MDAHALO WA IJUMAA: Waziri Mkuu akiachwa na wengine kubadilishwa itaridhisha?

Ukosefu wa uwajibikaji wa PM ndio sababu nyingine iliyosababisha uovu, wizi ama kutowajibika kwa mawaziri waliotajwa. Kutokana na hilo, hapa Mawaziri ni matawi ya mti uliokosa uwajibikaji wakati PM ndie shina lenyewe. Najua ni kupoteza muda kwa sasa kujadili mzizi....vyovyote iwavyo kwa sasa, huwezi kung'olewa (mzizi). Shina goi goi mara zote litatoa matawi goi goi! Hivyo basi, kuwaondoa mawaziri peke yake pasipo na kumwajibisha PM, ni sawa na hakuna kwa vile hata wale maziri watakaokuja hapo baadae atashindwa kuwasimamia na hatimae kurudi tena uovu ule ule!
Hilo la mafao ya PM kuja mapema zaidi nazani ni mada pana inayohitaji mjadala hususani katika mchakato wa katiba mpya. Hapa lazima pawe na sheria kwamba inapotokea PM au Rais ( na wengine kama hao) amejiuzuru au kuachishwa kazi kwa kashfa inayohusiana na ukosefu wa uwajibikaji, ufisadi au jambo lolote linalotishia maslahi ya taifa basi muhusika asiwe asipate stahiki ambazo angezipata endapo angemaliza muda wake wa utumishi! Na kama ni lazima apate basi labda iwe kiasi tu....kinyume chake, tutakuja kupata kiongozi aliyekaa madarakani chini ya mwaka mmoja halafu taifa likalazimika kugharamia maisha yake yote! Hii si sawa!
 
Kama tunataka ku-deal na tatizo la ufisadi na uwajibikaji wa mawaziri, suluhisho sio kubadilisha Baraza au kuleta awamu nyingine ya CCM, bali ni kuleta utawala mpya kabisa wa chama tofauti. Chama tofauti kikiingia kina jeuri ya kufumua uozo wote uliofanywa zama za Mwinyi, Mkapa, na JK. Lakini kama ni mawaziri wa CCM, tusitegemee lolote la maana.

Ufisadi wote mkubwa unaofanyika, una mikono ya Ikulu. Ufisadi mkubwa uliofanyika zama za Mkapa, JK ameshindwa kushughulikia, maana akisema ashughulikie mwisho wa siku Mkapa na watu watakwenda Segerea na JK hayuko tayari hilo. Hata akija mwingine yeyote kutoka CCM, stori itakuwa ni hiyo. Mawaziri wakipewa "ulaji" [wakiteuliwa] wanaendeleza ufisadi kwa kuwa wanaamini kwamba yeyote mwingine atakayekuja kuteuliwa hatakuja kufunua mdomo kumwangamiza, so wanaendelea kutafuna kama mchwa au dumuzi (scania).

tatizo la nchi hii ni kufikiri ya kuwa ukiwaondoa baadhi ya watendaji na kuwaleta wengineo basi matatizo yamekwisha la hasha............ila matatizo na kashfa hubadili sura tu.......majibu ni kuangalia kwa kina mfumo mzima wa uendeshaji wa nchi na hii serikali ya ccm haina baraka au hata rekodi ya kuurekebisha ............angalia jinsi wanavyopambana kuuchakachua utaratibu wa kuandika katiba mpya ili waweze kuiandika watakavyo kupitia tume ambayo wao wenyewe wameiteua................ccm sasa ni wapinga marekebisho ya mfumo lakini nao hulalamika kila siku na wako madarakani.....hili linashangaza sasa wanamlalamikia nani?

JK is the biggest problem lakini yeye ataendelea kutuvuga kwa kuwalaumu mawaziri wake ili kufunika mapungufu makubwa yake binafsi ya kiutawala..........madaraka ya kuubadili mfumo ili kuongeza uwajibikaji anayo lakini hawwezi kutumia madaraka yake kwa sababu kwanza hana ujuzi wa kufnaya hivyo kwa sababu yeye ni matokeo ya mfumo wa kubebana..........
 
Kubadilisha baraza la mawazili bila kuchunguza na kubadilisha mfumo mzima wa uendeshaji wa serikali yetu ni mabadiliko ya kinadharia tu,theory za wizi bado ziko palepale.
 
Nimeuliza hili kwa sababu dalilii ya kukamilika kwa illusion kunakaribia! Kwamba, wataingia wengine na WM atabakia, JK atabakia na tutaambiwa "tuwape nafasi" na kuwa "hawa wanafaa"!!!

Kwanza ni kweli haitaridhisha.

