Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais

Hivi kwa tuhuma alizo nazo Makonda, Ushahidi unapaswa kuweje kwa mfano???
Ni nini kinachoweza kusemwa kikubalike kuwa ushahidi wa kweli au wa uongo?
Ni nani anayeweza kusema ili ikubalike kuwa ni kweli?

Paschal, Huwezi kuwa na vipimo tofauti vya kupimia uadilifu au Kweli ............... Kama unaamini kwamba Gwajima anapaswa a behave kama yuko mbinguni sijaweza kujua ni kwa kipimo gani?

Paschal, kipimo ukweli unachompimia Gwajima ndicho kipimo hicho hicho ambacho Makonda anapaswa kupimwa nacho. Ukweli hauna tafsiri mbili na hautegemei mazingira .................................... Unapaswa kujua!
 
Wanabodi,
Manabii wa Uongo na Tutawatambuaje?.
Kwa sisi waumini wa dini ya Kikristo, tunayemwamini Bwana wetu Yesu Kristo, kabla hajapaa mbinguni, alituhusia kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".

Mchungaji Dr. Josephat Gwajima ni Nabii wa Kweli au Nabii wa Uongo?.
Hii ni thread ya swali kumhusu Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo wa Uzima, Mchungaji, Dr. Josephat Gwajima, Jee ni Mtumishi wa Mungu wa Kweli?!, ni Nabii wa kweli au ndio wale manabii wa uongo aliowazungumza Bwana wetu Yesu Kristo?.

Akiwa katika mimbari, madhabahuni, mbele ya Mungu na wana kondoo wake, badala ya kuihubiri Injili na neno la Mungu lenye uzima na lenye kujenga upendo, amani na mshikamano miongoni mwa jamii, yeye anahubiri siasa kwenye nyumba ya ibada, tena mahubiri juu ya chuki dhidi ya binadamu mwingine hadi kumuita "kiumbe".

Japo ni kweli Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda alimdhalilisha Mchungaji Gwajima kwa kumtaja kujihusisha na madawa ya kulevya, jee namna ambayo Mchungaji Gwajima, anavyomzungumzia Mkuu wetu wa Mkoa, ndivyo Bwana Yesu alivyofundisha namna ya kuwashughulikia wale walio tukosea?. Yesu alifundisha mtu akikupiga kibao shavu la kushoto mgeuzie na la kuume. Adui mpende. Samehe saba mara sabini. Vipi kuhusu Baba Mchungaji Gwajima kumuishi Bwana Yesu kwa maneno na matendo? .

Jee Maneno na Matendo ya Mchungaji Gwajima ni Kama Yesu, ni ya KiMungu?.
Swali ni jee huu ndio utendaji wa watu wa Mungu, kuwatakia wenzao mabaya?, kuwazushia uongo mchana kweupe tena madhabahuni kwenye mimbari ya Mungu?!. Yesu alitufundisha, "tumpe Kaisari yaliyo ya Kaisari, na tumpe Mungu yaliyo ya KiMungu, kwanini Mchungaji Gwajima, analeta ya Kaisari mezani kwa Bwana?!. Jee huyu Mchungaji Gwajima, ni mchungaji wa Mungu au ni wa mungu?. Mchungaji Gwajima kama mtu wa Mungu wa kweli, anaweza kweli kusema uwongo kama ule madhabahuni kwa Bwana?!. Jee huyu ni mchungaji wa kweli anayemtumikia Mungu wa kweli, au ndio wale wachungaji aliyewasema Bwana wetu Yesu Kristo kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Bwana Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".
Jee kwa matendo kama haya, kuna kitu chochote cha kutambua?.
Mchungaji Gwajima ni Nabii wa Mungu, au nabii wa mungu?.

Jumatatu Njema.
Paskali

For your perusalo_O:confused:
upload_2017-3-1_18-7-21-png.475777
 
Wanabodi,
Manabii wa Uongo na Tutawatambuaje?.
Kwa sisi waumini wa dini ya Kikristo, tunayemwamini Bwana wetu Yesu Kristo, kabla hajapaa mbinguni, alituhusia kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".

