mchezaji wa yanga ajenga hotel ya kitalii

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
5,139
1,139
Nonda shabani "Papii" si jina geni kwa wapenzi wa soka wa bongo,huyu ni mchezaji wa zamani wa yanga ya dar es salaam ambae ameonyesha mfano wa kuigwa kwa wachezaji wetu wa bongo kutokana na mafanikio yake ya kisoka na maisha kiujumla.Nonda amezindua hotel yake ya kitalii hivi karibuni hapa kinshasa aliyoipa jina "VILLA FATUMA" uzinduzi uliohudhuriwa na watu wengi maarufu congo akiwemo mwanamuziki wa zamani wa bendi ya wenge musica ADOLPHE DOMINGUEZ.Gonga hapo chini utizame video ya uzinduzi wa hoteli hiyo ya kisasa na nzuri kuliko club za simba na yanga!

Last edited by a moderator:
Mchezaji wa Yanga? Hivi kumbe anaichezea Yanga? Mi najua alipitia Yanga kabla hajaenda alipostahili. Mchezaji wa Yanga akifanikiwa sana labda anunue Starlet na kakibanda ka rooms tatu, choo passport size.

Chezeya soka la bongo?
 
YANGA ndio ilimtoa from zero to hero,nani angemjua bila yanga iliyomuokota mwananyamala?
 
Safi sana sana,ingawa kwa level yake inatakiwa iwe kawaida sana!!kwa level ya kiafrika na soka la afrika hapo ni sana sana!
 
Mimi nilidhani Bahanuzi au Twite au Yondan, kumbe Nonda, kweli kaonyesha njia inabidi Kavumbagu naye atoroke kwenda South maana Nonda naye alitoka Atletico ya Burundi akaja Yanga ila akatoroka kwenda South ndo alikoanza kufanikiwa lakini sio pale kwenye majaruba.
 
Nonda shabani "Papii" si jina geni kwa wapenzi wa soka wa bongo,huyu ni mchezaji wa zamani wa yanga ya dar es salaam ambae ameonyesha mfano wa kuigwa kwa wachezaji wetu wa bongo kutokana na mafanikio yake ya kisoka na maisha kiujumla.Nonda amezindua hotel yake ya kitalii hivi karibuni hapa kinshasa aliyoipa jina "VILLA FATUMA" uzinduzi uliohudhuriwa na watu wengi maarufu congo akiwemo mwanamuziki wa zamani wa bendi ya wenge musica ADOLPHE DOMINGUEZ.Gonga hapo chini utizame video ya uzinduzi wa hoteli hiyo ya kisasa na nzuri kuliko club za simba na yanga!

Mbona naona kama bendera ya tanzania?
 
Last edited by a moderator:
YANGA ndio ilimtoa from zero to hero,nani angemjua bila yanga iliyomuokota mwananyamala?

Halafu ikamtupa wapi? ingekuwa raha zaidi kama mafanikio hayo yengepatikana kwa m-bongo. Akiwa wa kigeni inakuwa haina mashiko sana, si unaona hata hotel yenyewe kajenga Kinshasa. Kwa nini asijengejenga Mwananyamala 'alikookwota'?
 
YANGA ndio ilimtoa from zero to hero,nani angemjua bila yanga iliyomuokota mwananyamala?

Ingekuwa bora kama angejenga hiyo hoteli Mwananyamala au angekarabati jengo la klabu jangwani ili kuepusha wachezaji kulala mzungu foo.

Mchezaji wa Yanga ya Dsm anajenga Kinshasa? Ova My Dedi Bode....
 
Hayo pekee ndiyo mafanikio ambayo watani zetu mnapaswa kujivunia lakini soka hakuna kajipangeni upya, lakini hapo si alifanya kupita tu hata uraia ni wa Kongo vipi kama angekuwa mbongo aliyelelewa na kuuzwa na Yanga kama ambavyo Simba wamefanya kwa akina Samata Magoli na wengine wengi wanaoitikisa Dunia mngefanyaje?

Another version of ulimbukeni's revealed..
 
Halafu ikamtupa wapi? ingekuwa raha zaidi kama mafanikio hayo yengepatikana kwa m-bongo. Akiwa wa kigeni inakuwa haina mashiko sana, si unaona hata hotel yenyewe kajenga Kinshasa. Kwa nini asijengejenga Mwananyamala 'alikookwota'?
Labda Kongo Kinshasa ya Kariakoo. Yanga mko juu kwa kufurahia harufu ya pilau ya jirani.
 
hivi yanga ilimuuza bil ngapi kwenda sauzi na baadae ulaya...
Mkuu Crashwise mbona maswali yako magumu sana? Ona sasa wamekimbia au ndiyo mafuta yameisha, ngoja waende kibandani wakirudi watatujibu. Ngoja wajibu halafu nitarejea na swali la nyongeza.
 
Hayo pekee ndiyo mafanikio ambayo watani zetu mnapaswa kujivunia lakini soka hakuna kajipangeni upya, lakini hapo si alifanya kupita tu hata uraia ni wa Kongo vipi kama angekuwa mbongo aliyelelewa na kuuzwa na Yanga kama ambavyo Simba wamefanya kwa akina Samata Magoli, Ulimwengu Tom na wengine wengi wanaoitikisa Dunia mngefanyaje?

Another version of ulimbukeni's revealed..

Mi ndo maana nasemaga siku zote,mashabiki wa Simba hata mpira wenyewe hawaujui,huyu naye amekariri kila Mtanzania anayecheza TP Mazembe katoka Simba,poor grafani11 .....embu pata msaada kwa Mwana Msimbazi mwenzio Masuke kuhusiana na wachezaji mliowauzia Mazembe,achana na huyo Bwana Mdogo Ulimwengu aliyekuwa atue Yanga akazuiwa na safari yake ya kwenda kufanya majaribio Ulaya kabla ya kurudi na kuangukia TP Mazembe
 
Last edited by a moderator:
vipi okwi hata india nako wamemkataa, kweli simba mnazalisha vipaji
Baada ya kuwatenda vibaya kwa Five O'clock na kuwastaafishia Fuso lenu kwa aibu, kila siku Okwi yupo vichwani mwenu, kwa taarifa yenu hatumuuzi kwa vihela uchwara kama nyinyi mpo tayari kutoa wachezaji wenu hata bure tena hata kwa kuwatoroka kwenda South Afrika halafu mnajisifu mmechina.
Kama angekuwa wa kwenu angekarabati hata lile bwawa la Kambare pale kaunda. El-nino inakuja tutaokota mpaka Sangara pale.
 
Halafu msimu huu kwa Okwi ni kama misimu yake ile mi'3 iliyotangulia,yaani hawezi ku'shine...mtaniambia
 
Nonda shaban papii hawezi kuisahau yanga maishani mwake!yanga umojawa mataifa endeleeni kulea vipaji!!
 
Halafu msimu huu kwa Okwi ni kama misimu yake ile mi'3 iliyotangulia,yaani hawezi ku'shine...mtaniambia
Fisi anayesubiri mkono uanguke wewe, utasubiri sana kama wafuasi wa kibwetere na kiama hakiwadii. Watu wanapeta, tukitoa sare tumefungwa hatujazoea na hatufurahii kama nyinyi malimbukeni wauza sura magazetini hata Tom Saintfet alikiri hilo.
 
Umeandaa habari nzuri ila umeshindwa kujieleza Nonda si mchezaji wa Yanga ila aliwahi kuichezea Yanga acha upenzi wa kijinga huna jipya
 
Back
Top Bottom