Pili hii illusion inaweza ikikamilika na huenda itawapa ccm nafuu ya muda mfupi ila CDM wakiwa makini ni mtaji wa muda mrefu. Kwa sababu sababu zile zile za kuwaondoa hao mawaziri kadhaa ndio hizo hizo zimeenea serikalini mwote anzia Rais mpaka serikali ya mtaa i.e. ufisadi, ubadhirifu, uzembe, ufuska nk nk; so ni kuwa more strategic by keep the masses focusing on really the main agendas.

Tatu, who really cares?
 
Diapers%2BAnd%2BPoliticians%2BShould%2BBe%2BChanged%2BOften%2BBoth%2BFor%2BThe%2BSame%2BReason.jpg


hivi wewe huchoki?


Ulishawahi kuisikia nyimbo ya zamani ya Kiunguja "fitina mbaya wala hana haya".

Mwenye kilema na mapungufu yake hayaachi, huyu ni fataani ambae hana uwezo wa kujionesha hata sura yake, anajificha nyuma ya keyboard yake akifitinisha watu kila kukicha.

Analysis zangu, kwa huyu kaka/dada anaejiita mzeemwanakijiji:

Ni mtu mfupi sana, aliyeshindwa kufanikiwa kimaisha na ana hamu ya makubwa ambayo hawezi kuyafikia kwa kuwa hana mvuto kimwili na ki personality, huwa hana mwanamke kama ni mwanamme na hana mwanamme kama ni mwanamke. Hana urafiki na hana mazowea ya kutembelea au kutembelewa na watu. Ni mtu mpweke sana kwa kuwa hajiamini kutokana na kujiona kuwa hana mvuto kimaumbile. Ni mtu ambae alikuwa "abused" utotoni amma sexually amma physically na alikuwa hapewi nafasi ya kuwekwa bila uoga na walezi wake, kitu kilichomfanya mpaka leo achukie kila mwenye mafanikio kwani anadhani kuwa yeye anajuwa zaidi ya wengine ila tu kajijengea pazia la kutojiamini kutokana na maumbile yake. Amma ana kifaa kidogo sana kama ni mwanamme amma ana shimo kubwa sana kama ni mwanamke.

Njia pekee ni kufitinisha kila anaemuona ana jina na mafanikio. Watu kama huyo huwa hawachoki mpaka siku ya kufa na hakuna wanachofanikiwa.
 
Wenye akili zao wanajadili ISSUES Wewe na mwenzako mpo busy mnamjadili mwanaume, eti mfupi hana mke.....kama mbataka mchumba nendeni facebook mtapata.

Utumwa mwa fikra ni mbaya sana.
Diapers%2BAnd%2BPoliticians%2BShould%2BBe%2BChanged%2BOften%2BBoth%2BFor%2BThe%2BSame%2BReason.jpg


hivi wewe huchoki?


Ulishawahi kuisikia nyimbo ya zamani ya Kiunguja "fitina mbaya wala hana haya".

Mwenye kilema na mapungufu yake hayaachi, huyu ni fataani ambae hana uwezo wa kujionesha hata sura yake, anajificha nyuma ya keyboard yake akifitinisha watu kila kukicha.

Analysis zangu, kwa huyu kaka/dada anaejiita mzeemwanakijiji:

Ni mtu mfupi sana, aliyeshindwa kufanikiwa kimaisha na ana hamu ya makubwa ambayo hawezi kuyafikia kwa kuwa hana mvuto kimwili na ki personality, huwa hana mwanamke kama ni mwanamme na hana mwanamme kama ni mwanamke. Hana urafiki na hana mazowea ya kutembelea au kutembelewa na watu. Ni tu mpweke sana kwa kuwa hajiamini kutokana na kujiona kuwa hana mvuto kimaumbile. Ni mtu ambae alikuwa "abused" utotoni amma sexually amma physically na alikuwa hapewi nafasi ya kuwekwa bila uoga na walezi wake, kitu kilichomfanya mpaka leo achukie kila mwenye mafanikio kwani anadhani kuwa yeye anajuwa zaidi ya wengine ila tu kajijengea pazia la kutojiamini kutokana na maumbile yake. Amma ana kifaa kidogo sana kama ni mwanamme amma ana shimo kubwa sana kama ni mwanamke.

Njia pekee ni kufitinisha kila anaemuona ana jina na mafanikio. Watu kama huyo huwa hawachoki mpaka siku ya kufa na hakuna wanachofanikiwa.
 
nahisi tumbo la kuhara kila uchao sababu ya haka kanchi kailkokosa msimamizi
 
Ni wazi kuwa endapo Rais atabadilisha mawaziri na kuwaondoa wale nane wanaotuhumiwa, kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu haitafanyika na hata kama ikifanyika haitapata uungwaji wa mkono na wabunge wa CCM.

Kitu kikubwa cha kuzingatia hapa ni kuwa kwa mujibu wa katiba yetu sasa waziri mkuu ni sawa na head prefect. Head prefect hana mamlaka ya kuwawajibisha ma-prefect wengine zaidi ya yeye kuwashitaki kwa walimu. Kwa kifupi waziri mkuu wetu anasimamia zaidi wizara ya tawala za mikoa na serikali za mitaa na pia ni kama coordinator wa mawaziri wengine katika kusimamia shughuli za maendeleo katika miji na vijiji.

Kwa maoni yangu ni kuwa mtu wa kulaumiwa na ufisadi unaoendelea ni rais mwenyewe!

Katika mabadiliko ya katiba hatuna budi kujadili ama kuwa na waziri mkuu mtendaji, kwamba akishateuliwa na kuthibitiswa na bunge awe na uwezo wa kuteuwa mawaziri wake mwenyewe na yeye awajibike kwa rais moja kwa moja au tuwe na mawaziri wasio wabunge wapendekezwe na rais wakishirikiana na waziri mkuu na kuthibitishwa na bunge. Kwa maana kuwa wabunge wawe na uwezo wa kumuwajibisha waziri ye yote:glasses-nerdy:
 
Kimbunga: Kwa maelezo yako sasa naona Waziri mkuu atawekwa rehani ambayo itakuwa inapanda bei kadri tunavyoelekea 2015, tutarajie misuguano zaidi ndani ya CCM ikisaidiwa na nguvu ya umma, wabunge hawawezi kukaa kimya wakiona wanainchi wanazidi kuwa hoi kisa wao wanatoka upande wa CCM, Wengi wao wamepita kwa taaabu sana na CCM yao toka majimboni kwao hilo wanalijua vizuri tu, hivyo hawatakubali 2015 kazi iwe kubwa mara mbili na amini maneno yangu kabla ya uchaguzi wa 2015 upinzani utavuna mavuno makubwa sana mpaka watakosa maghala.

Mkuu vipik2 hayo mavuno hakika yatakuwepo kuelekea 2015 kama CCM hawatafanya radical reengineering kwenye chama na serikali ili angalau hii miaka 3 iliyobaki CCM itengemae japo kidogo. Mavuna yameanza kwa kuwa ukiona kuna uasi wa wabunge ujue kabisa kwamba Party Caucus ambayo tuliizoea kuzima baadhi ya hoja imeshindwa kufanya kazi. Ukiona badala ya hoja kunakuja vitisho kwamba nikifika Dodoma mtanitambua basi ujue mavuno yanasubiri kuingia tu ghalani.

Lakini CCM bado wana nafasi ya kujitengeneza isiwe sikio la kufa halisikii dawa.
 
Last edited by a moderator:
Naona System Ndio Tatizo!! sisi wenye nchi Tunachotaka na Hawa Wahujumu Uchumi Tuwaone wakifuatiliwa na Takukuru na Kwenye Mahakama wakijibu tuhuma zao!! Sio watu waendelee Kuponda Mali walizochuma Kifisadi (usd 410,000 kwa miezi 16!!!!!) Halafu tusema kubadilisha inatosha!! That is a joke!!
Pia waziri Mkuu ameprove failure ya kuwasimamia mawaziri wenzake na sioni sababu yoyote ya yeye Kuendelea Kuwepo
Tumkumbuke mzee wa kararacha alionjeshwa Unaibu mkuu kidogo ila alifanya wonders!! Sasa iweja kwa huyu full Waziri Mkuu unashindwa Hata kuwajibisha mkurugenzi wa Halmashauri? Kuna Haja gani sasa ya Huyu Mtendaji?

duh! Nionavyo hawa watendaji wanaopewa nafasi hizi ni kama hawana meno ya kung'ata (sport dog) ama wapo kama vile geresha lakini mambo yote ni kwa rais tht why kama utakumbuka siku waziri mkuu alipokuwa anatoa majibu kuhusu madudu ya aliyekuwa katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini alisema kuwa kama angekuwa yeye ndo aliyemteuwa angejua la kumfanya kwa maana nyingine yeyote anayeteuliwa na rais waziri mkuu hana uwezo wa kumfanya lolote suluhu ya haya yote ni katiba mpya au CHADEMA kukamata nchi tumechoka kubadilishiwa viongozi hali ya kuwa uwizi bado unaendelea hata kama baraza likibadilishwa hakuna jipya shehe ni yuleyule bali kanzu ndo tofauti
serikali hii ni ya kulindana ya kishkaji chukua chako mapema
 
