Mdahalo ni muhimu kwa wagombea urais

ngumarwa

Member
May 15, 2015
12
13
Mdahalo ni muhimu kwa wagombea urais
Takribani mwezi mmoja umepita Tangu , Baraza la Habari Tanzania (Media Council of Tanzania) kwa kushirikiana na taasisi nyingine kadhaa, ikiwemo Twaweza, Kutoa mialiko kwa vyama vya siasa vilivyosimamisha Wagombea wa nafasi ya urais juu ya kufanyik akwa mdahalo kwa wagombea wote vyama vyote wa nafasi ya urais nafasi ambayo ni ya juu kuliko zote kwa mujibu wa katiba yetu . Wapenda demokrasia ya kweli tunapenda kuwapa pongezi , Baraza la Habari Tanzania (Media Council of Tanzania) na taasisi zingine zinazoshiriki kuandaa Mdahalo huo ambao utatupa nafasi ya kuwaona na kuwapima wale wanaotaka kupewa fursa ya kuiongoza nchi yetu miaka mitano ijayo. Tunataka yale kuyaon n kusikia yale ambayo hatuwezi kuyaona wal kuyasikia katika majukwaa ya kisiasa katika kampeni. Tunataka kuona uwezo wa wagombea katika kujenga hoja na si kupiga porojo. Midahalo pia itatusaidia Watanzania kuona na kuwapima wagombea wote wa nafasi ya urais kwa ufundi wao wa kujenga hoja na kutetea hoja pamoja na ufundi wa kushindana kwa hoja na fursa ya kushindana kwenye jukwaa moja angalau mara moja. Pia umoja wa wagombea kwenye mdahalo ni miongoni mwa mambo yanayochangia umoja wa kitaifa. Tukiwaona katika Mdahalo Mama Anna Mghirwa, Chief Yemba, Fahm Dovutwa Edwarad Lowassa, Hashim Lungwe, Janken Kasambala, Dk. John Magufuli pamoja na Maxmiliani Lymo wanakumbatiana baada ya mdahalo Tatajifunza kuwa siasa si ugomvi bali siasa ni utaratibu wa kupingana kukubaliana na kutokubaliana kiungwana na kufanaya mambo yaendelee vema hata baada ya October 25. Hata hivyo kuna uwezekano mkubwa kwa mdahalo huo kutofanyika baada ya umoja wa katiba ya wananchi ukawa kutotaka mgombea wao wa nafasi ya urais Edward Lowassa kutoshiriki katika mdahalo huo badala yake mdahalo Mdahalo uwe bina ya wenyeviti wa vyama vya siasa. Hayo yalisemwa na Mwenyekiti mwenza wa vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), James Mbatia September 18, 2015 aliomba kufanyika mdahalo kati ya vyama vinavyounda umoja huo na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Mbatia alitoa ombi hilo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo aliwasihi viongozi wa CCM kuwachagua wasemaji wao ili waweze kujumuika pamoja katika mdahalo kwa lengo la kunadi sera na ilani za vyama vyao. “Tunawataka CCM wachague msemaji wao, na kwa kuwa Ukawa haitambuliki kama chama cha siasa, vyama vyote vya upinzani vitaweka wasemaje wao, ili tuache porojo na maneno maneno,” alisema Mbatia na kuongeza kuwa vyama ndivyo vinavyowakilisha mfumo wa serikali inayotarajiwa na sio mtu mmoja”. Hata hivyo ombi hilo limepigwa vikali na wadau mbalimbali wa demokrasia na utawala borana wanaharakati, pia kma ilivyotarajiwa na wengi chama cha mapinduzi kwa kupitia kwa mjumbe wo wa halmshauri kuu ya chama hicho taifa na mjumbe wa kamati ya kampeni January Makamba amabaye bila Kumung’unya maneno amesema kuwa wanataka mdahalo wa wagombea urais na si wenyeviti wa vyama. Makamba aliongeza kuwa mgombea wwao kupitia Ccm. Dr. Magufuli amekubali kushiriki katika mdahalo huo bila kipingamizi chochote na muda wowote utakapopangwa mdahalo huo. Kwa mujibu Makamba wa chama chake wanafurahishwa na utamaduni wa midahalo ambao unaanza kujitokeza katika chaguzi zetu. Na ccm inaamini kwamba midahalo ya Wagombea Urais nisehemu muhimu ya kuwashirikisha wapiga kura katika mchakato wa uchaguzi na kuwasaidia waamue nani wamchague kwa misingi ya hoja na sera na sio kwa ushabiki, kwa mihemko, na kwa propaganda. Mdahalo unatoa fursa ya wagombea kuulizwa maswali ya moja kwa moja na kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu sera na ahadi zao, fursa ambayo hawaipati kwenye mikutano ya hadhara kampeni. CCM kupitia kwa mjumbe wa huyo Halmashauri kuu taifa ya chama hicho na mjumbe wa kamati ya kampeni wapinga hoja ya iliyotolewa na wenzao wa Ukawa kupitia kwa Jems Mbatia, kwa kusema hawakubaliani na kauli ya UKAWA kwamba mdahalo usiwe baina ya wagombea bali uwe baina ya Wenyeviti wa Vyama. Makamba alisema kuwa hoja