Mdahalo wa UDA Live on Star TV: Updates

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
1,025
475
Masaa Manne kutoka sasa Star TV kupitia kipindi cha Tanzania Tunayoitaka kinachoendeshwa na Rosemary Mwakitwange wataendesha Mjadala kuhusu sakata la UDA lililojaa sura tofauti kwa sasa

Updates zitapatikana hapa kwa kadiri mjadala utaklvyokuwa ukiendelea.

Kwa kuwa anasoma hapa pia muda huu kabla ya mjadala huo wadau tunalitazmaje hilo na nini hasa kinaweza kuwa cha msaada kwa muendesha kipindi hicho

Mjadala utaanza saa 12 kamili jioni

ADIOS

Kama anasoma hapa basi ninauhakika kapata data nyingi mno kutoka kwa thread za Invisible, Mwanakijiji na wengineo, kitu cha muhimu ni kuwa mali ya Umma irudi kwa wenyewe period

Huu sio muda wa kuvuna shamba la bibi!! Hawa wawekezaji uchwara watuachie shirika letu, Labda huku tuendako Mungu anaweza kutuletea wenye akili na wakatukomboa hapa Tulipokwama!!

Kama anasoma hapa basi ninauhakika kapata data nyingi mno kutoka kwa thread za Invisible, Mwanakijiji na wengineo, kitu cha muhimu ni kuwa mali ya Umma irudi kwa wenyewe period

Tatizo ni Utayari. Maana hawa jamaa kama wako labelled na element fulani za anti-government, wanatoa Hoja zenye ujazo ila watanzania vichwa ngumu

Nafanya maarifa kumpata mwezeshaji kutoka Star TV awasilishe mawazo haya yatakayochangiwa hapa

Wazungumzaji ndio watuhumiwa wa Ufisadi Mayor Makaburi ahh sory Masaburi, na Mteja wake Simon Group hapo ukweli utakuwa wa upande mmoja maana deal yao wote. Tusubiri tuusikilize na kuangalia

Maoni yangu: Ipendekezwe kwenye hicho kipindi kuwa suruhisho la matatizo ya viongozi wanaotufirisi kupitia nyadhifa tunazowapa "za umma" na wanajali matumbo yao kwa ghalama ya jasho la wanyonge WANYONGWE kama uchina maana hatuwezi kuendelea kuwa na UTAWALA BORA na HAKI ZA BINADAMu huku wakifaidi wachache na wengi wakizidi kutaabika. mijadala itakuwa mingi, tume zitaundwa nyingi bado suluhu hamna maana wao wamekaa pembeni wanatucheka sisi tunalaani na kukemea wao wanaingiza siku so ki-vitendo zaidi tuachane na u-magharibi tujaribu kuwa wakali japo kwa kuweka pembeni sheria ya haki za binadamu kwa makosa fulani kama rushwa na uujumu uchumi na tusisikilize kelele za mnaowaita wadau wa maendeleo. Baada ya kubadilisha mfumo-wizi uliojengeka tutarejesha hayo matakwa ya haki za binadamu na utawala bora.
nawasilisha.

Masaa Manne kutoka sasa Star TV kupitia kipindi cha Tanzania Tunayoitaka kinachoendeshwa na Rosemary Mwakitwange wataendesha Mjadala kuhusu sakata la UDA lililojaa sura tofauti kwa sasa

Updates zitapatikana hapa kwa kadiri mjadala utaklvyokuwa ukiendelea.

Kwa kuwa anasoma hapa pia muda huu kabla ya mjadala huo wadau tunalitazmaje hilo na nini hasa kinaweza kuwa cha msaada kwa muendesha kipindi hicho

Mjadala utaanza saa 12 kamili jioni

ADIOS

Nipo hapa naona mafundi mitambo wanafunga mitambo mpaka wamevua mashati yao! Ingawa mimi simtaalamu wa mitambo maeneo waliyofungia hili dish lao hapa Moven Pick msishangae mitambo kukatikakatika!!

Nipo hapa naona mafundi mitambo wanafunga mitambo mpaka wamevua mashati yao! Ingawa mimi simtaalamu wa mitambo maeneo waliyofungia hili dish lao hapa Moven Pick msishangae mitambo kukatikakatika!!

Good kama upo eneo la Tukio. Tatizo si eneo ishu ni capacity ya signal na ilipo satelite, sogea karibu yao chungulia hapo lazima watakuwa na monitor screen au analyzer itakuonyesha Percentage ngapi ya signal wamepata na kama ni above 70 hata inyeshe mvua ya mawe hapatakuwa na shaka ya kukatikakatika kwa mawasiliano

Kuna runinga wameweka hapa nje kwenye dish lao! Kwa kuwa sina tiketi ya kuingi ndani nimeamua kukaa hapahapa nje na nitafuatilia mdahalo huu hapa! Mlio mbali nitawajuza japo kwa uchache!!

cha msingi masaburi wazungumzie ni namna gani jiji linaweza kuwa safi, kupunguza msongamano na kupunguza tatizo la vijana wasio na ajira katika jiji letu kwani mambo yao ni ya kisiasa zaidi, pia walete mpango mbadala wa kuhakikisha ya kuwa waindi na wachina wanaofanya biashara wawe na vibali na watambulike na afisi za uamiaji na walipe kodi stahiki.....pia jiji lishirikiane na TRA kudhibiti wafanyabiashara wanaouza vitu kariakoo na maeneo mengine bila kutoa risiti au kutoa risiti zisizo na record

wacheni siasa wakati nchi hii makampuni ya simu yanakwepa kodi na wageni wanafanya biashara bila vibali na wanakwepa kodi , sasa si muda wa maneno ni muda wa vitendo watanzania tumechoka na tuhuma za ufisadi zinazoishia kwa michezo ya kujivua gamba bila kuchukua atua
zozote

kampuni za simu zinakwepa kodi kubwa zaidi ya fedha zinazoliwa na mafisadi kwa hiyo fisadi namba moja ni VODA,TIGO,AIRTEL. na kampuni za madini

Wageni ndo wamefika,meya wa jiji la Dar hayupo ana udhuru,amealikwa ikulu!

Nani hasa ni mmiliku wa UDA hilo ndo swali la kwanza, maswali yote yanaulizwa na mwenyekiti kwa dakika 30 za kwanza.

Back
Top Bottom