mchezaji huyu wa taifa stars afundishwe adabu;akome kutuzalilisha watanzania

Ndugu yangu hebu acha kumuonea mzanzibari mwenzangu...

hilo sekeseke ni wengi tulilishuhudia, wengine walikuwepo uwanjani na wengine kupitia runinga.

kwanza hayo maneno ya kipumbavu ni yepi? unaweza kuya-quote hayo maneno?

Mie nilikuwa nimekaa upande wa orange straight kulia kwa jukwaa kuu na hilo tukio nililishuhudia.

Abdulhalim hakumfanyia chochote kibaya Aruna Dindane, isipokuwa Dindane ndiye alionyesha dharau kwa abdulhalim. Na kama unakumbuka vizuri abdulhalim ndiye alimfuata Dindane kumpa mkono na kuyamaliza kutokana na purukushani iliyokuwa imetokea hapo kabla. Sasa unadai afundishwe adabu ipi?

baada ya dindane kuonyesha kumpandishia na kumsukuma ndipo jamaa nae akawa anakomaa nae, isingekuwa rahisi katika hali ile wenyewe wayamalize bila mtu mwingine kuingilia kati na ndio sabau ya refa kuingilia kati kuwatenganisha, so usimlaumu bure kijana wa watu hakufanya jambo lolote baya la kufaa kufundishwa adabu, labda utafute jambo lingine.

au unataka kumfagilia maximo kiujanja ujanja?

Uko sahihi Mwita nilikuwa na mawazo kama ya kwako nilichoelewa mimi Abdulhalim alimfuata jamaa wamalizane kwa kuwa ndio mpira ulivyo. Lakini jamaa ndio akaanza kumaindi.

Inawezekana jana ana mapungufu kidogo kwenye nidhamu na anatakiwa ajirekebishe ila binafsi nimemkubali ana kiwango cha holding midfielder!!
 
Ndugu yangu hebu acha kumuonea mzanzibari mwenzangu...

hilo sekeseke ni wengi tulilishuhudia, wengine walikuwepo uwanjani na wengine kupitia runinga.

kwanza hayo maneno ya kipumbavu ni yepi? unaweza kuya-quote hayo maneno?

Mie nilikuwa nimekaa upande wa orange straight kulia kwa jukwaa kuu na hilo tukio nililishuhudia.

Abdulhalim hakumfanyia chochote kibaya Aruna Dindane, isipokuwa Dindane ndiye alionyesha dharau kwa abdulhalim. Na kama unakumbuka vizuri abdulhalim ndiye alimfuata Dindane kumpa mkono na kuyamaliza kutokana na purukushani iliyokuwa imetokea hapo kabla. Sasa unadai afundishwe adabu ipi?

baada ya dindane kuonyesha kumpandishia na kumsukuma ndipo jamaa nae akawa anakomaa nae, isingekuwa rahisi katika hali ile wenyewe wayamalize bila mtu mwingine kuingilia kati na ndio sabau ya refa kuingilia kati kuwatenganisha, so usimlaumu bure kijana wa watu hakufanya jambo lolote baya la kufaa kufundishwa adabu, labda utafute jambo lingine.

au unataka kumfagilia maximo kiujanja ujanja?

Ah bwana weh, si unajua wabongo na ile 70% ya kufuata upepo?
 
Pdidy,

Yule jamaa alinikera hata mimi binafsi, ukiacha liletukio baada ya mpira kuisha, wakati wa mchezo ule alikuwa na confrontation za kipumbavu sana na wale jamaa wa IC...hasa huyo jamaa anaitwa Dindane.....! sijui alikuwa anataka kuonyesha nini....but kwa harakaharaka anaonekana jamaa wa ndumu sana, na anataka kuonyesha ubabe kwamba na yeye hawavumi lakini wamo....hopeful!...angalia hata alivyojieleza wakati anahojiwa na mtangazaji.......the boy is totally out of his mind & undisciplined!

Mze wa Docebit vipi tena? ulianalia mechi wapi? au projector ilikuwa inaonyesha lateral images???:confused:
 
Kiukweli yule dogo soka inaijua may be tatizo kubwa nililoona mimi ni kale katabia ka kujiona matawi ya juu sana. wakati anahojiwa na mtangazaji ni matamashi yake ni wazi ya kuonyesha ubabe fulani..tofauti kabisa alivyo-behavu Mrisho Ngasa he was polite na aliongea jambo la msingi kuwa mechi ilikuwa ngumu na matokeo ndio yalivyokuwa. Nadhani wachezaji wetu wanatakiwa kupata wataalam wa ushauri nasaha kuhusu mambo mbali mbali na jinsi ya ku-behave once wanapokuwa katika level za juu za uchezaji wao.
 
michezaji mihuni kazi kuvuta bange tu hakuna lolote pale ..
 
Basi miye kweli mshamba;
Kwa kweli nilivyouangalia ule mpira, aliyenikera ni yule mkodivaa ambaye baada ya kupewa mkono (baada ya foul) alimsukuma abdulhalim... Baada ya mpira kwisha, abdulhalim alikwenda kumpa mkono tena mkodivaa na akasukumwa; nikachukia sana na sikuwa peke yangu...

kuhusu yale mahojiano, i thought the guy was fired up na majibu ya kusema kwani wao waweze wana nini na sisi tushindwe tuna nini ni inspirational kuliko majisifu ya kijinga!!

KWakweli, mimi binafsi nampongeza abdulhalim kwa kucheza vizuri sana sehemu ya kiungo na kwa kuwa fired up all the game, tukumbuke kwamba kuna wachezaji bila ule munkari mpira hauendi, akina Gazza, Gatusso, Gerrad, Roy Keane etc. Siwezi kumlinganisha abdulhalim na Nyosso au Mrwanda...

Kama mliona tofauti basi ni mtazamo na cha maana ni kiumsaidia abdulhalim kwani ana potentials zote kama walizokuwa nazo akina Gaga kwenye soka la bongo afike mbali zaidi, ana height, physique, pace, control, stamina, pace nk

Lets go positive japo kwa dakika!!

Its true, abdulhalim hana kosa, alichofanya alienda kumpa hi baada ya game yule mjinga akamsukuma na kumpa maneno ya ukali sasa mlitegemea dogo afanye nini?

Mjue hata hawa Professionals baadhi yao pia ni washamba, mi nilifuatilia dogo hana kosa lolote.
 
Ingawa sijaona tukio wala mechi yenyewe, kijana anayo haki ya ku-behave vile anavyoona inafaa as long as anajua consequences. Otherwise sioni cha kujadili hapa.
 
Ingawa sijaona tukio wala mechi yenyewe, kijana anayo haki ya ku-behave vile anavyoona inafaa as long as anajua consequences. Otherwise sioni cha kujadili hapa.

Ni kweli kama hukuona, then huna cha kujadili... walioona wahca wajadili!!
 
Kila ktk maisha yako unachokijadili umekiona??

Hapa tunaongelea Abdulhalim mchezaji wa taifa stars... turudi kwenye mada

  • alicheza vizuri sana
  • ana umri swafi wa kujiendeleza
  • anahitaji msaada kidogo kama mtoa mada alivyosema ingawa mimi sikuona utovu wa nidhamu kama ambao dindane alionyesha siku ya mechi
 
Dodo ni noma anapiga mpira wa europe hatakiwi kuwepo hapa, nafikiri huyo ni mchezaji atakae tutoa kwa kucheza ligi/timu kubwa uropa, kikubwa TFF wanapotafuta kocha mpya watafute na mtaalam wa saikolojia. tusiwaache wachezaji wajirekebishe wenyewe, Pia haisaidii sisi kujifanya hatuoni matatizo ya nidhamu yaliyopo YAPO tena ni makubwa sana, Tukumbushane kidogo tu kadi tulizo pata CHALENJI, kadi ya Boban iliyo wagharimu Simba na ile ya juzi ya Ngasa Hawa(Boban na Ngasa) hawakutakiwa "kuongea" na mshika kibendela kwa namna walivyofanya, Kama juzi Ngasa angekua na kadi ya njano mapema kwa upuuzi wake ingekuwa nyekundu. Tunaishia kuraumu waamuzi wa kibongo. Ninaaamini muamuzi yeyote ANAEFUATA sheria (sio waamuzi wengi wa ligi kuu Tz) atatupa kadi nyingi sana.
 
really yule mchezaji aliboa kwani hata baada ya mechi wakati akihojiwa na mtangazaji alikuwa akijibu kwa lugha ya kijeuri na kama alikuwa akiwadharau wa ivory coast wakati alitakiwa kuwarespect kwani vyovyote vile wale wako juu na hawakuwa na mchezo wowote mbaya na kama kuna jambo baya linatokea mwishoni mwa mchezo watu mnapeana mikono na kusameheana
the guy is a fool
nafikiri wachezai wetu wanahitaji sana kufundishwa suala zima la nidhamu kwani waweza kuwa mchezaji mzuri lakini nidhamu ikakukosesha nafasi
 
Pamoja na wachezaji kucheza kwa kiwango cha hali ya juu hakika katika mpira nidhamu ni kitu cha muhimu sana sana;

jana kwa walioangalia mpira kuna kijana ambae leo kwenye gazeti la dar leo kapongezwa na maximo na kweli alicheza vizuri sana ila nafikiri maximo anaitajika kumfundisha awe na adabu uwanjani;mechi ya jana wacha walio uwanjani hadi watoto wadogo wanangalia;anaitwa ABDULHALIM alikuwa amesuka nywele zake,ni mchezaji mzuri sana kama mlivyokuwa mkiona alikuwa akikabana na mchezaji mmoja wa ivory coast,,