Mchungaji Dr. Josephat Gwajima ni Nabii wa Kweli au Nabii wa Uongo?.
Hii ni thread ya swali kumhusu Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo wa Uzima, Mchungaji, Dr. Josephat Gwajima, Jee ni Mtumishi wa Mungu wa Kweli?!, ni Nabii wa kweli au ndio wale manabii wa uongo aliowazungumza Bwana wetu Yesu Kristo?.

Akiwa katika mimbari, madhabahuni, mbele ya Mungu na wana kondoo wake, badala ya kuihubiri Injili na neno la Mungu lenye uzima na lenye kujenga upendo, amani na mshikamano miongoni mwa jamii, yeye anahubiri siasa kwenye nyumba ya ibada, tena mahubiri juu ya chuki dhidi ya binadamu mwingine hadi kumuita "huyu kiumbe"!.

Japo ni kweli Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda alimdhalilisha Mchungaji Gwajima kwa kumtaja kujihusisha na madawa ya kulevya, jee namna ambayo Mchungaji Gwajima, anavyomzungumzia Mkuu wetu wa Mkoa, ndivyo Bwana Yesu alivyofundisha namna ya kuwashughulikia wale walio tukosea?. Yesu alifundisha mtu akikupiga kibao shavu la kushoto mgeuzie na la kuume. Adui mpende. Samehe saba mara sabini. Vipi kuhusu Baba Mchungaji Gwajima kumuishi Bwana Yesu kwa maneno na matendo? .

Jee Maneno na Matendo ya Mchungaji Gwajima ni Kama Yesu, ni ya KiMungu?.
Swali ni jee huu ndio utendaji wa watu wa Mungu, kuwatakia wenzao mabaya?, kuwazushia uongo mchana kweupe tena madhabahuni kwenye mimbari ya Mungu?!. Yesu alitufundisha, "tumpe Kaisari yaliyo ya Kaisari, na tumpe Mungu yaliyo ya KiMungu, kwanini Mchungaji Gwajima, analeta ya Kaisari mezani kwa Bwana?!. Jee huyu Mchungaji Gwajima, ni mchungaji wa Mungu au ni wa mungu?. Mchungaji Gwajima kama mtu wa Mungu wa kweli, anaweza kweli kusema uwongo kama ule madhabahuni kwa Bwana?!. Jee huyu ni mchungaji wa kweli anayemtumikia Mungu wa kweli, au ndio wale wachungaji aliyewasema Bwana wetu Yesu Kristo kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Bwana Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".
Jee kwa matendo kama haya, kuna kitu chochote cha kutambua?.
Mchungaji Gwajima ni Nabii wa Mungu, au nabii wa mungu?.
Japo nimewahi kushiriki Ibada kwa Mchungaji Gwajima, naomba mimi nisiseme kitu bali msikilize mmoja wa waumini wake ambaye pia ni mwanachama mwenzetu hapa jf.

Kwa ushuhuda huu mtaona tuhuma unga kwa Mchungaji hazikutolewa na Makonda kwa wivu wa helicopter au vita vya Jimbo bali Makonda alipewa majina na akayaanika.
Paskali
Jumatatu Njema.
Paskali
Ndugu Mayalla.
anayesamehewa ni yule anayeomba msamaha. ( soma Luka 18:4.) Kama ni kweli Bw . Makonda amemkosea Mch . Gwajima, ni vizuri amwombe msamaha ndivyo Maandiko yanavyosema. MTU akimkosea mwenzie, amwonye, akitubu asamehewe. Kabla ya Mch. Kuombwa msamaha, amwachilie Bw. Makonda.(Mch. atengeneze mazingira ya kuwa tayari kusamehe. Wapendwa, hata MUNGU hawezi kutusamehe mpaka pale tutakapotubu makosa yetu. Ndio maana Mungu anasema tubuni makosa yenu. Ndiyo sababu kubwa leo wanaadamu tunakufa kwa sababu Adamu na Hawa, hawakutubu Bali walijitetea kwa kutoa lawama. Kama wangaliomba msamaha MUNGU angewasamehe.
 
