaa aliposema kwenye debate kuwa hata Rais Kikwete ni fisadi na ndio maana nilipomtaja kwenye orodha yangu ya mafisadi hajanichukulia hatua, pale alikuwa kwenye mdahalo au alikuwa chumbani kwako?

Unachojaribu kukifanya hapa ni kumshusha Dokta wa Ukweli ili tu afanane na dokta wenu wa kuchovya kuuridhisha moyo wako. Huyo Lipumba huzungumza hizo hizo pumba mikutanoni na kwenye midahalo. Ukitaka kusikia mambo mazito na yenye uthibitisho basi tune to Daktari Slaa. Na kamwe hajawahi kukwepa mdahalo, be fair to yourself.
 
We una stresses zako za maisha ni wapi nilipomtaja Dr slaa ama kikwete,mimi nimewataja watu wawili ambao kwangu mimi,simlazimishi mtu wae kama mimi,nawakubali kwa kuwa ni nimeshawaona sehemu mbalimbali wakishiriki mijadala na kufanya vizuri!wewe unaweza kuwa na list yako ya unao wakubali haimaanishi na mimi lazima niwakubali!unasema mapenzi yangu kwa jk sasa mbona sikumtaja kama kweli nampenda sana huyo mtu,msipende kuchanganya kila kitu na ushabiki wenu wa vyama,msidhani kila mtu ni mwanachadema au mwana ccm!
 
Mdahalo????labda kwa chama au mtu msafi lakini kwa mtu mchafu dhamira itakuhumu tu lazima ukimbie tu hao waliowahi kukimbia walipima wakakuta hawana kitu cha kusema na kudanganya wakaona picha haitaenda CDM go,go CDM.
 
mdahalo ni njia nzuri ya kumjua kiongozi kilaza ila karibu nchi zote za Kiafrika utamaduni huu haupo hiyo ni kwa sababu viongozi wanataka kupata madaraka ili kujinufaisha wao wenyewe halafu ni waoga sana kujibu hoja za wananchi

Ndio maana wakubwa wanakula corner wakisikia mdahalo! Hata telephone conference za wakubwa ni watu wa Usalama wa Taifa ndio wanaopewa nafasi, wewe mlala hoi. mfurukutwa ukitaka kupiga line busy kila wakati. This is bongo!
 
Back
Top Bottom