Nionavyo hata wa kibadilishwa madudu ni yale yale tu hawa majamaa wameshatuzoea wa tz kwamba tukipiga sana kelele wanafanya change kwa baadhi ya mawaziri thn tunanyamaza kimya kinachofanyika ni shehe yule yule kanzu ndo tofauti
suluhu ni katiba mpya au chadema kushika nchi kabla hatujauzwa
waziri mkuu ni kama anaonewa au hana meno ya kung'ata yupo pale kama urembo tu (sport dog) kama utakumbuka wakati alipokuwa anajibu zile tuhuma za aliyekuwa katibu wa wizara ya nishati na madini bwana jaairo
PM alisema kuwa kama angekuwa yeye ndo rais siku ile ile angemwajibisha
kwakuwa serikali ni ya kishkaji na ya kulindana inabidi kila anayeteuliwa achukue chake mapema thn asepe
anajua kuwa akibainika ataondolewa bila kuwajibishwa
na wtz kama kawaida yao watanyamaza kimya
mkapa, chenge, rostam, karamagi, mramba, sumae, ngeleja. Meghji, balali, liyumba, mahita, wametufikisha hapa tulipo
 
nimeuliza hili kwa sababu dalilii ya kukamilika kwa illusion kunakaribia! Kwamba, wataingia wengine na wm atabakia, jk atabakia na tutaambiwa "tuwape nafasi" na kuwa "hawa wanafaa"!!!
walipokwama ni kwamba kuna mahala ipo sheria aidha ya uchaguzi au katiba kwamba baraza la mawaziri likishavunjwa mara mbili basi waziri mkuu wa tatu atatoka katika chama kilichoshinda uchaguzi mkuu wa mwisho nafasi ya pili mpo hapo?ndo hapo magamba wanapoona kama wamebeba gunia la misumari kichwani na hao mawaziri wapya anawateua toka wapi maana rais alikuwa na nafasi saba kisheria na tatu alishatumia wanaotakiwa kutolewa mawaziri nane!! Tunafanyaje? Wanaoelewa zaidi watuelimishe
 
Hakuna Waziri hata mmoja atakayeondolewa kwa Tz ninayoifahamu, badala yake watabadilishiwa wizara tu
 
Badala ya kuvunja baraza kama wengine wanavyotarajia au kutegemea Rais anaweza kufanya tu mabadiliko makubwa (major reshuffling) ambayo yatagusa karibu wizara zote lakini yasimguse Waziri Mkuu. Hii itakuwa ni katika kuonesha kuwa ana imani na Waziri wake Mkuu lakini hana imani na mawaziri wengine na itakuwa ni njia rahisi ya kupunguzia serikali mzigo wa kikao cha Bunge kumpitisha Waziri Mkuu mpya au kutengeneza WM wa zamani ambaye ataanza kupata mafao ya ki-waziri mkuu mapema zaidi kuliko kama angeachwa kumaliza ngwe nzima.

Najiuliza zaidi kuwa kama WM ataachwa kura ya kutokuwa na imani naye bado itaendelea kwani ilikuwa predicated na wazo kwamba mawaziri wakijiuzulu au kuondolewa basi WM hatopigiwa kura ya kutokuwa na imani naye...?
Bado nabaki kuamini kuwa huyu PM tuliyenae bado ni mzigo mzito sana TZ..i mean..the guy has no guts yaani.....yupo yupo tu...anaomba muda wake ufike apate haki zake za kustaafu apumzike....hana jipya Pinda.....na ndio sababu hata mawaziri wanajifanyia wanavyotaka maana hawafatiliwi na PM....yeye Pinda anaganga njaa tu muda wake uishe....bado naamini kama JK atataka aone mabadiliko ya utendaji wa mawaziri wake...yabidi aanze kwa kumuondoa PM....amweke PM mkora atakae deal na mawaziri ipasavyo..i mean mtu type ya Magufuli......mtu asiye na mzaha mzaha..maana Pinda hana kauli yaani.....watu hili wanatakiwa walijue...pamoja na kwamba si mwizi...lakini he is too slow...we need a very firm PM...atakae deal na mawaziri wazembe immediately......Pinda hana hiyo jeuri...you can see it in him......mifano tunayo mingi sana tu....refer kilio chake bungeni...kwenye issue ya albino....au issue ya jairo..au madaktari walivyomtoa jasho......Pinda is a very very weak PM........
 
Solution hapa ni mpaka Wabunge wa upinzani wawe zaidi ya nusu wa chama TAWALA ndio serikali hii itashika adabu ! vinginevo tunapoteza muda bure!
 
Wenye akili zao wanajadili ISSUES Wewe na mwenzako mpo busy mnamjadili mwanaume, eti mfupi hana mke.....kama mbataka mchumba nendeni facebook mtapata.

Utumwa mwa fikra ni mbaya sana.

Kumbuka wengine tumebobea katika psychoanalysis na tunamsoma mtu kwa maandiko yake tu. Hata wewe unaonesha ni mvivu wa kutupwa.
 
Back
Top Bottom