ya kutaka midahalo washiriki wenyeviti badala ya wagombea wa urais ni kichekesho. Haijawahi kutokea popote duniani kwenye utamaduni wa midahalo, kwamba wagombea wasishiriki bali watu wengine ndio wafanye midahalo kwa niaba yao. “Sasa tunawahakikishia tuko tayari kufanya nao midahalo hiyo, isipokuwa tunataka midahalo hii ifanyike baina ya wagombea Urais. Sisi mgombea wetu Dk Magufuli yuko tayari hata kesho mkitaka,” Binafsi napinga na hoja ya Ukawa na kuungana na ndugu January Makamba kuwa mdahalo huu unapaswa kuwa baina ya wagombea wa nafasi za urais. Wao ndio wanaoomba dhamana na ndio wanaopaswa kujibu maswali na kufafanua kuhusu ahadi zao. Haiingii akilini kwa Ukawa kumkimbiza mgombea waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa kwa sababu zozote zile katika kushiriki katika mdahalo ambao utaleta afya na tija katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu amabao unakuwa ni uchaguzi wa kihistoria tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi nchini mwaka 1992. Kuleta sababu zisizo na kichwa wala miguu kwa Ukawa kutaishushia kuushusha hadhi umoja huo na kuwafanya wananchi wawe na mashaka nao na kujiuliza maswali mengi yasiyo na majibu pamoja na kuleta mkanganyiko kwa jamii kuweka dhana kuwa kuna ukweli unafichwa amabao wanauogopa unaweza kuleta sintofahamu katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu kwa umo0ja huo . Kutakuwa na maswali kwanini ukawa wamkimbize mgombea wao katika mdahalo wakati duniani kote ni kawaida ya midahalo, anayenufaika ni yule wa kutoka kambi ya upinzani. Yeye ndiye atakayekuwa na fursa ya kuponda sera mbaya za serikali iliyo madarakani, ambaye hatakuwa na woga wa kutoa siri yoyote ya serikali na hana la kupoteza. Lakini tunashangazwa na upinzani kuogopa kupeleka mgombea katika mdahalo wakati wao hawana cha kupoteza tofauti na chama tawala. Kama atashindwa uchaguzi, ataendelea kuwa mtu yuleyule lakini kwa aliye madarakani, atapoteza kila kitu kama atshindwa kwenye uchaguzi. Mbatia na Ukawa wanapswa kufahamu kwamb Kwenye uchaguzi duniani kote midahalo hufanyika kwa ajili ya wagombea na sio watu wengine. Sababu ya kufanya hivi ni kuwawezesha wananchi kuwasikia na kuwauliza maswali wagombea wakati wanaelezea sera ya vyama vyao na jinsi gani walivyojipanga kutekeleza sera hizo. Ni kwa njia hii pia wananchi wataweza kuwaelewa zaidi na kuwatathimini wagombea hawa na hivyo kuwapa fursa ya kufikia uamuzi wa busara wa nani kumpa kura zao wakati wa uchaguzi. Kwa mantiki hii mdahalo unaotakiwa kufanyika ni wa wagombea pekee wala wasikwepe katika hili ikiwa wanaamini kuwa wamefanya uchaguzi sahihi juu ya mgombea wao na kuja kukuuza kwa wananchi. Watanzania wenye vyama na wasio na vyama wataka kuchagua kiongozi atakaye iongoza nchi na siyo atakayeongoza chama au vyama. Viongozi wa vyama tayari wapo na kila chama kina utaratibu wake wakumchagua kiongozi wao pale muda utakapo fika. Hivyo sisi wananchi tunataka mdahalo wa hawa viongozi wanaogombea urais na ambao kila mmoja wao anasema ana uwezo wa kutuongoza. Hivyo basi viongozi wa Ukawa kwa ujumla wao wakubali kushiriki kwenye mdahalo huu ili watusaidie katika kufikia maamuzi yetu ya nani atafaa kuchukua jukumu hili kubwa na zito la kuiongoza nchi. Kukacha kushiriki katika mdahalo kunaweza kukaleteleza wananchi, ambao ndio wapiga kura, kumfikiria mgombea husika vingine. Tunataka mdahalo wa kina kuhusu masuala kitaifa tujue jinsi gani tutakaowapa dhamana wataendesha nchi yetu , jinsi gani ilani zao zitatekelezwa, utamaduni huu ujengeke kwenye chaguzi zetu , tena sio tu kati ya wagombea urais wa vyama vya siasa , bali pia ndani ya vyama wakati wa mchujo , kama wenzetu wenye demokrasia imara wanavyofanya , wataokaoshiriki ndio tutawapima na ndio tukaowachagua , wasioshiriki midahalo inaashiria hawajiamini na sera zao hazitekelezeki, isokuwa wana nia za kuwalaghai na watanzania Tunanaamini kwamba ili mdahalo huu uwe na tija, wagombea Urais wote, hasa wa vyama vikuu, wawepo na washiriki. Mdahalo hautakuwa na maana kama mgombea mmojawapo wa vyama vikuu atatengeneza kisingizio ili asishiriki
 
Back
Top Bottom