Pascal Mayala haeleweki, ila nae atuambie alikopitia elimu yake mpaka anapata digrii. Make mimi Mayala nimeanza kumsikia anaandika habari wakati hana digrii.......sasa atuambie alikuwa mwandishi vipi wakati hana digrii......na ameipataje digrii yake hapo baadae. Hizi elimu za kuunga zina shida sana.
 
Gwajima kikwetu ni kilichozimika. Katika kilipu yake kuhusu "Kiumbe yule", HAKUTAJA JINA. Hapo kisheria ana kosa? Kisha kusema kuwa "Mtumishi wa Ni zaidi ya Raisi" pia hakutaja ni Raisi (gani au wa Nini). Hakutaja wa TFF, Wa DARUSO, wa chochote. Sijui pia hapo kama atakuwa layabo..
 
Salaam humu, nina hasira sana na Gwajima...

Laiti, mm ningekuwa RC Makonda, saa hizi Gwajima angekuwa maabusu and behind unknown bars..

Serikali, kamateni huyu mchungaji feki, mmemlea sana, kaota mapembe, akijua yuko juu ya state.. Iweje Gwajima, anamchafua Mkuu wa Mkoa, Makonda kwa kiwango hiki, na asikamatwe? With immediate action, kamateni mhuni mchungaji feki, iwe funzo la milele..

HATUWEZI kuwa na mchungaji mhuni mhuni kuchafua viongozi wa serikali kutumia kanisa lake . I wish ningekuwa RC Makonda, sitanii, Gwajima ungejuta, kamata huyu mhuni haraka.. Aaaaarrghh

Haiwezekaniki mchungaji feki huyo kumchafua RC kiasi hiki, no way, no how, not acceptable, lazima lazima heshima iwepo kwa viongozi wa serikali ikibidi kwa lazima, Who is Gwajima? Mandate ya kuchafua kiongozi wa serikali anapata wapi? I was offline for 2 weeks, namuona Gwajima anaachiwa kucheza hovyo, piga ndani huyu mhuni mkubwa, ww Gwajima ww, jua wazi hauko juu ya serikali, na serikali inakujua ww kuliko unavyojijua, acha ujinga mara moja.. Aaaarrghh

Huyu Gwajima anasema yeye ni zaidi ya Rais? Eeeehh.. Ooohh, noo..!!
 
Sasa nani kamchafua mwenzie kati ya makonda na ngwajima hivi wewe unadhani tuhuma za kuuza madawa ya kulevya ni ndogo?

Unajua popularity ya ngwajima duniani ?unafananisha na ya makonda ? ngwajima asibitishe tuhuma za makonda kufoji vyeti na makonda asibitishe tuhuma za ngwajima kuuza au kutumia madawa ya kulevya.

msimtetee makonda kwa kigezo cha ukuu wa mkoa mwacheni yeye mwenyewe atoke aweke vyeti hadharani kwanza yeye sio wa kwanza kutuhumia iweje iwe ngumu kwake wenzie wote waweze
 
Mlifeli pale mlipomuita ngwajima central halafu mkawa hamna kidhibiti za kumuweka ndani?

Hapo zimekutoka fa fa fa fa fa wala hujaweka sababu kwanini akamatwe...!

Makonda awekwe ndani naye kwa kutumia jina la mtu kwenye vyeti...

Ngwajima ana vyeti yeye mwenzenu
 
Tatzo Gwajima nae anajisahau sana....Up to this moment ameishajiona kakaa juu ya IKULU....ni suala la MUDA.....maana this guy si MTUMISHI wa MUNGU KABSA......ana mengi machafu TU sema wakati mwingne busara ni jambo la MSINGI sana..na ndicho tunachikiona kwa sasa kupitia hii SERIKALI juu ya GWAJIMA
 
Freedom of press. Hajamchafua Bali kaongea ukweli. Kamata halafu uoneshwe nyaraka uone aibu na umlipe fidia.
Think twice
 
Back
Top Bottom