anayeongea sasa hivi ni mgeni wa heshima Mahinda saburi Mahinda, anaanza na kusema SLAA sio mpinzani, aliondoka CCM kufuata cheo, kwani 1995 alimshinda Padri kikoyo kura za maoni ndani ya CCM, kamati kuu ilipomuengua akahamia CDM, lengo lake ni cheo mheshimiwa, pia hoja zote za ufisadi ziliasisiwa na Prof Lipumba, Wizi BOT, NDEGE YA RAIS, RADA yote haya yaliasisiwa na Prof Lipumba, anasema kuwa MTEI mwasisi wa chadema ni Fisadi mkubwa aliyefirisi BOT mwaka 1979 ambapo alikuwa GAVANA. Mkutanoni watu ni wengi sana na anawashika watu kweli kweli, anaielezea safu nzima ya Walioiasisi chadema. MKT-MTEI, makamu mwenyekiti- Ally nyange makani, katibu mkuu Brown ngwilulupi na Naibu katibu mkuu Edward Barongo, wakuu hotuba ni nzuri leo inanyanyambuliwa chadema