mchumba ni tofauti na mpenzi?

Mwl Ngasa

Member
Aug 9, 2012
32
7
mara nyingi saana napata wapenzi ambao napenda kuwafanya wachumba lakin cha kushangaza ni kwamba hawajiweki tayari kwa ajili ya ndoa je hii nayo nashindwa kujua mchumba anakuaje? kama haanzii kupendwa kama mpenzi?
 
Anatakiwa ajiwekeje tayari kindoa?

Nyie ndio mnapenda fake people, mtu akiwa herself mnaona hafai; ngoja wawahadae ili ukimuingiza ndani ndio uone jinsi alivyo!

By the way wewe unajiweka kibaba wa familia?
 
Mchumba na mpenzi ni vitu viwil tofouti, mchumba ni yule umeisha enda mchumbia kwao na mpenzi ni yule mnaye jidanganya tu kama mnapendana.
 
mara nyingi saana napata wapenzi ambao napenda kuwafanya wachumba lakin cha kushangaza ni kwamba hawajiweki tayari kwa ajili ya ndoa je hii nayo nashindwa kujua mchumba anakuaje? kama haanzii kupendwa kama mpenzi?

Mwl Ngasa kunatofauti kubwa sana kati ya mchumba na mpenzi. Mchumba ni yule ambaye umeamua kwa dhati ya moyo kuja kuishi naye kama mke na utaratibu wote husika umefuatwa, kwa kifupi mchumba ni mke mtarajiwa! Mpenzi ni mtu mnayepeana kampani tu, anaweza baadaye akaja kuwa mchumba au mkaachana na kila mtu akawa kivyake.

Tatizo ulilonalo wewe si namna gani wachumba wako wanajiweka kwa ajili ya ndoa, ila ni namna unavyowaandaa kwa ajili ya ndoa. Inawezekana matendo na tabia zako zinadhihirisha wazi kwamba haujafikia wakati wa kuoa na wakati huo huo wewe unatamani na kuwatamkia hao wachumba habari za ndoa, Ni kama unawachanganya na ndiyo maana wako reluctant kukubaliana na wazi lako!

Nafikiri jaribu kuangalia mapungufu yako kwenye tabia, mwenendo, mazungumzo, nk kupitia kwa rafiki zako wa karibu na ubadilike na kisha uone kama hao wachumba hawatajileta wenyewe kwa ajili ya ndoa, kwa taarifa yako walio wengi wanapenda ndoa!
 
Hapa huwa kuna kazi kweli kuna watu wanapendwa danganywa kuliko ambiwa ukweli
 
Hapa huwa kuna kazi kweli kuna watu wanapendwa danganywa kuliko ambiwa ukweli
Na hili ni tatizo la wanaume wengi wanapenda mno wasichana wanaoigiza na baada ya ndoa wanakimbiliia jamiiforums kulalama yani mtu ukiwa muwazi wanakuonna namna gani tusiojua kuigiza kazi ipo
 
mara nyingi saana napata wapenzi ambao napenda kuwafanya wachumba lakin cha kushangaza ni kwamba hawajiweki tayari kwa ajili ya ndoa je hii nayo nashindwa kujua mchumba anakuaje? kama haanzii kupendwa kama mpenzi?

Shkamoo mwalimu (afu kama we sio Mwl Ngasa wa ........... return my greetings)
 
Mchumba anaheshimiwa zaidi maana pande zote mbili wanamtambua.Mpenzi ni kama kudanganyana tu mda mwingine mnakutana gest biashara inakwisha.
 
Mchumba, Mke, wote ni wapenzi. ungeuliza tofauti kati ya mchumba na hawara ingetulia zaidi. lkn mpenzi ni title., aweza kuwa mke/mume/ mchumba. Hao unaoanza nao huwa ni mahawara tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom