Voice of Wisdom
JF-Expert Member
- Oct 4, 2011
- 537
- 240
Heshima zenu wakuu, na poleni na majukumu ya wiki nzima.
Kuna jambo naomba kujuzwa kuhusu kubadili jina. Hii inatokana na ukweli huu "nilipokuwa std 4 tz nilihamishiwa shule huko kenya ambapo nilisoma miaka miwili ( std 4 &5) kisha nikarudi tz, ile shule niliyokuwa mwanzoni nikakuta jina langu kuna mtu analitumia naye yupo std 7. Nikahamia shule ya jirani mwalimu mkuu akanipa jina la mwanafunzi mwingine ambaye alirudia std 6 nikawa nalitumia hadi sasa nipo chuo mwaka wa 2.
Kuna tetesi nimepata kwamba mtu unaweza kubadili jina. Wajuzi naomba mnijuze, je ni hatua gani natakiwa kuzifuata na je inagharimu fedha yeyote?
Nawasilisha.
=====================
==========================
Kuna jambo naomba kujuzwa kuhusu kubadili jina. Hii inatokana na ukweli huu "nilipokuwa std 4 tz nilihamishiwa shule huko kenya ambapo nilisoma miaka miwili ( std 4 &5) kisha nikarudi tz, ile shule niliyokuwa mwanzoni nikakuta jina langu kuna mtu analitumia naye yupo std 7. Nikahamia shule ya jirani mwalimu mkuu akanipa jina la mwanafunzi mwingine ambaye alirudia std 6 nikawa nalitumia hadi sasa nipo chuo mwaka wa 2.
Kuna tetesi nimepata kwamba mtu unaweza kubadili jina. Wajuzi naomba mnijuze, je ni hatua gani natakiwa kuzifuata na je inagharimu fedha yeyote?
Nawasilisha.
=====================
=====================Nawasalimu Wana Jukwaa La Sheria na Wanachama wote wenzangu wa Jamiiforum!!
Zaidi Sana,niwape pole na Shughuli za Kujenga Taifa!!
Naomba nieleze kwa Muhtasari tatizo Langu halafu nisikie kutoka kwenu Kuhusu namna gani Mnaweza Kunishauri maana Peke Yangu nahisi kuishiwa Hekima Kuhusu namna gani niendee Changamoto hii!!
Mm nilimaliza Elimu ya Msingi katika Shule ya Serikali Mwaka 1997 na nikajiunga na Sekondari ya Serikali Mwaka 1998-2001,Mwaka 2002-2004 nikamaliza Kidato cha Sita,Katika hatua zote hizo nilimaliza kwa Matokeo Mazuri tu!!
Tatizo Langu ni Jina,Jina Langu La kwanza ni La Kiislamu na La Pili ni La Kikristo(Yaani Jina La Baba Yangu) Hii imetokana na Mama Yangu Kuwa Muislamu ambaye Kimsingi ndiye aliyenilea na Kunisomesha na Baba Yangu ni Mkristo!!
Sikupenda kuwa na Jina Moja La Imani hii na Lingine La Imani ile na kwa sababu hiyo Mwaka 2005(Mwaka mmoja baada ya Kumaliza kidato cha Sita) nikabadilisha Jina Langu la Kwanza kwa taratibu zote za Kisheria nikapewa Document inayoelezea Kubadilisha kwangu Jina Kisheria inaitwa Deed Poll!!
Kwa Kutumia Deed Poll nikaweza Kubadilisha Jina hadi kwenye Pasi yangu ya Kusafiria,kwenye Mchakato wa Kitambulisho cha Kupigia Kura nikaweka Jina Langu Jipya na hata Kwenye Mchakato wa Kitambulisho cha Taifa.
Shida ni kwamba Mwaka Huu nimeazimia Kuingia Chuo Kikuu na nilipokwenda Mlimani Kuulizia nilipata wakati Mgumu sana,Academic Certificate ni Msaafu hapa Tanzania,hauwezi Kubadilishwa asilani!!
Chuo kimesema kama nikitaka Kusoma nitatumia Majina yaleyale yanayo-appear kwenye Vyeti vyangu Vya O'level na A'level vinginevyo imekula kwangu,Sasa nikawauliza Kwa nini Sheria Mama iruhusu kubadili Jina Halafu taratibu za Chuo tu zikatae? Kwamba Taratibu za Chuo ni Kuu Kuliko Sheria za Nchi maana Deed Poll ni Nyaraka ya Kisheria na Utaratibu wote wa Kisheria Umefuatwa,Pamoja na Hoja zote nilizojaribu Kuzijenga Dean of Students wa Shule ya Biashara hakunielewa,Akasema HAIWEZEKANI!!
Nina Imani kubwa na Jf,Najua Wadau wengi hapa Wana Fikra Pevu,nitafanyaje kujinasua kwenye kadhia hii,Ninawezaje kwenda Chuo kwa Jina Langu Jipya maana hata NECTA niwapigia Simu Majibu ni hayohayo,hawawezi Kubadili Jina kwenye Cheti!!
Neno hili Limekuwa Kubwa kwangu nami kwa Unyenyekevu Mkubwa ninalileta kwenu!!
Ninatanguliza Shukrani!!
======================Habari wana JF?
Mimi ni mzima wa afya tele namshukuru Mungu kwa pumzi na afya na kila ki2(all is well) hope mko pouwa, back 2 the topic! Mimi kwa jina naitwa Frank Shedrack na nimwanafunzi kwa sasa, wakuu naomba mwongozo na ushauri kuhusu kubadili jina, I declare kuwa silipendi jina langu (Frank) na niwe wazi kuwa mimi sio muumini wa majina ya kigeni, nawaombeni ushauri na mwongozo jinsi ya kubadili Jina ambalo pia lipo kwenye cheti cha kuzaliwa na taaluma.
Kiukweli katika hili sijui nianzie wapi, mwenye ufahamu kuhusu hili naomba anisaidie. I real hate my name so please help me.
ALL IS WELL....
=======================Wadau,
Jina la ukoo mimi natumia jina la baba wa kambo, tangu shule mpaka sasa niko kwenye ajira. Makosa yalifanyika mwanzo kabisa tangu niko mdogo.
Ni hadithi ndefu sitoweza kueleza hapa, kwa sasa inawezekana kubadilisha? Na kuhusu nyaraka je?
==========================Habari wa JF!
Kuna ndugu yangu anataka kubadili jina lakini yeye toka darasa la kwanza mpka chuo kikuu anatumia jina aliyo sawa kwenye vyeti vyake.
Sasa swali ni hivi, je, akibadili jina sasa hivi halitamsumbua wakati wa kutafuta kazi na kadhalika, yeye ndo amemaliza chuo kikuu mwezi uliopita.
==========================
Ni kazi rahisi sana na haina gharama ya kutisha.
Nenda kwa lawyer yoyote wa karibu yako.
Atakuchapia barua moja inaitwa "change of name deeds" au wakati mwingine inaitwa (deed pol) ambayo itaonyesha jina lako la zamani na jina lako jipya.
Na huwenda akakuuliza sababu ya kubadili jina. Na hio uliotoa ni sababu tosha. Hakikisha hio barua mnasaini wote, yaani wewe na huyo lawyer.
Gharama za hio barua isizidi shs 50,000/= Na lazima akupe original copy kama tano.
Uli moja iende kwenye passport na zingine utapeleka kazini kwako . Na zingine benki kama una account. Na zingine unaweka kwa ajili ya ushahidi.
Good luck.