Baada ya mechi kuisha ,huyu bwana akamfwata kama anampa fairplay kwa yaliotokoea uwanjani;yule mchezaji akampa mikono miwili kwa heshima gafla jamaa akasukuma akaanza kuongea maneno ya kipumbavu mpaka refa akamfwata baadae maximo akamzuia;

Hawa ndio wachezaji tunatarajia waende kucheza hata sweden loh?shame on u.mpira ukiisha mnamaliza matatizo yenu kama unaitaji kuwa international player,kama uamini abdul subiri yatakayomkuta boban .utakumbuka ninachokwambia kakangu,kama mtakuwa na uchezaji mzuri bila nidhamu mtaishia na patririon ya kuja bongo bila police.....,

Tunaomba viongozi wetu wajue jinsi ya kuwafuundisha awa watu;wazima

Halafu na wewe PDIDY,

Yaani huyu ndio umeona anatudhalilisha, hao viongozi wa soka je? na hao viongozi huko jikoni je?
 
nahisi malaika amekuleta;nilitaaka kumwonglea alivyokuwa anajibu kihuni kama amepata ganja;nahisi atakuwa wale wale;bila ndumu game aipandi;

Pdidy, na mimi nilikuwa nahisi hivyo hivyo kuwa huyu jamaa lazima anatumia!!
 
Tatizo la wabongo kweli wanafuata upepo, aliyeangalia mpira atabaini kuwa Hamoud hakufanya jambo baya. Alimchezea rafu Dindane akakasirika akamuomba msamaha jamaa akakata msamaha mpira ulivyoisha akaenda tena kumuomba msamaha still Dindane akawa hataki
 
Siyo huyo mngazija wa watu tu...
Tumeshaona kina zidane wakichezewa rafu na kisha palepale chini wanalipiza kwa viwiko...
Yeye si wa kwanza.
Kwa mtu yeyote aliyewahi kucheza mpira atakuwa na jibu la kutosha coz ukiwa uwanjani huku damu ikiwa inachemka unaweza kufanya maamuzi ambayo ukija kaa baadae unaweza kujiuliza hv yule aliyefanya upumbavu ule ni mimi kweli?
So msimlaumu dogo.
atafutwe mtaalam wa kuwaweka sawa wachezaji akili zao na tempa zao.
 
Tatizo la wabongo kweli wanafuata upepo, aliyeangalia mpira atabaini kuwa Hamoud hakufanya jambo baya. Alimchezea rafu Dindane akakasirika akamuomba msamaha jamaa akakata msamaha mpira ulivyoisha akaenda tena kumuomba msamaha still Dindane akawa hataki

safi mwanaspoti... ngoja na balantanda naye aje atoe ya kwake... sijui watu wengine waliangalia mpira gani... Inawezekana kabisa baadhi ya Tivii waligeuza images kama kioo

Gangchoma... umesomeka
 
Ndugu yangu hebu acha kumuonea mzanzibari mwenzangu...

hilo sekeseke ni wengi tulilishuhudia, wengine walikuwepo uwanjani na wengine kupitia runinga.

kwanza hayo maneno ya kipumbavu ni yepi? unaweza kuya-quote hayo maneno?

Mie nilikuwa nimekaa upande wa orange straight kulia kwa jukwaa kuu na hilo tukio nililishuhudia.

Abdulhalim hakumfanyia chochote kibaya Aruna Dindane, isipokuwa Dindane ndiye alionyesha dharau kwa abdulhalim. Na kama unakumbuka vizuri abdulhalim ndiye alimfuata Dindane kumpa mkono na kuyamaliza kutokana na purukushani iliyokuwa imetokea hapo kabla. Sasa unadai afundishwe adabu ipi?

baada ya dindane kuonyesha kumpandishia na kumsukuma ndipo jamaa nae akawa anakomaa nae, isingekuwa rahisi katika hali ile wenyewe wayamalize bila mtu mwingine kuingilia kati na ndio sabau ya refa kuingilia kati kuwatenganisha, so usimlaumu bure kijana wa watu hakufanya jambo lolote baya la kufaa kufundishwa adabu, labda utafute jambo lingine.

au unataka kumfagilia maximo kiujanja ujanja?

Unajuwatangu nilipoanza kuisoma hii thread kinishahisi hichi kitu (choyo cha wapi anatoka na nani mtu mwenewe).
Hongera kwa kutupa upande wa pili wa sarafu.
 
Unajuwatangu nilipoanza kuisoma hii thread kinishahisi hichi kitu (choyo cha wapi anatoka na nani mtu mwenewe).
Hongera kwa kutupa upande wa pili wa sarafu.

Mkuu mbona unaleta tena yale mambo yetu na bara na visiwani?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom